Nafikiria kuitelekeza familia nianze maisha upya, sababu zangu ni hizi..

Joel Johansen

JF-Expert Member
May 12, 2016
242
319
WanaJF,

Disclaimer: Naomba kwa mwenye kutoa ushauri asiegemee upande wowote*

Mimi ni moja kati ya vijana waliooa wakiwa na umri mdogo. Nilikuwa nina miaka 21 (now I'm 23) tu na ni kwasababu ya shinikizo la Bosi wangu aliyekuwa kama mlezi wangu kipindi hicho, maana nilimsimulia mazingira yangu ya ukuaji; ni yatima niliyekulia kwenye vituo vya watoto pia nilikuwa nimepitia hekaheka nyingi kama maisha ya mtaani, Mungu si athumani nikafanikiwa kufika chuo na kupata fani inayoeleweka.

Kingine kilicho leta msukumo wa kuoa ni ulimbukeni wa wanawake maana nilishika pesa hivyo nikawa nafantasize maisha ya mtu mwenye hela na aliyekulia maisha ya kawaida; wazazi, shule, ndugu, marafiki, kula bata, party kila wiki, mitoko n.k. Kwahiyo huwa nasema mke huyu alisaidia mimi kutulia maana pengine ningeambulia UKIMWI.

Lakini baada ya kuoa, na hata baada ya kupata mtoto 1, mambo yalianza kuniendea kombo kwa kasi na hakuna nilichofanya nikafanikiwa; iwe ni kujiajri, kutafuta kazi au kutulia kwenye jiji moja. Gharama ya kumantain familia hii na kipato cha kuyumba yumba kilifanya ugomvi usiishe ndani, afya zetu zizorote, na nikaingia kwenye ulevi mzito kuepuka stress ya kutofanikiwa kwenye malengo mbalimbali.

Sasahivi nimeirudisha familia ukweni kwa jina la likizo na mjukuu kutembelea bibi zake, na nimepata kazi mpya ambayo nikidumu nayo, inaenda kunifanya kuwa mmoja wa vijana wazito mjini...lakini sina amani kila nikifikiria gharama za familia na madhaifu ya mke k.v. kutokuwa mwepesi kuomba msamaha pale anapokosea, na ieleweke tupo Dini tofauti. Na nina mconsider "Non-submissive".

Ieleweke kuwa; nina heshimu sana harakati za kuifanya dunia a better place kwa kutozalisha mabinti ovyo, watoto wasio na malezi ya pande 2 na kutokuoa oa ovyo just bcoz u can..I BELIEVE IN FAMILY. Lakini nikiangalia umri wangu (pia watu wamekuwa wakinibeza kwa kuoa haraka vile, na wengine kukata tamaa ya kutowekeza kwangu). Maana wanaona ni kweli I'm fresh, lakini nina msalaba wa ndoa na familia.

Sasa lengo la kuomba ushauri huu, ni ili kupata tafsiri ya uamsho ambao umeanza kuota ndani yangu tangu wiki jana, kwamba I can forge a better life again...I can re-launch lost opportunities..she's not the first one to be abandoned, and your Son will grow on his own just as you did (did you know you'll reach this much?), Abandon the ship n.k.

Naomba usitumie huruma kunishauri, share facts, share ukweli. Maana hadi umri huu...hakuna huruma iliyowahi kunipa la maana. Mambo makubwa niliyofanikisha maishani ni kwa sababu ya "Cleverness", everybody who spends time with me, huwa anaishia kusema mimi ni kama Yakobo wa kwenye Biblia, yaani sio Extremely Smart, but I'm Extra Ordinary Clever to a point I almost can get away with anything...CLEAN.

Lengo ni kuanza maisha upya kwa kupigania ndoto za maisha yangu bila (mzigo wa) ndoa au familia, maana nategemea nguvu zangu mwenyewe, sina urithi sina ndugu...ni jeshi la mtu mmoja. Na mwanzoni kabla ya kuoa nilikuwa nikienda speed kali na nzuri sana.

Nawasilisha.

P.S. Mke hana shughuli, ni form 4 leaver. Nimeshajaribu kumtafutia kazi anashindwa, nikamfungulia biashara ya Hotel mtaji ukafia huko.

UPDATE:
Naona wengi wananukuu vibaya kipengele nilichosema kwamba mimi ni "Clever". Ni kwamba, apart from relationship/marriage failure I'm going through, I'm extremely talented; under the age of 23, I managed to secure 2 high profile jobs in Banks headquarters (names undisclosed)...I have a chain of man-work accomplishments ambazo hutaamini niki-unveil (and I won't do it here, it's not a proper platform)...Hapa nimeleta swala la familia nipate ushauri. FULL STOP. Pia madhaifu yangu nayajua fika; I'm arrogant and I have an exaggerated sense of self importance.
 
