Nafasi ya mume. . .

Tatizo pia kuna wanawake wakishaolewa wanaanza kuonesha makucha yao. Hapo mwanaume aangalie ni upande upi wenye makosa na sio kumtetea mkewe hata kama anafanya upuuzi.

upuuzi wa mke ni kama upi?
 
AshaDii kwanini mke awe na kazi yakuangalia ndoa yake(majukumu yao,mume,watoto,nyumba yao) na pia awe na kazi ya kudeal na mawifi ambao obviously hawamtakii mema? Kwanini kaka yao asimalizane nao?

Binafsi najaribu kujiliza kama ningekua kwenye ndoa alafu ndugu zangu wakawa busy kumpa mume wangu wakati mgumu nani atakaefaa kumaliza hayo matatizo. Je nimwambie mume," ahhh we wasome tu hao alafu udeal nao" ?? Kwanini wakati mimi ndio nnaowafahamu ndugu zangu na kama isingekua mimi asingekua na mahusiano nao? Sioni kama ni sahihi. Mimi ndie ntakaewakalisha chini niwaambie waache wanayofanya.

Kuhusu "USAWA" bado sijaona unahusiana vipi na ndugu kuingilia ndoa ya ndugu yao.
 
ukitaka kujua wanawake ni viumbe vya ajabu ni hapo kwenye ugomvi wa mke na mawifi....
kila ambacho watapinga unachomfanyia mkeo ndio wao wataenda kukidai kwa waume zao....
hivi viumbe hivi lol

Hahahaha. . . ndo ujue ugomvi wenyewe hua hata hauna mantiki. Yani wanafanya tu kwasababu ndivyo walivyo.
 
Tatizo lako wewe hujaelewa bado au unakataa kuelewa bado.

Let put this way, kwenye ndoa yoyote lazima kuna up and down au vipi, ikiwa nyie mnawapa chance watu wajue matatizo yenu basi weka akilini mtailetewa tu matatizo na watu.

Kama mme anaonyesha dalili siku zote mbele za ndugu zake na wazazi wake anampenda mke wake, vipi watasababisha matatizo katika ndoa yake.???

Unless huyo mwanaume kila wakati yuko kulalamika kwao kuhusu mke wake, hata kama mke wake kachelewa kumfanyia chai basi anaenda kupiga report kwao mke wake kachelewa kumfanyia chai.

Mimi naamini wazi kabisa Mme na Mke wakiwa napendana nawako kitu kimoja nawanamaliza matatizo yao wao kwa wao, hakuna atakaye subutu kuwaleta matatizo.

Siku njema.

Ningekua nimeelewa nisingeuliza.Thanks anyway!!
 
mafahari wawili hawakai zizi moja.

Ataweazaje kucontrol familia wakati hana power as the man of the house?

Aipate wapi?
Kila siku anamwambia wote humu ndani tuko sawa, mwishowe anajidharau hata yeye.

Anasahau hata nafasi yake ndani ya nyumba.

Sidhani mwanamme anayepandwa kichwani na mkewe ana-power hata kwa hausi gelo.

Wanakuwa hawajiamini kwa lolote.

Sasa huu ni ushabiki usio na maana.

Kwan hata wakiwa sawa huo usawa unamnyima mume uwezo wa kucontrol ndugu zake? Usawa wake na mkewe unamfanya awe chini ya nduguze?

Namna watu wanavyoamua kuishi (tajiri na kijakazi, mke na mume ambao hawashindanii madaraka) haina nafasi kwenye conflict ambazo zinawahusisha watu wa nje.
 
TB, nakubaliana na TF, kuna wandugu wa mwanaume wasomi, wameoa na kuolewa, wana hela zao na nafasi mjini ila kutwa kucha wao na pua zao kwa ndugu yao! Pengine hiyo ya kukosa kazi ya kufanya!
Lizzy, tatizo sio tu kwa ndugu wa mume, nina rafiki ambaye ndugu wa mke wanamtoa jasho! Na wanakaa karibu na kwake, hawapangi jambo na mkewe kesho yake mke anageuza kibao! Tatizo kubwa liko kwenye 'kuambatana'! Mwanamke hataki kuambatana na mumewe na mwanaume hataki kuambatana na mkewe! Kama mnapanga mipango yenu wenyewe na kuitekeleza bila kushirikisha ndugu, wataanzia wapi kuwachokonoa?
 
