Nafikiria kuitelekeza familia nianze maisha upya, sababu zangu ni hizi..

Fanya kile unachoona kinakufaa.

Ila kumbuka Mungu anaona haya yote.
 
Unasema tusikuonee huruma... Unafikiri hapa tunaoneana huruma au tunaambiana facts tu.

Sikiliza usitekeleze familia eti kisa na wewe ulikua bila wazazi ni ujinga tu mdogo wangu.

Kila MTU ni clever kwa nafasi yake usijione wewe ni clever kuliko wengine. Kuna vijana talented lakini wana akili za maisha kuliko wewe.

Mwisho:
 
Naona wengi wananukuu vibaya kipengele nilichosema kwamba mimi ni "Clever". Ni kwamba, apart from relationship/marriage failure I'm going through, I'm extremely talented; under the age of 23, I managed to secure 2 high profile jobs in Banks headquarters (names undisclosed)...I have a chain of man-work accomplishments ambazo hutaamini niki-unveil (and I won't do it here, it's not a proper platform)...Hapa nimeleta swala la familia nipate ushauri. FULL STOP .

YADA YADA YADA No one asked for your success story, we're not interested.

kama your so financially fit kinachokufanya ufikirie kumtelekeza mtoto ni kitu gani??

there's a difference between separating with your wife and abandoning your child!! kisa mke kakuchosha ndo unamuona mwanao hana maana!!!

.
Pia madhaifu yang nayajua fika; I'm arrogant and I have an exaggerated sense of self importance...and I can't solve these now; I'm busy with work and economic projects., na hii familia.
shameless. kwani kuwa busy na familia manake nini kama sio kujaribu kubadilisha whatever's breaking you guys apart, including your icky nasty personality.

huyo mwanamke kama anajielewa anapaswa kukushitaki kwa ustawi wa jamii ukimtelekeza mtoto.
 
Yaani wewe ni clever, una kazi kubwa bank halafu unashindwa kumtunza mke na kitoto kimoja?

Ni kazi sana ku-maintain yatima(siyo wote, bali asilimia kubwa) hakika nakuambia.

Wao kila kitu kutoka na maisha waliyopitia wameathirika kisaikolojia Siyo rahisi kuona positivity kwenye maisha especially relationship
 
Huo ni muendelezo,hata mwanao naye akijaaliwa uhai baadae naye atakuja kwenye jukwaa hili kuwauliza ambao watakuwa wajukuu zetu haya haya,ila yeye atasema baba yake alimu abandon na mama yake,to me familia ni Baraka haya ni mapitio tu,kaa chini jipange weka Imani kwa mungu unayeabudu atakuongoza na kukuvusha
 
Mpaka Umeleta Hapa Hii mada Maana imekuendesha sana kichwani,Pole kijana..

Ushauli.
i) Acha Miamuko Isiyokuwa Na Tija..
ii)Achana na kampani inayokushauli ivyo.
iii) Uliza kwa watu unao waamini wataweza kuwa Msaada kwa Hili Tatizo (Mwenye Experience na Ndoa).
Usikulupikee..Ndoa Ina mambo mengi magumu
 
sawa utafanikiwa,lakini mwanzoni ulipokuwa unafanikiwa ulikuwa na tatizo la kuponda raha,una hakika this time around hautojikuta ktk hali ile ile ya kupenda kuponda raha??kama utafanikiwa tena lakini ukaishia kulekule kuponda raha ambako unakiri uliokolewa na mkeo kupitia ndoa...hivyo basi tambua hauko salama kwako kwa maamuzi hayo!!utabadilisha tu aina ya matatizo ktk maisha yako,kutoka unaouita mzigo w kulea familia yako kwenda kubeba mzigo wa kuponda raha kutakakokuangamiza!!!
Mkuu kumbe tunaweza kuongeza product line ingine ya "marriage councelling" kwenye mambo yetu ya ushereheshaji eeh? Think about it...
 
Mkuu una tatizo kubwa.
Hapa hujaelezea matatizo ya kifamilia yanayokufanya utake kuachana na mkeo na mtoto.
Umejaribu kuelezea mafanikio yako. Hapo huna sababu ya kuachana na mkeo. Labda uelezee sababu zaidi. Ila ulizotoa hazijitoshelezi
 
Acha ubinafsi tunza familia.Wewe ni mwanaume.

Hayo ni majaribu Tu.Au unataka mwanao awe yatima Kama wewe.

Hakuna kusema umeoa umri mdogo.Mwili haudanganyi hata,pale ulipobarehe Tu mwili ulikuwa upo tayari kumrutubisha mwanamke yeyote mpevu.

Being born a male means you become a master.Masters don't run from responsibilities.
 
WanaJF,

Disclaimer: Naomba kwa mwenye kutoa ushauri asiegemee upande wowote*

Mimi ni moja kati ya vijana waliooa wakiwa na umri mdogo. Nilikuwa nina miaka 21 (now I'm 23) tu na ni kwasababu ya shinikizo la Bosi wangu aliyekuwa kama mlezi wangu kipindi hicho, maana nilimsimulia mazingira yangu ya ukuaji; ni yatima niliyekulia kwenye vituo vya watoto pia nilikuwa nimepitia hekaheka nyingi kama maisha ya mtaani, Mungu si athumani nikafanikiwa kufika chuo na kupata Fani inayoeleweka.