tafuta njia mbadala, family is everything
ila kama imeshindikana kabisa, na kweli kabisa kwamba huyo wife imeshindikana kumbadilisha achana nae,
ila nina wasiwasi inawezekana labda kutokana na immaturity yake au yako akawa mjeuri na asie mwelewa lakini akabadilika kadri atakavyo pevuka kiakili na kimaisha,
anyway mimi naamini sana kwenye family but sio kuishi na mtu unreasonable just for the sake of family
 
sawa utafanikiwa,lakini mwanzoni ulipokuwa unafanikiwa ulikuwa na tatizo la kuponda raha,una hakika this time around hautojikuta ktk hali ile ile ya kupenda kuponda raha??kama utafanikiwa tena lakini ukaishia kulekule kuponda raha ambako unakiri uliokolewa na mkeo kupitia ndoa...hivyo basi tambua hauko salama kwako kwa maamuzi hayo!!utabadilisha tu aina ya matatizo ktk maisha yako,kutoka unaouita mzigo w kulea familia yako kwenda kubeba mzigo wa kuponda raha kutakakokuangamiza!!!
 
Ha ha bro hatutatui matatizo kwakuyakimbia, bali kuyakabiri, wala sio kuwa usipokuwa na familia ndio maisha yatakuwa mazuri. Mtoto mmoja na mke ndio familia ya kukurudisha nyuma?

Wacha habari zako kama mke ana madhaifu kwakuwa wewe ni mtoto kiumri kua kiakili mwende sawa maana nae bila shaka ni mtoto ndio maana mnashindwana au mnasigana maana kila mmoja anataka kuwa kidume ndani.

Pili kama mke wako ni jobless mtaftie biashara yake nae awe anazalisha hapo anakuwa na vijiela vyake kwa shuguli zake.

Kuteleza familia ili upate mafanikio nakuambia ni sawa na kutoa familia kafara ya kichawi uwe tajiri hutofanikiwa, na ukifanikiwa its a matter of a moment kabla hujarudi ulikotoka
 
Uliwahi mno kuoa. Tena dini au imani tofauti. Chakarika, na yeye msupport arudi shule, baada ya hiyo miaka 5 rudi kamtafute ukiona na yeye akiona inafaa kuoana basi oaneni upya lkn mkiwa imani moja. Hii ndicho ninachoweza kukushauri kwa sasa na bila kuingia sana kwenye mambo ya kiroho.
 
kuna familia zinahitaji sana maombi hii ni mojawapo yeye mwenyewe hakulelewa na wazazi ila yeye ni kwa bahati mbaya walikufa ila na yeye anataka kuacha mtt wake ateseke bila malezi ya baba kweli kunaunalolitafuta utalipata muda si mrefu.
 
You are completely wrong ndoa sio msalaba na wala sio mzigo ni hatua mojawapo tu katika maisha. Unasema huna urithi unajitegemea mwenyewe nani kakwambia kuwa na maisha bora lazima utegemee urithi? Elimu ni urithi tosha. Usitumie kisingizio cha kutokuwa na wazazi kuhalalisha ukatili na ukosefu wa ubinadamu unaotaka kuufanya. Mimi kwa nipo mid 40s lakini nilioa nikiwa early 30s wakati huohuo nikisomesha wadogo zangu. Wakati wote maisha sio rahisi kama unavyofikiri hata kidogo. Unachotaka kufanya ni kukimbia majukumu yao ya kawaida tu basi.

Ushauri wangu usiitelekeze familia yako wewe endelea kuishi nayo, kama mke ana mapungufu endelea kuvumilia huku ukimpa ushauri hatimaye atabadilika. Mimi kwa miaka karibu 13 nilikuwa kwenye ndoa siwezi kusema kwamba maisha yalikuwa rahisi tu, hapana magumu yapo lakini na marahisi na mazuri pia yapo. Maisha daima yana pande mbili.
 
Bahati mbaya Hukuwa na msingi wa kifamilia, kuna uwezekano usiweze kuthamini maisha ya binadamu mwenzako katika maisha yako yote. Unayoyaongelea hayaleti maana kwa yeyote mwenye akili timamu. Watu wanaokushauri na kukusifia mnaendana kimawazo.
 
Unahisi umemchoka mkeo?

Lakini pia jaribu kupitia hadithi hii: Watoto 100...!

Hasa pale palipoandikwa: Mzee Izadin, dereva wa bosi wetu hapa kazini, alinijibu, “Kwani mimi ndo nawalisha mdogo wangu Mentor? Mimi ni njia tu ya kupitishia riziki yao, ila mtoa riziki ni Mungu pekee

Nahisi umefikia mahali unajiona wewe ni bora sana na kwamba bila wewe mkeo na mwanao watashidika sana. Kama umeshaamua kusepa wewe sepa uone ambavyo - kama alivyofanya kwako - atatafuta tu mtu mwingine wa kuwafikishia riziki yake.
 
