NACTE wametoa majina waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu

SOCIETY'S FOCUS

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
424
490
NACTE walimu angalieni profile zenu

MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VYA UALIMU


  1. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na kozi mbalimbali za Ualimu kwa ngazi ya Stashahada na Stashahada ya Juu kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Kikao cha Pamoja cha Udahili (Joint Admission Committee on Teachers Education) kilichofanyika tarehe 15 Oktober 2015 na kukutanisha Uwakilishi wa Wizara, Baraza (NACTE), wakuu wa vyuo vinavyotoa Mafunzo ya Ualimu na wadau wengine washiriki kiliidhinisha uteuzi wa awali ambapo waombaji 8544 kati ya 14470 wameteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali.
  2. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji na pia yatatangazwa moja kwa moja na vyuo husika kwa wale waliopitia kwenye "institutional panels". Matokeo ya jumla yanapatikana pia katika tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (www.nacte.go.tz)
  3. Waombaji wote ambao wamechaguliwa katika awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na mwisho wa kuthibitidha ni Ijumaa tarehe 30 Oktoba 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha, nafasi hiyo itatolewa kwa mwingine.
  4. Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo, kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu za kutopangiwa chuo katika awamu hii na maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu ya pili siku ya Jumatatu 26 Oktoba 2015 idadi kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo kwani hadi sasa nafasi zipatazo 14548 hazijajazwa.

Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTE)
20 Oktoba 2015

 
Nahiji kwenda kusoma lakini kila nikiangalia profile yangu hakuna chochote. Nimeapply kwenda diploma ya Ualimu. Ama wezangu mmeshapokea selection za vyuoni?
 
Mbona kuna thread hapa imeonyesha post zenu za diploma tayari zimeachiwa,hebu jaribu kupitia kwenye web ya nacte
 
Funguka vizuri hueleweki

ingia kwenye website ya www.nacte.go.tz utaona update waliyotoa leo inawahusu mlio omba ualimu matokeo tayar na mwisho wa kudhibitisha kua utafika chuon ni tar 30 oct usipo fanya hivyo nafasi inachukuliwa na mtu mwingne. kwa maelezo zaid nitafute 0753440127
 
wale walio chaguliwa na chuo cha ustawi naomba msaada wa kukamilisha usahili na kufanya malipo ya ada
 
Back
Top Bottom