Kingine kilicho leta msukumo wa kuoa ni ulimbukeni wa wanawake maana nilishika pesa hivyo nikawa nafantasize maisha ya mtu mwenye hela na aliyekulia maisha ya kawaida; wazazi, shule, ndugu, marafiki, kula bata, party kila wiki, mitoko n.k. Kwahyo huwa nasema mke huyu alisaidia mimi kutulia maana pengine ningeambulia Ukimwi.

Lakini baada ya kuoa, na hata baada ya kupata mtoto 1, mambo yalianza kuniendea kombo kwa kasi na hakuna nilichofanya nikafanikiwa; iwe ni kujiajri, kutafuta kazi au kutulia kwenye jiji moja. Gharama ya kumantain familia hii na kipato cha kuyumba yumba kilifanya ugomvi usiishe ndani, afya zetu zizorote, na nikaingia kwenye ulevi mzito kuepuka stress ya kutofanikiwa kwenye malengo mbalimbali.

Sasahivi nimeirudisha familia ukweni kwa jina la likizo na mjukuu kutembelea bibi zake, na nimepata kazi mpya ambayo nikidumu nayo, inaenda kunifanya kuwa mmoja wa vijana wazito mjini...lakini sina amani kila nikifkiria gharama za familia na madhaifu ya mke k.v. kutokuwa mwepesi kuomba msamaha pale anapokosea, na ieleweke tupo Dini tofauti. Na nina mconsider "Non-submissive".

Ieleweke kuwa; nina heshimu sana harakati za kuifanya dunia a better place kwa kutozalisha mabinti ovyo, watoto wasio na malezi ya pande 2 na kutokuoa oa ovyo just bcoz u can..I BELIEVE IN FAMILY. Lakini nikiangalia umri wangu (pia watu wamekuwa wakinibeza kwa kuoa haraka vile, na wengine kukata tamaa ya kutowekeza kwangu). Maana wanaona ni kweli I'm fresh, lakini nina msalaba wa ndoa na familia.

Sasa lengo la kuomba ushauri huu, ni ili kupata tafsiri ya uamsho ambao umeanza kuota ndani yang tang wiki jana, kwamba I can forge a better life again...I can re-launch lost opportunities..she's not the first one to be abandoned, and your Son will grow on his own just as you did (did you know you'll reach this much?), Abandon the ship n.k.

Naomba usitumie huruma kunishauri, share facts, share ukweli. Maana hadi umri huu...hakuna huruma iliyowahi kunipa la maana. Mambo makubwa niliyofanikisha maishani ni kwa sababu ya "Cleverness", everybody who spends time with me, huwa anaishia kusema mimi ni kama Yakobo wa kwenye Biblia, yaani sio Extremely Smart, but I'm Extra Ordinary Clever to a point I almost can get away with anything...CLEAN.

Lengo ni kuanza maisha upya kwa kupigania ndoto za maisha yangu bila (mzigo wa) Ndoa au Familia, maana nategemea nguvu zangu mwenyewe, sina urithi sina ndugu...ni jeshi la mtu mmoja. Na mwanzoni kabla ya kuoa nilikuwa nikienda speed kali na nzuri sana.

Nawasilisha.

P.S. Mke hana shughuli, ni form 4 leaver. Nimeshajaribu kumtafutia kazi anashindwa, nikamfungulia biashara ya Hotel mtaji ukafia huko.

UPDATE:
Naona wengi wananukuu vibaya kipengele nilichosema kwamba mimi ni "Clever". Ni kwamba, apart from relationship/marriage failure I'm going through, I'm extremely talented; under the age of 23, I managed to secure 2 high profile jobs in Banks headquarters (names undisclosed)...I have a chain of man-work accomplishments ambazo hutaamini niki-unveil (and I won't do it here, it's not a proper platform)...Hapa nimeleta swala la familia nipate ushauri. FULL STOP. Pia madhaifu yang nayajua fika; I'm arrogant and I have an exaggerated sense of self importance.



something is wrong with you I think. Your past is ghosting you and your child. Hilo tu do naweza kukupa kwa haraka. Ila husisahau kuwa kuhusu kufanikiwa hutakaa ufanikiwe kwa uwazalo kufanyia familia yako. Fikiria upya.
 
Du binadamu Ni kaZi yaani umepitia maisha Ya shida na unataka Mtoto wako naye apitie. Mungu aliyejuu hatakusamehe hata kama unakazi ya high level utaishia kuwa gozi gozi tu
 
We dogo sitaki kukurembea maneno, ni hivi hacha ujinga ujinga wako huo!
 
Teh teh teh another man with a wrong woman!yaani hata baada ya hiyo miaka Mitano hutamuoa huyo yaani hujuti kuoa ila unajuta kukurupuka so mi sikushauri wewe ila nawashauri vijana ambao hawajaoa wasije wakakurupuka yaani wajiridhishe kwa kina juu ya wanachoendea na marry only for love... Ungekuwa unampenda wala usingefikiria kumwacha na kwakuwa humpendi kadri unavyozidi kukaa nae ndo damage inavyozidi so vumilia mpaka mwisho
 
Back
Top Bottom