Nafundisha Gitaa bure!

Michael Ngusa

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
1,637
458
Wadau,

Leo nimefanikiwa kununua Gitaa langu la kisasa kwa pesa yangu, nimefurahi sana! Nilianza kupiga Gitaa nikiwa darasa la tano shule ya msingi hadi leo nimeshamaliza chuo, nina familia...bado naendelea kupiga Gitaa! Nilifundisha kwaya nyingi sana jijini Mwanza miaka ya 2006 - 2010.

Natangaza nafasi ya bure kwa anayetaka kujifunza Gitaa. Nilifundisha wengi na leo najivunia kuwa na vijana wangu wanapiga mzigo kwenye makanisa mbalimbali jijini Mwanza na wachache hapa Dar. Kama kwako ni mbali basi utakuwa unanigharamia nauli. NiPM kama uko interested.

Hii ni Hobby nzuri sana kwangu, mke wangu akinuna tu nashika Gitaa langu...baada ya dakika kadhaa mara naona tabasamu kuuuubwa hadi raha! JIFUNZE GITAA.
 
M kinanda mkuu nataman saana kujua icho ktu

Hapo tuko pamoja mkuu, gitaa napenda sana na nnalo, tatizo nikipiga vidole vinauma huenda nakosea kushika nyuzi kama inavyopaswa.
Nimejikuta nahamishia mapenzi kwenye kinanda.
 
Uko Mkoa gani Mkuu, mimi nipo Mwanza na nahitaji sana hiyo kitu, na nina gitaa la Mzee wangu lkn hakuwa na muda wa kunifundisha
 
Dah!
Natamani sana nijue kupiga gitaa na piano! Ila mdo hivyo tena, muda na vitendea kazi.
 
Gitaa na nundu ya vidole hakuna namna upo wapi Mkuu nitaweza kweli kucharaza gitaa kama Diblo Dibala?

Mkuu umetishaaaaaa........mimi nataka nicharaze sawasawa kama Monsieur Luambo Makiadi (RIP).......
 
Wadau,

Leo nimefanikiwa kununua Gitaa langu la kisasa kwa pesa yangu, nimefurahi sana! Nilianza kupiga Gitaa nikiwa darasa la tano shule ya msingi hadi leo nimeshamaliza chuo, nina familia...bado naendelea kupiga Gitaa! Nilifundisha kwaya nyingi sana jijini Mwanza miaka ya 2006 - 2010.

Natangaza nafasi ya bure kwa anayetaka kujifunza Gitaa. Nilifundisha wengi na leo najivunia kuwa na vijana wangu wanapiga mzigo kwenye makanisa mbalimbali jijini Mwanza na wachache hapa Dar. Kama kwako ni mbali basi utakuwa unanigharamia nauli. NiPM kama uko interested.

Hii ni Hobby nzuri sana kwangu, mke wangu akinuna tu nashika Gitaa langu...baada ya dakika kadhaa mara naona tabasamu kuuuubwa hadi raha! JIFUNZE GITAA.

Niko Mwanza ningependa kuhudhuria classes zako! Vipi ulinunua ule mzigo online?
 
Hapo tuko pamoja mkuu, gitaa napenda sana na nnalo, tatizo nikipiga vidole vinauma huenda nakosea kushika nyuzi kama inavyopaswa.
Nimejikuta nahamishia mapenzi kwenye kinanda.
Rudisha mapenzi kwenye Gitaa mkuu. Moja ya faida ya Gitaa ni kwamba halihitaji umeme...muda wowote kazi tu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom