Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,220
Sidhani kama wasomaji wa Biblia wanatafuta ushahidi wa maandiko katika mambo ya dunia. La hasha! Wasomaji wazuri wa Biblia yaani waaminio, wanaiamini Biblia kuwa ni neno la Mungu kwa ushuhuda ulio ndani yao. Tunaleta vilinganishi hivi kwa sababu baadhi yenu mnapinga matukio katika biblia yanayokubaliana na sayansi ama historia ya mwanadamu. Hatuhitaji kuiamini Biblia kwa kusaka matukio duniani yanayoithibitisha ama la. Tunaliamini neno na kulishika basi. Na hapo tunaokoka na kukutana na Yesu mwokozi wa Ulimwengu. Basi. Mambo ya Anga, nyota, sayari Ayubu aliyasema zamani kabla ya hata Galilio Galilieo. Dunia kuwa duara yalisemwa zamani na Biblia. Mikataba ya ushirikiano imefanyika zamani sana katika Biblia. Upembuzi yakinifu umefanyika zamani sana hata enzi za Yusufu Misri. Utawala Bora ulitumika tangu ziku za Sulemani Mfalme. Sema hata Diplomasia ya Kimataifa. Matumizi ya askari wachache katika vita maalum ilitumika na kina Gideon kabla ya Jeshi la Israel kuiasili mbinu hii na kuitumia Uganda na Lebanon. Gideon aliwarejesha nyumbani wanajeshi wa Israeli zaidi ya 22,000 na kubaki na 300 tu na wakashinda vita. Usikipungukie kile ambacho Biblia imekiandika. Ikiwa hukiamini basi ni vizuri kuwaacha wanaokiamini na kukifanyia kazi waendelee maana hutaweza kukizima.
Good. Bora umesema kuwa mfuasi wa Biblia lazima awe closed mind. Ukisema utafute ushahidi na logics hutaelewa.
So, tutaipimaje KWELI katika maandiko? How can we identify the right book kama tunaishi kwa kuambiwa tuamini tu bila kutafuta shahidi za kidunia?