WanaJF,

Disclaimer: Naomba kwa mwenye kutoa ushauri asiegemee upande wowote*

Mimi ni moja kati ya vijana waliooa wakiwa na umri mdogo. Nilikuwa nina miaka 21 (now I'm 23) tu na ni kwasababu ya shinikizo la Bosi wangu aliyekuwa kama mlezi wangu kipindi hicho, maana nilimsimulia mazingira yangu ya ukuaji; ni yatima niliyekulia kwenye vituo vya watoto pia nilikuwa nimepitia hekaheka nyingi kama maisha ya mtaani, Mungu si athumani nikafanikiwa kufika chuo na kupata Fani inayoeleweka.

Kingine kilicho leta msukumo wa kuoa ni ulimbukeni wa wanawake maana nilishika pesa hivyo nikawa nafantasize maisha ya mtu mwenye hela na aliyekulia maisha ya kawaida; wazazi, shule, ndugu, marafiki, kula bata, party kila wiki, mitoko n.k. Kwahyo huwa nasema mke huyu alisaidia mimi kutulia maana pengine ningeambulia Ukimwi.

Lakini baada ya kuoa, na hata baada ya kupata mtoto 1, mambo yalianza kuniendea kombo kwa kasi na hakuna nilichofanya nikafanikiwa; iwe ni kujiajri, kutafuta kazi au kutulia kwenye jiji moja. Gharama ya kumantain familia hii na kipato cha kuyumba yumba kilifanya ugomvi usiishe ndani, afya zetu zizorote, na nikaingia kwenye ulevi mzito kuepuka stress ya kutofanikiwa kwenye malengo mbalimbali.

Sasahivi nimeirudisha familia ukweni kwa jina la likizo na mjukuu kutembelea bibi zake, na nimepata kazi mpya ambayo nikidumu nayo, inaenda kunifanya kuwa mmoja wa vijana wazito mjini...lakini sina amani kila nikifkiria gharama za familia na madhaifu ya mke k.v. kutokuwa mwepesi kuomba msamaha pale anapokosea, na ieleweke tupo Dini tofauti. Na nina mconsider "Non-submissive".

Ieleweke kuwa; nina heshimu sana harakati za kuifanya dunia a better place kwa kutozalisha mabinti ovyo, watoto wasio na malezi ya pande 2 na kutokuoa oa ovyo just bcoz u can..I BELIEVE IN FAMILY. Lakini nikiangalia umri wangu (pia watu wamekuwa wakinibeza kwa kuoa haraka vile, na wengine kukata tamaa ya kutowekeza kwangu). Maana wanaona ni kweli I'm fresh, lakini nina msalaba wa ndoa na familia.

Sasa lengo la kuomba ushauri huu, ni ili kupata tafsiri ya uamsho ambao umeanza kuota ndani yang tang wiki jana, kwamba I can forge a better life again...I can re-launch lost opportunities..she's not the first one to be abandoned, and your Son will grow on his own just as you did (did you know you'll reach this much?), Abandon the ship n.k.

Naomba usitumie huruma kunishauri, share facts, share ukweli. Maana hadi umri huu...hakuna huruma iliyowahi kunipa la maana. Mambo makubwa niliyofanikisha maishani ni kwa sababu ya "Cleverness", everybody who spends time with me, huwa anaishia kusema mimi ni kama Yakobo wa kwenye Biblia, yaani sio Extremely Smart, but I'm Extra Ordinary Clever to a point I almost can get away with anything...CLEAN.

Lengo ni kuanza maisha upya kwa kupigania ndoto za maisha yangu bila (mzigo wa) Ndoa au Familia, maana nategemea nguvu zangu mwenyewe, sina urithi sina ndugu...ni jeshi la mtu mmoja. Na mwanzoni kabla ya kuoa nilikuwa nikienda speed kali na nzuri sana.

Nawasilisha.

P.S. Mke hana shughuli, ni form 4 leaver. Nimeshajaribu kumtafutia kazi anashindwa, nikamfungulia biashara ya Hotel mtaji ukafia huko.
Kaka familia haikimbiwi...mi nadhani ni kuongea na wazazi kama wataweza kukaa na mjukuu muendeleze kidogo mkeo...course yeyote ambayo itamfungua kidogo upeo wake
msaidie katika kumuendeleza kibiashara na wewe pia ukiwa unamsaidia kumshauri maana ya ndoa ni kuwa pamoja kwa baya na zuri....
 
Bahati mbaya Hukuwa na msingi wa kifamilia, kuna uwezekano usiweze kuthamini maisha ya binadamu mwenzako katika maisha yako yote. Unayoyaongelea hayaleti maana kwa yeyote mwenye akili timamu. Watu wanaokushauri na kukusifia mnaendana kimawazo.
Duh
 
Kwanza unaonekana bado unamatitizo ya kuish maisha ya dhiki.....
Hyo fani ya maana ni ipi?ukifananisha na zingine....
Kama si kujitakia matatizo nn wakat una matatizo kuoa mke si din yako?
Nan kakwambia ukikaa mwenyewe ndio utanikiwa au ukioa umakosa baadhi ya fursa??
 
Back
Top Bottom