Nafasi za kazi 200 NARCO

Sojochris

Member
Jan 28, 2012
27
3
NAFASI ZA KAZI ZA WAKALA MAUZO “SALES AGENTS”

“Kongwa Beef” ni Nyama yenye Ubora wa Kimataifa inayozalishwa na NARCO, Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited ambayo hivi sasa inafanya maboresho ya namna ya kuwafikia wateja wake wa nyama ya “Kongwa Beef”. Ili kuhakikisha tunawapatia wateja wetu huduma zinazozidi matarajio yao, tumeamua kutoa nafasi 200 za Wakala Mauzo “Sales Agents” kwa vijana wa kike na wa kiume wa miaka 18-30. Hii ni fursa muhimu sana kwa vijana wote wenye uzoefu au wanaopenda kujenga uzoefu na kufanya kazi katika upande wa Masoko na Ujasiriamali.

Kama unashauku ya kupata nafasi ya kutafuta oda za “Kongwa Beef” kutoka kwa wateja, basi hii ni nafasi yako.

MAJUKUMU YA WAKALA MAUZO WA “KONGWA BEEF”
  • Kutangaza Ubora wa Kongwa Beef na kutafuta oda kutoka kwa wateja kwenye maofisi, mahoteli, na taasisi mbalimbali.
  • Kugawa vipeperushi na kushawishi wateja kununua “Kongwa Beef”.
  • Kukusanya na kutunza kumbukumbu za wateja na mauzo
  • Kuelimisha wateja wajue Ubora wa Kongwa Beef

MALIPO NA FAIDA UTAKAZOPATA
  • Utalipwa kwa kila kilo moja ya nyama utayoleta oda na kuhakikisha imemfikia mteja kupitia wasambazaji wetu.
  • Kadiri utakavyoleta oda nyingi zaidi na kuhudumia wateja vizuri zaidi ndivyo utakavyopata kipato ki-kubwa zaidi.
  • Utakutana na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kupata changamoto za kujiendeleza kitaaluma na kimapato.
  • Utapata mafunzo ya masoko, biashara na ujasiriamali ili kukuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
  • Vyeti vya heshima na vya mafunzo vitatolewa
  • Utapata fursa ya kuendeleza ujuzi na taaluma yako katika fani za biashara,ujasiriamali na masoko.

TAALUMA NA UZOEFU UNAOHITAJIKA
Mwombaji:-
  • Awe na uwezo mkubwa wa kutoa huduma inayozidi matarajio ya wateja.
  • Awe na uwezo wa kujieleza vizuri kwa Kiswahili.
  • Uwezo wa kuongeza Kiingereza kwa ufasaha itakua ni sifa ya nyongeza
  • Awe mwenye shauku ya kuuza sana.
  • Uwe na uwezo wa kuandaa na kutunza kumbukumbu za wateja na taarifa za Mauzo na Masoko.
  • Awe Mbunifu na Anayependa Kujiendeleza

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
  • Andika barua kwa mkono bila kuchapisha na uambatanishe “CV” yako pamoja na barua kutoka kwa wadhamini watatu (3) mmoja kati yao awe mzazi au mlezi wako. Barua ziwe na namba za simu za wadhamini
  • Ambatanisha namba za simu na anuani ya barua pepe kama unayo.
  • Ambatanisha barua kutoka kwa Serikali za Mitaa iliyogongwa Muhuri na yenye picha yako.
Maombi yote yatumwe kwa:

Meneja Mkuu,
Kampuni ya Ranchi za Taifa Ltd (NARCO),
Mavuno House, Azikiwe Street,
S.L.P 9113,
Dar es Salaam.

Simu : +255 22 211 0393/211 1956
Barua Pepe: info@narco.co.tz
Tovuti: www.narco.co.tz

Tuma maombi yako kwa kuleta mwenyewe ofisini au kwa Posta. Kila tutakapopokea maombi tutayafanyia kazi mara moja.

