Nachukua kadi ya CCM sababu nimeamua kuwa FISADI, Kwani ukiwa mpinga ufisadi, utakufa masikini

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Nimeaua kuchukuwa kadi ya CCM ili nianze rasmi UFISADI. Najua bila kuwa mwanachama naweza kwenda kunyea debe kwa urahisi zaidi. Siwezi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya UFISADI wakati nafasi yangu inaniruhusu kuwa FISADI. Bosi wangu FISADI, wafanyakazi wa chini yangu hawalazi damu. Nao ni MAFISADI, wafagiaji wa ofisi, MAFISADI. Wenzangu wengi nimeanza nao kazi pamoja, mishahara yetu inalingana, lakini kila nikiwatizama nakuta kuwa ni matajiri wakubwa huku familia zao zikiishi maisha ya raha mustarehe tena kwenye majumba makubwa ya kifahari, wanashindana kununua magari ya thamani kubwa. Mimi naishi kwa kutegemea mshahara tu kwa kisingizio eti mwanaharakati wa kupinga UFISADI wakati ninayo nafasi ya KUFISADI kama wenzangu. Huu ni upuuzi mtupu, upuuzi kwa sababu UFISADI ndiyo mfumo maalumu wa maisha ya sasa. UFISADI ni mtoto wa ubepari. maisha ya usawa huu bila ya kuwa FISADI. Hakuna maendeleo. Natangaza rasmi kuwa, sasa naanza UFISADI. Naamini wale mlio na uchungu wa maisha mtaniunga mkono.
 
Hata hiyo ada ya mwaka utakayokuwa unalipia kadi yako itaishia kwa MAFISADI !
 
:shock:, unayo haki kufanya hivyo. ata vile hujawahi kuwa na kadi ya chama chochote bali wewe ni CCM tangu mwanzo. :mvutaji:
 
Namie ntafutie basi kadi mbili za ccm, nisaidie pia na bendera ya ccm, nataka kufungua biashara sehemu isiyoruhusiwa, nikiweka bendera na kibao Shina la wakereketwa wa ccm limefunguliwa rasmi na nape hamna atakaye nikamata,

najamaa yangu naye anauza bangi na bwimbwi kwenye mtaa karibu na mahakama ya mwanzo arusha, anataka kadi na bendera ili kulinda biashara yake.
 
Back
Top Bottom