Hahahaha. . . ndo ujue ugomvi wenyewe hua hata hauna mantiki. Yani wanafanya tu kwasababu ndivyo walivyo.

umewahi sikia ile hadithi ya mama
ambae watoto wake wawili walifunga ndoa?
mmoja wa kiume wa kwanza anaitwa michael
na wa kike anaitwa jane.........

alikuana na mtu akamuuliza watoto wako wanaendeleaje na ndoa zao?
unajua alijibu nini?

ahhh michael kapata hasara sana....mke wake hafai
kwanza mvivu,michael ameingia gharama za kuajiri housegirl...
pili anatumia pesa vibaya..kutwa kwenda kula out badala ya kupika....hafai hafai...

akaulizwa na jane je anaendeleaje???

ahh Jane kapata mume saafi sanaa
anamjali.kamuwekea housegirl wa kumsaidia kazi ..ili asichoke saana..
na mara kwa mara anamtoa Jane out na shopping...kwa kweli Jane mume kapata...lol
:biggrin:
 
mafahari wawili hawakai zizi moja.

Ataweazaje kucontrol familia wakati hana power as the man of the house?

Aipate wapi?
Kila siku anamwambia wote humu ndani tuko sawa, mwishowe anajidharau hata yeye.

Anasahau hata nafasi yake ndani ya nyumba.

Sidhani mwanamme anayepandwa kichwani na mkewe ana-power hata kwa hausi gelo.

Wanakuwa hawajiamini kwa lolote.

Kama mkiwa sawa sidhani kama kuna anaekua amemkalia mwenzake kichwani.

Hata hivyo nakubali kwamba mwanaume akishushiwa kujiamini sana anaweza akashindwa kusimamia mambo kama mwanaume.
 
Lizzy mwanamke has power over handling house issues than a man can ever have. Hio ni common knowledge na the truth, na ninaposema handling I mean vitu kama house order, Amani ndani ya ndoa kati ya watoto na wazazi na hata hio family na ndugu wa pande zoote. Ukitaka ku-prove hii kitu angalia saana in most families watoto wapo comfortable zaidi na ndugu wa mama kuliko wa baba... Do you think it Coincidence?

Lingine la msingi mwanamke (kama mke) anaweza roho imuume saana Mpenzi wake (ambae ni mume) kusumbuliwa... Kuliko dada roho itavoomuuma juu ya kakaake. Mama ndo nimuache kabisaaaa (yee anaona kamzaa hivo she has the right to any decision she makes).

Take note: Nature ya matatizo ya tofautiana.... Kuna matatizo ambayo yapo kati ya Mke na Wifi zake ambazo yeye kama mwanamke anaweza kabisa kuhimili bila kumshirikisha mume wake. Na kuna matatizo ya kuvuka mpaka ambayo yeye mwanaume inabidi adeal nayo. La msingi ambalo wewe Lizzy inabidi ujiulize ni kwa nini mawifi huleta mdomo mdomo na mizengwe miiiingi? Ukijua hilo ni rahisi saana kujua how to hit them where it hurts most.
 
Mkuu kuna wale wenye kazi zao nzuri na wana maisha yao binafsi lakini ni vurugu tupu kwenye ndoa za kaka zao I've seen that happening ndio maana nina conclude kusema kuwa ni hulka ya mtu saa zingine haijalishi kama amesoma au lah..

....Mkuu TF uyasemayo ni kweli kabisa, lakini pia mara nyingi kama mawifi shule imepanda na pia wana maisha mazuri migogoro huwa si mikubwa sana ukilinganisha na wale ambao wameishia madarasa ya chini.
 
TB, nakubaliana na TF, kuna wandugu wa mwanaume wasomi, wameoa na kuolewa, wana hela zao na nafasi mjini ila kutwa kucha wao na pua zao kwa ndugu yao! Pengine hiyo ya kukosa kazi ya kufanya!
Lizzy, tatizo sio tu kwa ndugu wa mume, nina rafiki ambaye ndugu wa mke wanamtoa jasho! Na wanakaa karibu na kwake, hawapangi jambo na mkewe kesho yake mke anageuza kibao! Tatizo kubwa liko kwenye 'kuambatana'! Mwanamke hataki kuambatana na mumewe na mwanaume hataki kuambatana na mkewe! Kama mnapanga mipango yenu wenyewe na kuitekeleza bila kushirikisha ndugu, wataanzia wapi kuwachokonoa?

Asante wifi, hapo pa kuambatana ndipo panaponisumbua mimi. Mtu utashindwaje kuwa upande wa mke/mumeo ikiwa sio yeye mwenye makosa? Eti kisa unaogopa kuonekana unachagua.Ofcourse unachagua, ungekua huchagui usingekua na familia yako binafsi.

Alafu huyo rafiki kama anaweza ahamie mbali na hao ndugu wa mke. Maana ukaribu nao ni kichochezi kibaya kweli.
 
Pamoja na mengine
Pia kuna nafasi ya malezi ya hao ndugu
kuna dada wengine hata wasomeje, umbea ni part ya maisha yao.
Hawawezi kuacha na wala hawaelezi kama ni tatizo.

mfano, kuna binti kaolewa ila dada zake wakorofi sana
na anayeongoza kwa ukorofi ni msomi, ana kampuni zake za maana na ana fweza.

