Nafuatilia Rushwa, Polisi na Mahakamani

Sophist

Platinum Member
Mar 26, 2009
4,484
3,400
Ndugu,
Hivi kesi ya Azim Dewj ya kukwepa kulipa kodi za serikali kiasi cha shs. millioni 300 iliishia wapi?
Kama nakumbuka vyema kesi hii ya mwaka 2001 haikuwahi kuhukumiwa wala kumalizwa na mahakama. Iliishia wapi, au bado inaendelea 'kupigwa tarehe'. Mwenye fununu tafadhali tufahamisheni.

Eh, na ile kesi ya madawa ya kulevya iliyohusisha watanzania waliosafirisha madawa hayo ndani ya maiti ya mtanzania aliyefia Lusaka Zambia, miaka takriban miwili iliyopita, imeishia wapi?

Wadau tutumie mtandao wa JF kufuatilia finality ya kesi hizi na nyinginezo nyingi (zitaje hapo chini), ambazo inaelekea 'zimeghubikwa na rushwa.'
 
Hizo kesi mbili zimekufa kimya kimya. Na ni kawaida sana. serikali inatumia mtindo wa kuuwa kesi kimya kimya kwa sbb inajua watz wana mtindo wa kusahau. Zakaria, yule mhindi (au sijui marabu) tajiri kuliko wote Tz aliwahi kukamatwa 2001 kwa kukwepa kodi, hadi leo kesi yake haijulikani imeishaje, na yupo mitaani anadunda.
 
Back
Top Bottom