Najuta Kukufahamu
Member
- Feb 29, 2012
- 54
- 17
Pole mwanangu.
Ninakushauri uandike barua kwa ufupi tu ya kuomba kazi. Tengeneza CV yako safi kabisa na usisahau kuweka referees wakuaminika watatu. Ambatanisha na vyeti vyako (IV, VI na chuo). Jitahidi upate address za mabenki yafuatayo: CRDB, NMB, NBC, AKIBA COMMERCIAL BANK, STANBIC, STANDARD CHARTERED BANK, EXIM.
Hakikisha unapeleka barua, CV na vyeti kwa mabenki yote haya. Kisha potezea kabisa na uendelee na shughuli nyingine. Utashitukia unaitwa kwenye Interview hata kama ni baada ya mwaka mmoja. Hakikisha unaweka contacts zako ambazo hazina utata haswa simu. Mara nyingi hawatumi barua, bali wanakupigia simu ya mkononi. Hizi Bank hawatangazi nafasi za kazi hata siku moja. Wanaita wale walioomba ambao tayari wana docs zao nilizotaja hapo juu.
Binti zangu wawili wamepata kazi CRDB kwa mtindo huu. Infact CRDB walikuwa na Interview ya watu almost 300 wiki mbili zilizopita na wameajiriwa wengi tu bila upendeleo hata chembe, including mabinti zangu. Nasikia Interview nyingine itakuwa mwezi wa saba. Nakutakia kila la heri na Mungu akutangulie mwanangu.
Mabenki na taasisi nyingi za fedha na za kimataifa huwa hawaajiri direct..wanatumia recruiting agencies..cha msingi ni yeye kuweza kutuma CV yake kwa agency mbali mbali kama Erolink, Proffesional Approach etc..hilo ndio litakalo mtoa kutoka kijiweni..otherwise itaendelea kula kwake.