*********Wahi Wateja Wanatusubiri Tuwahudumie**********
 
NAFASI ZA KAZI ZA WAKALA MAUZO "SALES AGENTS"

"Kongwa Beef" ni Nyama yenye Ubora wa Kimataifa inayozalishwa na NARCO, Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited ambayo hivi sasa inafanya maboresho ya namna ya kuwafikia wateja wake wa nyama ya "Kongwa Beef". Ili kuhakikisha tunawapatia wateja wetu huduma zinazozidi matarajio yao, tumeamua kutoa nafasi 200 za Wakala Mauzo "Sales Agents" kwa vijana wa kike na wa kiume wa miaka 18-30. Hii ni fursa muhimu sana kwa vijana wote wenye uzoefu au wanaopenda kujenga uzoefu na kufanya kazi katika upande wa Masoko na Ujasiriamali.

Kama unashauku ya kupata nafasi ya kutafuta oda za "Kongwa Beef" kutoka kwa wateja, basi hii ni nafasi yako.

MAJUKUMU YA WAKALA MAUZO WA "KONGWA BEEF"
  • Kutangaza Ubora wa Kongwa Beef na kutafuta oda kutoka kwa wateja kwenye maofisi, mahoteli, na taasisi mbalimbali.
  • Kugawa vipeperushi na kushawishi wateja kununua "Kongwa Beef".
  • Kukusanya na kutunza kumbukumbu za wateja na mauzo
  • Kuelimisha wateja wajue Ubora wa Kongwa Beef
MALIPO NA FAIDA UTAKAZOPATA
  • Utalipwa kwa kila kilo moja ya nyama utayoleta oda na kuhakikisha imemfikia mteja kupitia wasambazaji wetu.
  • Kadiri utakavyoleta oda nyingi zaidi na kuhudumia wateja vizuri zaidi ndivyo utakavyopata kipato ki-kubwa zaidi.
  • Utakutana na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kupata changamoto za kujiendeleza kitaaluma na kimapato.
  • Utapata mafunzo ya masoko, biashara na ujasiriamali ili kukuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
  • Vyeti vya heshima na vya mafunzo vitatolewa
  • Utapata fursa ya kuendeleza ujuzi na taaluma yako katika fani za biashara,ujasiriamali na masoko.
TAALUMA NA UZOEFU UNAOHITAJIKA
Mwombaji:-
  • Awe na uwezo mkubwa wa kutoa huduma inayozidi matarajio ya wateja.
  • Awe na uwezo wa kujieleza vizuri kwa Kiswahili.
  • Uwezo wa kuongeza Kiingereza kwa ufasaha itakua ni sifa ya nyongeza
  • Awe mwenye shauku ya kuuza sana.
  • Uwe na uwezo wa kuandaa na kutunza kumbukumbu za wateja na taarifa za Mauzo na Masoko.
  • Awe Mbunifu na Anayependa Kujiendeleza
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI
  • Andika barua kwa mkono bila kuchapisha na uambatanishe "CV" yako pamoja na barua kutoka kwa wadhamini watatu (3) mmoja kati yao awe mzazi au mlezi wako. Barua ziwe na namba za simu za wadhamini
  • Ambatanisha namba za simu na anuani ya barua pepe kama unayo.
  • Ambatanisha barua kutoka kwa Serikali za Mitaa iliyogongwa Muhuri na yenye picha yako.
Maombi yote yatumwe kwa:

Meneja Mkuu,
Kampuni ya Ranchi za Taifa Ltd (NARCO),
Mavuno House, Azikiwe Street,
S.L.P 9113,
Dar es Salaam.

Simu : +255 22 211 0393/211 1956
Barua Pepe: info@narco.co.tz
Tovuti: www.narco.co.tz

Tuma maombi yako kwa kuleta mwenyewe ofisini au kwa Posta. Kila tutakapopokea maombi tutayafanyia kazi mara moja.

*********Wahi Wateja Wanatusubiri Tuwahudumie**********

Dah, Mkuu hii ni best Business Opportunity...mtu unakula jasho lako!! am very impressed kuona kitu kama hii ambayo ina-motivate uwajibikaji kwa sasa inatumika na govt agency! Palipo na 200 Sales Agents, lazima pawepo pia na Team Leader. Mie nasubiria hizo posts za Team Leader.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom