Nadharia ya mahusiano

KipimaPembe

JF-Expert Member
Aug 5, 2007
1,285
696
Wanawake na wanaume hawapendani, bali ni maslahi huwaweka pamoja. Lakini vile vile kuna nguvu nyuma. Nguvu hiyo ni "evolutionary forces" ambazo hufanya kazi bila yeyote kupenda au kuamua - Matokeo yake mambo huwa kama tunavyoyaona.

Kimsing wanaume hupenda ngono - Evolutionary forces zimewalazimisha hivyo. Wako tayari kuuawa kwa ajili ya ngono. Ndo maana wanaume huoa ili wazidishe nafasi za kujipatia ngono. Ngono ni chombo cha uzazi. Ili binadamu waendelee kuwepo inabidi wazaliane. Mwanaume husukumwa kuzaaa maisha yake yote ndo maana siku zote wanaume hukimbilia wanawake walio katika umri wa kuzaa, hasa visichana.

Wanaume huweza kuoa wake wengi. Wanaume ndo wanaojenga familia ili kuhakikisha their offsprings (watoto wao) anaishi kwa hiyo kuendeleza vinasaba vyao (genes). Kwao nguvu za kibayolojia huwasukuma kuzaa na kulea watoto wao, haijalishi amezaa na mwanamke gani, la muhimu azae na watoto wake wakue.

Kujenga familia lengo lake ni kutoa uwezekano wa kudumu kwa kizazi chake, lakini vile vile kumwongezea uwezekano wa kupata ngono isiyo na ushindani, kwani wanaume hushindana wao kwa wao, kama males wa ng'ombe wanavyopigania nafasi ya kufanya ngono.

Wanawake husukumwa na nguvu ya kibaolojia kuzaa na wanaume tofauti tofauti ili kupata watoto wenye uwezekano mkubwa wa kukua na kuepuka uwezekano wa kuzaa watoto wenye matatizo yanayofanana. Hivyo nguvu za kibaolojia huwasukuma wanawake kupenda kuzaa na wanaume tofauti - Tatizo wanawake wanahitaji kulindwa kwani child bearing ni hatari.

Kwa hiyo ili wanawake kupata watoto kutoka kwa baba tofauti - tofauti, kutoka nje kwa siri ni muhimu. Lakini wanalazimika kuwa submissive kwa mwanaume aliyewahakikishia ulinzi - wanawake huhitaji kulindwa.

Wanawake na wanaume wote husukumwa kufanya uzinzi na nguvu zilizo nje ya uwezo wao (evolutionary forces) ila tu kwa sababu tofauti tofauti. Mwanaume hajali azae na nani provided amezaa na watoto wake wamepata nafasi ya kukua. Mwanamke hupenda azae na wanaume tofauti, tofauti, ikiwezekana kila mtoto na babake, kwani hiyo huongeza nafasi ya survival kwa watoto.

Ndiyo maana pamoja na mageti makali, pamoja na hatari ya kutoka nje ya himaya (mara nyingi adhabu ni kuuawa au kutupwa nje ya geti) bado wanawake hujikuta wakitoka nje kwa wanaume wengine. Kwa mwanamke, Mapenzi na mwanaume huisha pale anapozaliwa mtoto wa kwanza. Huko mbele, mwanamke anatafuta ulinzi tu kwa mwanaume, mapenzi hamna tena.

Ndo maana Wanawake wengi akishazaa na mwanaume huyu, mapenzi yamekwisha. Hamtaki tena, nguvu ya evolution inamsukumia kwa baba mwingine. Angalia hili, mwanamke akizaa na mwanaume kabla ya kuolewa uwezekano wa kuolewa na huyo mwanamme hushuka mno kufikia chini ya kumi kwa mia. Sababu ni kuwa yule mwanamke hamtaki huyo mwanaume tena na atafanya hiki na kile (kwa kujua au bila kujua) kuzuia kuolewa na huyo bwana.

Wanaume hujenga mageti makubwa kuzuia ushindani kutoka kwa wanaume wengine. Hujaza wanawake humo ndani ili walee wanao tu. Wanaume hutumia kila hila (family values, mila na desturi, DINI, n.k.) kuhakikisha wanawake hawatoki ndani ya himaya zao. Hata hivyo wanawake wakishapita umri wa kuzaa ni rahisi kutupwa nje ya geti, kwani thamani yake kiuzazi imekwisha.

Ndo maana uwezekano wa kupata divorce kwa mwanamke huongezeka sana umri wa kuzaa unapofika kikomo. Mwanaume husukumwa kuingiza ndani ya himaya yake (familia) mwanamke mwingine mwenye uwezo wa kuzaa (ndo source ya polygamy). Wanawake hawataki tena ngono na humuona mwanamme kama mzigo kwake.

Vile vile wanaume hutoa ulinzi kwa wanawake ili kuwa -entice- kufanya nao ngono ili hatimaye wawazalie watoto na kuwasaidia kulea.

Mwanamke ambaye umri wake wa kuzaa umepita, matumaini yake ni kwa watoto wake tu. Mme hana hamu naye na humwona kama liability. Ingawa huyu mwanamke bado anahitaji kulindwa na mwanaume, hata yeye hamtaki tena huyu mwanaume naye humwona mmewe kama liability. Anatamani atoke kwake (toka alipozaa mtoto mmoja alikuwa anatamani atoke) ila ulinzi wa kiuchumi, kijamii na kiusalama anaopata kwa mwanamme humfanya abaki pale. Wanawake wenye kipato hapa hujiondoa kwa waume kirahisi tu na kuishi kivyao vyao.

Mwanamke ambaye umri wake wa kuzaa umekwisha, hujaribu kushindana na mme kwa kuingiza dogodogo, ila anajikuta yeye hawezi, kwani nguvu ya dogodogo wa kiume hawezi kuihimili. Hata ule msukumo wa kufanya ngono haupo tena, hivyo hata huyo dogo dogo wa kiume humkimbia au huwa naye kama njia ya kumnyonya chochote alicho nacho.

Chuki na hasira ya kupoteza thamani yao, huwakusanya wanawake walioishiwa nguvu ya kuzaa katika FEMINISM MOVEMENTS (Kudai haki za wanawake) wakati wanaume zao wakichukua visichana vipya vilivyoingia kwenye child bearing age.

KWA HIYO;

Ndoa kuisha mvuto hutokea mara tu mtoto wa kwanza anapozaliwa - Mwanamke husukumwa kuzaa na mme mwingine mtoto anayefuata.

Infidelity - Wote wanaume na wanawake wako responsible kwa sababu tofauti - infidelity ipo na itaendelea kuwepo. Dini na mila zimeshindwa kwa sababu nguvu za kibaolojia ni kubwa zaidi na zinafunika.

Mapenzi - Ni wakati wa uchumba tu, hadi mtoto atakapozaliwa. Ikiwa mtoto atazaliwa kabla ya ndoa, uwezekano wa ndoa ni kidogo mno (karibia 0).

Ndoa - Wanaume na wanawake ni wadau, ila sababu ni tofauti. Ndoa zote zina migogoro ile ile (kinachosababisha ni nguvu ile ile isiyoonekana - bayolojia).

Watoto wa nje - Wanawake wanapenda kulea watoto wao tu (ila haijalishi baba ni nani). Wanaume hupenda kulea watoto wao tu (haijalishi mama ni nani). Wanaume huweza kulea watoto wasio wao kama mbinu mkakati (strategy) ya kumpata mwanamke aliye bado kwenye umri wa kuzaa. wanawake nao huweza kufanya hivyo kama strategy ya kupata ulinzi kutoka kwa mme mwenye mtoto.

Feminism - Mbinu mkakati kwa wanawake walioishiwa uwezo wa kuzaa.

YOTE HAYA HUTOKE BILA KUPANGWA. ILA BAYOLOJIA YA EVOLUTION IKO KAZINI. MUNGU WALA MILA HAVINA NAFASI!
 
nimekupata. kaaazi kwelikweli! It's good analysis anyway. Kama watu wakiwawanajua hii kabla ya kuoana nadhani kungekuwa hakuna kuoana tena hapo.
 
Haya malalamiko tunayoyaona kila siku mara oo nimetendwa, yote huwa ni ku play victim tu ili jamii imuonee huruma. Ila kila mtu yuko responsible na ana makosa yake.

Kuoa na muoe tu, ila mkishapata mtoto usione surprise mama atakapoanza kukukacha katika kila kitu huku kisingizio ikiwa eti kahamishia mapenzi kwa mtoto.

Vile vile wanaume wengi hawajui kuwa wanalea watoto wengine si wao. Ukijua hilo mapema hutaona surprise!
 
nimekupata. kaaazi kwelikweli! It's good analysis anyway. Kama watu wakiwawanajua hii kabla ya kuoana nadhani kungekuwa hakuna kuoana tena hapo.

Wanaojua vizuri suala la ndoa huliweka suala hili kwenye silence mode. Wasiojua hili la ndoa huwa wanafikiri walioweka ndoa kwenye silence mode hawajui maana ya kuanzisha familia au akili zao haziwatoshi. Uzuri kuna wanaotaka kutoka na wanaotaka kuingia, so equation ina balance
 
Eeh bwana hongera una moyo wa kutype this big unless its copy and paste
 
Madame X,
Hii naweza kuiwekea patent. It was flowing from the head. Long term observations reading from various sources na personal experiences has made that theory possible.
 
It depends sio kila kinachotokea kwa mwenzako basi kitatokea na kwako watu wameishakuwa na perception nyingi za ajabu tu ni wewe na mwenzi wako how do you sit down and solve your issues
 
kipimba pembe thax thaxxxxx very much ma dia
umenipa darasa jema na jeupe kwa ubongo wangu huu wenye wekundu juu ya kitu mahusiano
thax very much i wl prnt for the nxt use cz the theory is live n i wl use t some day some where wen braaabraaaaoccurs in ma life na au ntaisoma ili inikumbushe aya MAZITO ya ndoa
may god blesss u do more staffs like dat nxt tyme.
tangu nianze kusoma jf leo nimepata DARASA JEMA LA MAHUSIANO thou sku zngne napataga madarasa mengine...
USENGWLE BAMBO!!!!
 
Madame X,
Hii naweza kuiwekea patent. It was flowing from the head. Long term observations reading from various sources na personal experiences has made that theory possible.

This is a very good analysis Kipima pembe,....na haoja zote hapo zimesimama....hapo anayebisha alete hoja mbadala tu na sio suala la kusema eti umekopi na kupaste...keep it up


Sasa nadhani pia umwone ndugu katibu St RR na mweka hazina Asprin A.k. ODM ...najua upo chamani naturally heheheheheh...I mean tunawaaambiana hapa jamani tupunguze presha vitu vingine ni nature ilivyo,, wengine wanaelewa, wengine hawaelewi...

I wish wangesoma tundiko lote
 
kipimba pembe thax thaxxxxx very much ma dia
umenipa darasa jema na jeupe kwa ubongo wangu huu wenye wekundu juu ya kitu mahusiano
thax very much i wl prnt for the nxt use cz the theory is live n i wl use t some day some where wen braaabraaaaoccurs in ma life na au ntaisoma ili inikumbushe aya MAZITO ya ndoa
may god blesss u do more staffs like dat nxt tyme.
tangu nianze kusoma jf leo nimepata DARASA JEMA LA MAHUSIANO thou sku zngne napataga madarasa mengine...
USENGWLE BAMBO!!!!


duh...hapa kazi...Usengwile....vipi nyumbi ii bombi ii nini lol
 
theory remains theory ....needs to be put in practise to prove it...assumptions need to be challenged ....kuna ukweli ndani yake lakini 'kibailojia" uliyonukuru hapo ni shetani....na huyu shetani myama mbaya haoenekani....i have reasonable doubts kuwa bilogy is behind the evils stated...
 
OK, binadamu pamoja na viumbe wengine wote bado tuko kwenye mchakato wa evolution, tunaendelea kubadilika! Hivyo kila sheria huwa ina mahali ambapo haifanyi kazi kama ilivyo kawaida, lakini hufanya kazi katika wengi (overwhelming majority). Ni kweli nadharia inabaki kuwa nadharia mpaka ithibitike ndani ya maabara. Ni vigumu kuwaweka watu kwenye maabara, kwa hiyo nadharia nyingi zinazowahusu watu na mambo yao zimebaki kuwa hivyo; ila hali halisi inajionesha huko mitaani tunakoishi.

Kwa mfano, overwhelming majority ya wanaume wanaotembea na wake za watu, ni wanaume waliooa. Sababu yake ni "competitive mentality" ambayo iko hardwired ndani ya akili za wanaume inayokuwa driven na evolution. Kwa kujua au bila kujua, mwanaume anayechukua mke wa mtu hujiona kama mshindi (yaani kamshinda mwenye mke) na kwake ni kama kateka maeneo mapya. Ukizingatia kuwa mwanamke mwenye mme always anatafuta alternative mate (provided alishazaa na mme wake), basi infidelity inakuwa haiwezekani kuizuia kabisa!
 
OK, binadamu pamoja na viumbe wengine wote bado tuko kwenye mchakato wa evolution, tunaendelea kubadilika! Hivyo kila sheria huwa ina mahali ambapo haifanyi kazi kama ilivyo kawaida, lakini hufanya kazi katika wengi (overwhelming majority). Ni kweli nadharia inabaki kuwa nadharia mpaka ithibitike ndani ya maabara. Ni vigumu kuwaweka watu kwenye maabara, kwa hiyo nadharia nyingi zinazowahusu watu na mambo yao zimebaki kuwa hivyo; ila hali halisi inajionesha huko mitaani tunakoishi.

Kwa mfano, overwhelming majority ya wanaume wanaotembea na wake za watu, ni wanaume waliooa. Sababu yake ni "competitive mentality" ambayo iko hardwired ndani ya akili za wanaume inayokuwa driven na evolution. Kwa kujua au bila kujua, mwanaume anayechukua mke wa mtu hujiona kama mshindi (yaani kamshinda mwenye mke) na kwake ni kama kateka maeneo mapya. Ukizingatia kuwa mwanamke mwenye mme always anatafuta alternative mate (provided alishazaa na mme wake), basi infidelity inakuwa haiwezekani kuizuia kabisa!

Asante kwa kuweka nadharia hii hapa tena kwa lugha nyepesi maana waliochanganua hii nadharia akina Darwin kwenye miaka ile ya 1880's na nadharia ya sexual selection na evolution walifafanua vizuri tu ila ndio hivyo siyo wengi wameipitia na kuidadavua kuiweka katika lugha nyepesi. Kwa kifupi ulichosema ndicho kinachopelekea utata mwingi kwenye mahusiano na hata behaviours za wanawake na wanaume. Umeniacha hoi ulipooanisha na Feminism. Hapo sijui kama nakuunga mkono lakini ni jaribio zuri.
 
aiseeee,sasa naanza kuwaza kuahirisha ndoa badala ya february iwe japo june ili kutafakari hii nadharia
 
Back
Top Bottom