Naanza kumkubali Naibu Spika Ndugai....

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,091
Nimekuwa nafuatilia vikao vya bunge kwa kipindi sana hasa katika bunge hili lililoanza mwaka 2010 ambalo limekuwa linakaribiana na changamoto kubwa nadhani kuliko mabunge yote yaliyowahi kutokea. Katika hali hii uongozi imara ni jambo kubwa kabisa lilikuwa linahitajika ambapo wote mtakuwa mashahidi kwamba ulionekana kutokuwepo katika vikao vya mwanzo vya bunge hili.

Hali naona kama imeanza kurekebika kidogo hasa kwa Naibu Spika ambaye naona kadri siku zinavyokwenda amekuwa akibadilika kwa mtazamo chanya kiasi cha kuanza kuaminiwa kwa uongozi wake. Napenda nikiri kwamba kwa Spika mwenyewe bado hajaonyesha hivyo na pia kwa wenyeviti (Hasa yule mwenyekiti ambaye mara zote akiongoza anaondoka na balaa)

Kwa ufupi napenda niseme kwamba naanza kumuamini naibu spika na nakuwa na imani ya kikao kwenda salama pale anapokuwa anaongoza bunge

Ni mtazamo wangu tu................
 
Tabia za nchi masikini ndo kama hii.Viongozi awapendi kujadili matatizo wa wananchi wao,Tumbo mbele kwa kila kitu
Toa mfano kipi naibu spika kafanya cha kuwanufaisha wananchi.?
 
Tabia za nchi masikini ndo kama hii.Viongozi awapendi kujadili matatizo wa wananchi wao,Tumbo mbele kwa kila kitu
Toa mfano kipi naibu spika kafanya cha kuwanufaisha wananchi.?
Kuna kitu kinaitwa logic, siku serikali inatoa taarifa juu ya mgomo wa madaktari bungeni ni yeye aliyesema hapana tumesikiliza upande mmoja tu wa kwenu so tunataka kujua upande wa pili. Kwa kawaida naamini kwamba kama angekuwa spika pale angesema na iwe kama mlivyonena lakini alisema hapana before we discuss it hebu tupate taarifa ya pande zote then ndio tudiscuss.

Hilo ni moja tu
 
Tabia za nchi masikini ndo kama hii.Viongozi awapendi kujadili matatizo wa wananchi wao,Tumbo mbele kwa kila kitu
Toa mfano kipi naibu spika kafanya cha kuwanufaisha wananchi.?

Kitendo cha kukubali muongozo na kutoa maamuzi kwa busara, alafu nimegundua kumbe spika Anna Makinda ana hasira sana.!
 
Ni kweli, Ndugai ameanza kuonyesha misimamo na maamuzi magumu pale inapolazimu.... amenifurahisha jinsi alivyojibu muongozo wa mgomo wa madaktari leo..... ngoja tuone kitakachoamuliwa.
 
Kanifurahisha sana pia alipotoa wito kwa madaktari kwa niaba ya speaker na bunge kwa ujumla kwamba wanaombwa kurudi kazini na ana imani kuwa masuala yao yanashughulikiwa ipasavyo na serikali. Nami pia naunga mkono wito huu na kuwaomba madaktari wawe na huruma kwa wananchi wenzao.
 
kama kweli unamuaminia mbona leo kashikwa kigugumizi cha kuruhusu hoja ya madokta kujadiliwa!? Hana lolote, wote ni walewale tu. anatafuta gia ya kumchomoa bi K kwenye kiti cha u spika.
 
Kengemumaji, hao madaktari hawawezi kurudi kabla waziri mkuu hajafuta usemi wake, cha muhimu tumuombe waziri mkuu afute usemi halafu tuwaombe madaktari warudi. Au kauli ya waziri mkuu ya kujifukuzisha kazi ilikuwa ni utani?
 
Kuna kitu kinaitwa logic, siku serikali inatoa taarifa juu ya mgomo wa madaktari bungeni ni yeye aliyesema hapana tumesikiliza upande mmoja tu wa kwenu so tunataka kujua upande wa pili. Kwa kawaida naamini kwamba kama angekuwa spika pale angesema na iwe kama mlivyonena lakini alisema hapana before we discuss it hebu tupate taarifa ya pande zote then ndio tudiscuss.

Hilo ni moja tu

Ndugai kasema maombi 6 ya wabunge yameendelea kukiomba kiti cha spika na hali kweli si shwari hivyo ni vema sasa kutafuta njia mbadala haraka ikiwa ni pamoja na kujadili bungeni.
 
2015 atakuwa spika kwakuwa makinda atakuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke!!
 
Kitendo cha kukubali muongozo na kutoa maamuzi kwa busara, alafu nimegundua kumbe spika Anna Makinda ana hasira sana.!

Hana hasira yule ni diffencive mechanism kukwepa changamoto, yule uwezo wake ni mdogo sana, wee tangu lini Uspika sifa yake kuu ikawa jinsia?? katika hili Kikwete na wenzanke hawakututendea haki watanzania kwasababu sisi tulitaka spika na siyo mwanamke.
 
Hapana anatumi hasira kuficha ujinga wake, na uwezo mdogo wa kiuongozi alionao.

kwa suala la madaktari mama amejitahidi kupunguza hasira. Nilimsikiliza kwa makini sana jana. Binadamu hawezi kuwa yuleyule kwa kila agenda.
 
Hapana anatumi hasira kuficha ujinga wake, na uwezo mdogo wa kiuongozi alionao.

Wajinga wote wanatumia mbinu hii.....lazima kautishe kwa ukali , ili uwe bize kumshangaa na kusahau point yako unayoisimamia kwa ujumala anakupoteza maboya mwisho wa siku unakuwa umeshindwa kumbaini ujinga wake!
 
kama kweli unamuaminia mbona leo kashikwa kigugumizi cha kuruhusu hoja ya madokta kujadiliwa!? Hana lolote, wote ni walewale tu. anatafuta gia ya kumchomoa bi K kwenye kiti cha u spika.
Unajua kuna vitu viwili hapa ambavyo kwa wabunge inabidi wawe very clear kabla ya kuanza kudiscuss hiyo, kuna taarifa ya waziri je hiyo ya madaktari itatoka wapi ili wanapojadili wawe wanafanya comparison? Logic inakataa la sivyo tungeishia kwa wabunge wengi kuambiwa wathibitishe wanayoyasema
 
Back
Top Bottom