Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 127
Salaamu zangu natuma, zifike kila mahali,
Tunaziomba rehema, za Mungu zituwasili,
Hapo siku ya Qiyaama, tuwe chini ya kivuli,
Nafunga ndoa natawakali, naoa mke Muumini.
Naoa mke Muumini, nafunga ndoa natawakali,
Mke aloshika dini, na kila siku kuswali,
Hijaab ipo kichwani, afunikae wote mwili,

Sijatafuta uzuri, au yule mwenye mali,
Nimechagua tabia nzuri, alotulia akili,
Aloleleka vizuri, kidini na kiasili,

Sikumtafuta kwa haraka, nijionyeshe kamili,
Zinifikie baraka, za Mola wangu Jalali,
Nitulie kwa hakika, tabia mbaya nibadili,

Fadhila zake ni nyingi, uliza kila pahali,
Huo ndio ni msingi, wa maisha ya halali,
Ni kinga kwa mambo mengi, kwa madhambi mbalimbali,

Kuoa ni utulivu, tumeshaona dalili,
Huyaondoa maovu, na mambo huwa sahali,
Hukufanya mtulivu, shida ikikukabili,

Wajibu wangu tatimiza, tutakapokuwa wawili,
Tukikaa kuzungumza, na mambo kuyajadili,
Tutajaribu kueleza, tuelezane ukweli,

Niwe msimamizi, kwa mali na kila hali,
Ayaonyeshe mapenzi, maneno kama asali,
Katika masimulizi, sitosema kwa ukali,

Mungu atupe watoto, hao ni rasilmali,
Mke ni mama watoto, awe mwema na mkali,
Awatazame watoto, wasikuwe kijahili,

Mke ni nguzo nyumbani, kama vile matofali,
Na mume ndio rubani, huona yaliyo mbali,
Kamba ya Mungu tuishike, ibada iwe awali,

Mungu Watunze vigoli, pamoja na wanawali,
Wawe kama wa awali, kama zama za Rasuli,
Nimemaliza kauli, hapa nafunga kufuli,