Nafasi za kazi jeshi la polisi

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,510
28,416
Jeshi la Polisi liko katika mchakato wa kuajiri vijana kujiunga na Jeshi kupitia mashuleni.
Tumeamua kuurudia utaratibu ambao ulikuwepo zamani wa kuajiri moja kwa moja toka mashuleni ambao ulikuwepo siku za nyuma kutokana na mahitaji halisi ya Jeshi la Polisi kwa sasa.

Hivi sasa Jeshi la Polisi linakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazotokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, ongezeko la uhalifu mpya kama vile wizi wa kutumia mtandao, usafirishaji haramu wa binadamu na kadhalika. Wahalifu wanaohusika na matukio kama hayo, wamekuwa wakitumia mbinu mpya na utaalamu wa hali ya juu.


Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na Programu yake ya maboresho. Maboresho haya yanalenga kulifanya Jeshi kuwa la Kisasa zaidi ambalo litatelekeza majukumu yake kwa Weledi huku likiwa karibu zaidi na raia katika utendaji wake wa kila siku.


Kutokana na changamoto hizo, Jeshi la Polisi linahitaji kuajiri, vijana wasomi, wenye utashi, ari na nia ya kufanya kazi za Polisi na wenye fikra na mtazamo unaoendana na dunia ya sasa.

Vijana hawa watakuwa viongozi na chachu katika kuleta mabadiliko yanayokusudiwa ndani ya Jeshi la Polisi.
[FONT=Georgia, 'Times New Roman', serif][/FONT]
A: – SIFA/VIGEZO VYA MWOMBAJI



  • Mwombaji awe Mtanzania kwa kuzaliwa.
  • Awe na afya njema iliyothibitishwa na Daktari wa Serikali.
  • Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
  • Awe na tabia njema na asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
  • Awe amemaliza Kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu.
  • Awe na umri kati ya miaka 18 na 25.


B: MASHARTI KWA MWOMBAJI
Kila mwombaji awe tayari kufanya kazi mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  • Kila mwombaji awe na ari,utashi na nia ya kufanya kazi ya Polisi.
  • Kila mwombaji aandike namba yake ya simu na anuani yake ya kudumu kwa usahihi ambayo itatumika wakati wa kuitwa kwenye usaili.

C: FOMU ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA:

Ofisi ya Mkuu wa shule
Ofisi za Makamanda wa Polisi Mikoa/Wilaya zilizo karibu
Pata fomu hapa ( sel-form )





Imetolewa na;


Ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 9141,
DAR ES SALAAM.
 
Duh! Kwa hiyo wale wa form IV hawana chao huko Police?? Hebu dadavua tena mkuu.
Make kuna ndugu yangu kabsaa,anaupenda Upolisi ajabu,lakini kamaliza Form IV mwaka 2011. Tutamsaidiaje?
 
Duh! Kwa hiyo wale wa form IV hawana chao huko Police?? Hebu dadavua tena mkuu.
Make kuna ndugu yangu kabsaa,anaupenda Upolisi ajabu,lakini kamaliza Form IV mwaka 2011. Tutamsaidiaje?
kwa nini asimalizie hiyo miaka miwili tu? unamaliza form four unaenda upolisi si utaenda kufa na bunduki begani na kutumwa tumwa tu
 
Subiri bado wapo kozi CCP wanaapa tarehe 24/06 /2016, karibu tukwepe mawe utaratibu utatolewa soon kupitia website yao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom