Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 264
Jamani Babu wa Loliondo kumbe anaongoza kwa kuwa Nabii wa Uongo Afrika Mashariki Nzima? Wakina Mrema, na Wanasiasa wengine waliomfagilia wako wapi?
Jamani Babu wa Loliondo kumbe anaongoza kwa kuwa Nabii wa Uongo Afrika Mashariki Nzima? Wakina Mrema, na Wanasiasa wengine waliomfagilia wako wapi?
Mkuu acha hizo wengine tumepoteza watu muhimu sana kutokana na huyu mzee. yaani siwezi hata kusimulia tena kwa hiyo hiyo kisukari waliacha dawa ya Hospital kisha walipokufa mzee akasema hakuwaambia waache dawa ya Hospital.. Sasa ponya gani ambayo bado mgonjwa ataendelea na dawa za Hospital tena baada ya muda wa mwaka na wamekufa kwa maradhi hayo hayo..Tumeuliza vipi kulikoni tunapewa jibu hata Muhimbili wagonjwa hufa! - Aliyekufa hakupona jamani..kuna watu nawafahamu kabisa ambao wamepona Kisukari. Labda utapeli wenyewe ni kwa wale waliomtumia!!
Mkuu acha hizo wengine tumepoteza watu muhimu sana kutokana na huyu mzee. yaani siwezi hata kusimulia tena kwa hiyo hiyo kisukari waliacha dawa ya Hospital kisha walipokufa mzee akasema hakuwaambia waache dawa ya Hospital.. Sasa ponya gani ambayo bado mgonjwa ataendelea na dawa za Hospital tena baada ya muda wa mwaka na wamekufa kwa maradhi hayo hayo..Tumeuliza vipi kulikoni tunapewa jibu hata Muhimbili wagonjwa hufa! - Aliyekufa hakupona jamani..
Kifo hakihusiani na ubora au udhaifu wa dawa na kupona pia hakuhusiani na dawa bali kiwango cha ugonjwa, uwezo wa mwili kusharabu dawa na utayari wa mgonjwa mwenyewe kupambana na ugonjwa unaomkabili. Mahospitalini kuna Mochuwari za kazi gani kama dawa kazi yake ni kuzuia kifo? Mimi nina watu zaidi ya sita ambao walikuwa ni wagonjwa taabani wa Kisukari na wote hao hivi sasa wanadunda mitaani wakiwa na kiwango kinachohitajika cha sukari.Mkuu acha hizo wengine tumepoteza watu muhimu sana kutokana na huyu mzee. yaani siwezi hata kusimulia tena kwa hiyo hiyo kisukari waliacha dawa ya Hospital kisha walipokufa mzee akasema hakuwaambia waache dawa ya Hospital.. Sasa ponya gani ambayo bado mgonjwa ataendelea na dawa za Hospital tena baada ya muda wa mwaka na wamekufa kwa maradhi hayo hayo..Tumeuliza vipi kulikoni tunapewa jibu hata Muhimbili wagonjwa hufa! - Aliyekufa hakupona jamani..
Mkuu wangu hata wewe?... Mtu yeyote anayekufa kwa ugonjwa fulani ina maana hakupona ugonjwa ule. Sasa ukinambia kwamba waliokufa siku yao imefika hali wamekufa kwa ugonjwa waliofikiri wamepona baada ya kunywa dawa na babu, hapo tena inakuwa kufuru kwa Mungu . Hao jamaa zako wanaodunda hawakuwa na kisukari bali Depression ambayo ilihitaji tu imani..Ni ugonjwa mkubwa sana sasa hivi Afrika lakini bado watu hawajagundua hilo.Kifo hakihusiani na ubora ua udhaifu wa dawa na kupona pia hakuhusiani na dawa bali kiwango cha ugonjwa, uwezo wa ,mwili kusharabu dawa na utayari wa mgonjwa mwenyewe kupambana na ugonjwa unaomkabili. Mahospitali kuna Mochuwari za kazi gani kama dawa kazi yake ni kuzuia kifo? Mimi nina watu zaidi ya sita ambao walikuwa ni wagonjwa taabani wa Kisukari na wote hao hivi sasa wanadunda mitaani wakiwa na kiwango kinachohitajika cha sukari.
Hata hivyo pole kwa kuondokewa na wapendwa wako!!
Kwanza Mkandara mimi sijasema kwamba "siku yao ilikuwa imefika" bali hoja yangu uponaji hutegemea mambo mengi sana na siyo dawa peke yake. nakubaliana kwamba inawezekana hao ninanowafahamu mimi sukari yao ilisababishwa na "depression" lakini kuna hoja naijua hata kwa wale wanaopenda kwenda kuombewa au kupungwa mashetani, wote kuna kitu kinawasukuma wao binafsi kwenda huko.Mkuu wangu hata wewe?... Mtu yeyote anayekufa kwa ugonjwa fulani ina maana hakupona ugonjwa ule. Sasa ukinambia kwamba waliokufa siku yao imefika hali wamekufa kwa ugonjwa waliofikiri wamepona baada ya kunywa dawa na babu, hapo tena inakuwa kufuru kwa Mungu . Hao jamaa zako wanaodunda hawakuwa na kisukari bali Depression ambayo ilihitaji tu imani..Ni ugonjwa mkubwa sana sasa hivi Afrika lakini bado watu hawajagundua hilo.
Inakuwaje mtu aliyeuawa ahukumiwe aliyeua ikiwa siku ya huyo mtu alokufa ilisha fika?.. Jamani hizi imani zenu za dini msiziingize ktk maswala haya tunashindwa hata mjadala.
gaziti gani hilo?
Mkuu wangu ndio maana nikasema usilete habari za imani yako ya dini ktk swala hili la kisayansi tutashindwa hata kujadili mada hii. Kisayansi tunasema tu kwamba mtu yeyote anayekufa kwa ugonjwa fulani ina maana mtu huyo hakupona ugonjwa ule hata kama alitibiwa. Hata hayo madawa tunayopewa Hospital na mtu asipone akafa ina maana dawa hiyo haikuweza kuponya ungonjwa huo ndio maana mtu huyo kafa kwa ugonjwa huo..Kwanza Mkandara mimi sijasema kwamba "siku yao ilikuwa imefika" bali hoja yangu uponaji hutegemea mambo mengi sana na siyo dawa peke yake. nakubaliana kwamba inawezekana hao ninanowafahamu mimi sukari yao ilisababishwa na "depression" lakini kuna hoja naijua hata kwa wale wanaopenda kwenda kuombewa au kupungwa mashetani, wote kuna kitu kinawasukuma wao binafsi kwenda huko.
Mimi ni mgonjwa lakini sikufunga safari kwenda Samunge kwa sababu sikuwa naiamini dawa yake, lakini kwa wale wenye kuamini walikwenda. Na lazima tukubaliane kwamba Babu hakuwa anatoa kinga ya kuzuia ugonjwa kurudia bali alikuwa anatoa "tiba' kwa wenye kuamini. Kitu pekee ambacho tangu mwanzo nilikikataa kuhusu babu ni pale alipodai kwama dawa yake inatibu magonjwa yote!!