Lakini bado anachunguza leo hawa wamekula nini, anavaa nguo za duka gani, mumewe mshahara wake ukoje, wamepanga nyumba ya hadhi gami?

Vitu ambavyo kwa hali ya kawaida mtu mwingine hawezi chunguza hasa ukizingatia aliyeolewa ni mdogo wake.

Hahahaha. . . ndo ujue ugomvi wenyewe hua hata hauna mantiki. Yani wanafanya tu kwasababu ndivyo walivyo.
 
umewahi sikia ile hadithi ya mama
ambae watoto wake wawili walifunga ndoa?
mmoja wa kiume wa kwanza anaitwa michael
na wa kike anaitwa jane.........

alikuana na mtu akamuuliza watoto wako wanaendeleaje na ndoa zao?
unajua alijibu nini?

ahhh michael kapata hasara sana....mke wake hafai
kwanza mvivu,michael ameingia gharama za kuajiri housegirl...
pili anatumia pesa vibaya..kutwa kwenda kula out badala ya kupika....hafai hafai...

akaulizwa na jane je anaendeleaje???

ahh Jane kapata mume saafi sanaa
anamjali.kamuwekea housegirl wa kumsaidia kazi ..ili asichoke saana..
na mara kwa mara anamtoa Jane out na shopping...kwa kweli Jane mume kapata...lol
:biggrin:

Hahahahahaha!!
Kwahiyo wakwake akiwa mtoaji TABU, akiwa mpokeaji BINGO.
 
upuuzi wa mke ni kama upi?

ni upuuzi kuonesha dharau kwa wifi na wakwe hata kama unammiliki kaka yao.
Ni upuuzi kufatilia mambo ya wifi zako wakati yako hutaki yajulikane.
Ni upuuzi kutoshirikiana na wifi zako kwa matukio kama vile ya misiba au ugonjwa.
Ni upuuzi kupenda kuishi kwa kujionesha kwa wifi zako baada ya ndoa.
Ni upuuzi kukataza mawifi au wakwe wasije nyumbani kwako.
Ni upuuzi na ukosefu wa akili vile vile.
 
. . . kwenye conflict kati ya mke na ndugu wa mume.

Kwanza nianze kwa kuuliza. .
Hivi kwa nini ndugu wa upande wa mume (mawifi, mashemeji, mama mkwe) ndio hua wanaonekana kusababisha matatizo zaidi kwa wanandoa kuliko ndugu wa mke? Hii inasababishwa na nini?

Nikirudi kwenye nilichokusudia kuandika, juzi nilikua naongea na mtu maswala ya ndoa including mahusiano kati ya mke na ndugu wa mume yanavyoweza kufanya ndoa iwe chungu ikiwa hakutakua na maelewano kati yao. Mwenyewe aliniambia kwamba "matatizo yanayosababishwa na ndugu wa mume yanatokana na mume kutokua MSIMAMO pia SAUTI mbele ya familia yake." Nilipofikiria nikaona kwamba kuna ukweli mwingi ndani yake. Embu fikiria ukiwa na mawifi wasiojua kutulia kwao, na kwako wakija ni maneno tu alafu kaka yao nae akawa anawaacha tu na kupuuza malalamiko ya mke wake nini kitatokea? Mawifi wataendelea au hata kuzidisha mbwembwe zao pale, mke atakasirika kwa kuingiliwa na mawifi + kupuuzwa na mume hivyo kupunguza au hata kuondoa maelewano kati ya mume na mke.

Wanaume nyie ndio wenye jukumu la kuhakikisha familia zenu (mama, baba,dada na kaka) wanaelewa kwamba nafasi yao ni tofauti na ya mke wako. Kwamba ukishaoa unakua na familia nyingine ambayo kwa kiasi kikubwa inatakiwa ijitegemee (uongozi na maamuzi ndani ya nyumba) hivyo hawaruhusiwi kuingilia iwapo hamjawaomba kufanya hivyo. Na inapotokea wakajaribu uwaeleze kwamba hivyo sivyo mambo yanavyoenda. Badala ya kumwambia mkeo awavumilie tu, wakalishe ndugu zako chini uwaeleze kwamba mkeo hayuko pale kwaajili yao, kama wanaona anayofanya hayawapendezi wao ilhali wewe huna tatizo nayo basi nao watafute maboma yao ili wakafanye mambo wapendavyo huko. Usiruhusu maneno maneno ya ndugu zako yamkoseshe mkeo raha, hata kama ni madogo. Ndugu zako ndio wanaotakiwa kuBEHAVE na sio mke wako KUWAVUMILIA.

Heri ya mwaka mpya. . . . natumaini utakua mzuri kwetu sote.

