Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,803
- 59,276
. . . kwenye conflict kati ya mke na ndugu wa mume.
Kwanza nianze kwa kuuliza. .
Hivi kwa nini ndugu wa upande wa mume (mawifi, mashemeji, mama mkwe) ndio hua wanaonekana kusababisha matatizo zaidi kwa wanandoa kuliko ndugu wa mke? Hii inasababishwa na nini?
Nikirudi kwenye nilichokusudia kuandika, juzi nilikua naongea na mtu maswala ya ndoa including mahusiano kati ya mke na ndugu wa mume yanavyoweza kufanya ndoa iwe chungu ikiwa hakutakua na maelewano kati yao. Mwenyewe aliniambia kwamba "matatizo yanayosababishwa na ndugu wa mume yanatokana na mume kutokua MSIMAMO pia SAUTI mbele ya familia yake." Nilipofikiria nikaona kwamba kuna ukweli mwingi ndani yake. Embu fikiria ukiwa na mawifi wasiojua kutulia kwao, na kwako wakija ni maneno tu alafu kaka yao nae akawa anawaacha tu na kupuuza malalamiko ya mke wake nini kitatokea? Mawifi wataendelea au hata kuzidisha mbwembwe zao pale, mke atakasirika kwa kuingiliwa na mawifi + kupuuzwa na mume hivyo kupunguza au hata kuondoa maelewano kati ya mume na mke.
Wanaume nyie ndio wenye jukumu la kuhakikisha familia zenu (mama, baba,dada na kaka) wanaelewa kwamba nafasi yao ni tofauti na ya mke wako. Kwamba ukishaoa unakua na familia nyingine ambayo kwa kiasi kikubwa inatakiwa ijitegemee (uongozi na maamuzi ndani ya nyumba) hivyo hawaruhusiwi kuingilia iwapo hamjawaomba kufanya hivyo. Na inapotokea wakajaribu uwaeleze kwamba hivyo sivyo mambo yanavyoenda. Badala ya kumwambia mkeo awavumilie tu, wakalishe ndugu zako chini uwaeleze kwamba mkeo hayuko pale kwaajili yao, kama wanaona anayofanya hayawapendezi wao ilhali wewe huna tatizo nayo basi nao watafute maboma yao ili wakafanye mambo wapendavyo huko. Usiruhusu maneno maneno ya ndugu zako yamkoseshe mkeo raha, hata kama ni madogo. Ndugu zako ndio wanaotakiwa kuBEHAVE na sio mke wako KUWAVUMILIA.
Heri ya mwaka mpya. . . . natumaini utakua mzuri kwetu sote.