Nakuunga mkono kabisa Lizzy, huo ndio ukweli.
Kuongezea mawifi, I mean maadada wa mume plus mama wakwe, kaka/mwanenu akishaoa. Jitulizeni majumbani kwenu, maana utakuta kabla ya kuoa hakuna cha dada wala mama. Akioa tu kila wiki wageni "tumekuja kusalimia, oo tumekuja likizo" then mnaleta matatizo kwnye ndoa ya mkaka/mtoto.
Tulieni kwenuu
 
Lizzy mwanamke has power over handling house issues than a man can ever have. Hio ni common knowledge na the truth, na ninaposema handling I mean vitu kama house order, Amani ndani ya ndoa kati ya watoto na wazazi na hata hio family na ndugu wa pande zoote. Ukitaka ku-prove hii kitu angalia saana in most families watoto wapo comfortable zaidi na ndugu wa mama kuliko wa baba... Do you think it Coincidence?

Lingine la msingi mwanamke (kama mke) anaweza roho imuume saana Mpenzi wake (ambae ni mume) kusumbuliwa... Kuliko dada roho itavoomuuma juu ya kakaake. Mama ndo nimuache kabisaaaa (yee anaona kamzaa hivo she has the right to any decision she makes).

Take note: Nature ya matatizo ya tofautiana.... Kuna matatizo ambayo yapo kati ya Mke na Wifi zake ambazo yeye kama mwanamke anaweza kabisa kuhimili bila kumshirikisha mume wake. Na kuna matatizo ya kuvuka mpaka ambayo yeye mwanaume inabidi adeal nayo. La msingi ambalo wewe Lizzy inabidi ujiulize ni kwa nini mawifi huleta mdomo mdomo na mizengwe miiiingi? Ukijua hilo ni rahisi saana kujua how to hit them where it hurts most.

The first para hits home, no doubt about that.Ila bado haibadili the fact that YOU know your family better, na ni rahisi zaidi kwako wewe kuwaweka sawa kuliko watu ambao ni outsiders. Hivyo mimi bado naona umuhimu wa mwenye ndugu kuchukua jukumu la kuwaweka ndugu zake sawa ikiwa mwenzake hawezi/hataki.

Alafu unajua kwamba baadhi ya watu hawawezi comfrontations? Mtu kama huyu akichokonolewa atafanya nini? Mke anatakiwa kumsupport mume na mume mke, hivyo mmoja wao akiona ndugu zake wanamkosesha mwenzake raha ni jukumu lake kuwaweka sawa. Ikiwa mke anaweza kumalizana nao
SAFI, kama hawezi mume anatakiwa awajibike.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa upande mwingine
ni bora wifi mshari ambaye hajasoma kuliko aliyesoma

mtu ambaye hajasoma ugomvi wake ni wa kumwagiana maji machafu au kutunga uongo usio na kichwa wala miguu

lakini msomi, anaweza kukuangamiza kama hauko makini

halafu hata mashemeji nao
wabo baadhi wana roho hata za mawifi afadhali
tena wanamme wakiwa wabaya ni hatari sana
wanaweza fanya vitu vya ajabu zaidi

....Mkuu TF uyasemayo ni kweli kabisa, lakini pia mara nyingi kama mawifi shule imepanda na pia wana maisha mazuri migogoro huwa si mikubwa sana ukilinganisha na wale ambao wameishia madarasa ya chini.
 
Ni upuuzi kupenda kuishi kwa kujionesha kwa wifi zako baada ya ndoa.
Hus embu naomba unifafanulie hiyo maana kuna watu hata ukila nyama wakati kwake kapika maharage basi umejionyesha. Je mtu anatakiwa aishije ili asionekane anaishi kwa kujionyesha?
 
Nakuunga mkono kabisa Lizzy, huo ndio ukweli.
Kuongezea mawifi, I mean maadada wa mume plus mama wakwe, kaka/mwanenu akishaoa. Jitulizeni majumbani kwenu, maana utakuta kabla ya kuoa hakuna cha dada wala mama. Akioa tu kila wiki wageni "tumekuja kusalimia, oo tumekuja likizo" then mnaleta matatizo kwnye ndoa ya mkaka/mtoto.
Tulieni kwenuu

Hahahaha. . . kumbe safari zenyewe hua zinaanza daada ya kaka kuoa ehhh? Wanakuja kuchunguza na kumzonga wifi yao!!
 
mpaka dada waje kuleta maneno kuna jambo moja hapo
shule ndogo na kukosa kazi ya kufanya.......
ukitaka kumlinda mkeo,somesha dada zako
hakikisha wanapata kazi za maana.......
na somesha mkeo pia ikibidi........

Sio kosa la elimu, ni kosa la pato. ni umasikini tu.
 
Back
Top Bottom