NAANDIKA DISSERTATION/RESEARCH REPORTS/PROPOSAL/Conference PAPERS

Mjini shule.....usipouelewa huu ujumbe wa huyu "MR DISSERTATION/RESEARCH REPORTS/PROPOSAL" Huwezi kusema kwamba umefuzu elimu!
 
Vilaza wengi humu sijawahi ona
Pole sana, swali langu umelichukulia juu juu. Ungelitafakari na ungejijua wewe ndio kilaza mara dufu. Sasa nikufafanulie kwa mimi nikifikia stage ya kuandika abstract maana kazi ya kuandika sehemu kubwa ya ripoti imeisha au tayari nimekuwa nimeshaandika research summary ambayo nitaitumia kuandika abstract. Sasa kama unaweza kuandika abstract kwanini ushindwe kuandika ripoti. Tafakari ndugu yangu. Ingawa kama jamaa yupo tayari kusaidia watu poa tu, maana sio kila mtu ana uwezo/ au uwezo hutofautiana.
 
blessing mtu asikukatishe tamaa endelea na mwendo huo huo. kiukweli TZ inahitaji watu wa aina yako fikiria Lecturer wa UDSM uki-mgoogle hukuti publication yoyote ya Kitaaluma mfano CHRIS MAUKI anajiita Mhadhiri wa UDSM lakini uki-mgoogle hana publications yoyote maana akili yake yote ameielekeza kwenye u-MC wa kitchen party, kipaimara/ubarikio na SEGERE na kwenye malavidavi wahadhiri TZ badilikeni.
 
Florence Majani
WAKATI Serikali na wadau wa elimu nchini wakifanya jitihada ya kuongeza idadi ya wahitimu wa shahada huku kampuni zikitoa vipaumbele kwa wenye sifa hizo, imebainika kuwa asilimia 80 ya shahada hizo si halali. W

alakini wa shahada hizo, umebainika kupitia utafiti uliofanywa na Dk Eliamani Sedoyeka wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar es Salaam. Katika utafiti huo, mhadhiri huyo, amebaini kuwa wahitimu wengi ama wameiba au wamenakili tafiti zao za mwisho kutoka katika tafiti za watu wengine au kwenye mitandao. Mtaalamu huyo wa Kitengo cha Hesabu na Mfumo wa Mawasiliano, alisema tatizo hilo ni kubwa na linaendelea kukua siku hadi siku. Kwa mujibu wa Dk Sedoyeka, baadhi ya wahitimu wanafanyiwa tatizo hizo na kampuni na wahadhiri wa vyuo. Alisema wengine wamekuwa wakipata alama za juu kwa kuibia kwenye mitihani yao.

Dk Sedoyeka ambaye amefanya utafiti kuhusu sababu za wanafunzi kunakili shahada na kuibia katika mitihani yao, alisema asilimia 80 ya shahada hasa za kwanza pili na shahada za juu zina walakini mkubwa. Alisema tatizo hilo limechangiwa na kukosekana kwa uwiano kati ya idadi kubwa ya wasomi na maendeleo ya nchi. Mhadhiri huyo alisema Serikali inawekeza katika kuzalisha wasomi wengi kwa kutoa mikopo ya elimu ya juu, bila kuangalia ubora na matokeo ya wasomi hao katika maendeleo.

“Serikali inatakiwa iliangalie suala hili kwa upana kwa sababu tutaendelea kuzalisha wasomi wengi wasiokuwa na tija kwa maendeleo ya taifa,” alisema Dk Sedoyeka. Sababu za wanafunzi kununua au kunakili shahada? Dk Sedoyeka alisema sababu zinazochochea tatizo hili ni wanafunzi kutojituma, matatizo ya kisaikolojia na upungufu wa wahadhiri. Alisema wahadhiri wachache wanaokuwepo vyuoni, wanasongwa na kazi nyingi na hivyo kushindwa kuwasimamia vyema wanafunzi.

“Mwanafunzi anapofanya ‘research yake’ tunategemea atumie ujuzi wake aliojifunza kwa miaka mitatu au minne. ‘Research anayoifanya itatuonyesha kama yuko tayari kufanya kazi au la,” alisema Dk Sedoyeka. “Anasema mwanafunzi anaponunua ‘research’ au kufanyiwa au kuiba ya mtu hawezi kuwa nguvu kazi yenye tija,” alisisitiza. Alisema kingine kinachochangia kuwapo kwa shahada mbovu i ni wahadhiri wenyewe. Dk Sedoyeka alisema wingi wa vyuo umesababisha kuajiriwa kwa wahadhiri ambao baadhi yao hawana ujuzi wa kina katika kuwasimamia wanafunzi kwenye tafiti zao.

“Huwezi kumsimamia mwanafunzi katika ‘dissertation’ wakati wewe mwenyewe hukuifanya vyema na hufanyi tafiti yeyote katika maisha yako,” alisema Anasema kinachosababisha shahada nyingi kuwa feki ni kitendo cha kununua au kuiga kugeuka utamaduni wa watanzania.

“Aghalabu mwanafunzi anasema, kama wengine wanaiba, wananunua na wanaiga, kwa nini na mimi nisifanye hivyo, Kwa kifupi mfumo umeoza,” alisema. Anasema hata kama chuo kinahitaji wanafunzi wengi wafaulu, lakini taaluma inabaki kuwa taaluma na wanachuo wanatakiwa wafaulu kwa uhakika na si kuwalipua kisha kuwatupa duniani wakiwa hawawezi kufanya lolote. Jambo lingine linaongeza kasi ya shahada feki, ni mabadiliko ya siku za karibuni ambapo shahada za juu zinakuwa kigezo cha kupata ajira. Dk Sedoyeka ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Usimamizi wa Takwimu, Data na Mipango alisema kinachosababisha tatizo hili kukua kwa kasi ni ari ya vijana kupata elimu kunakoambatana na sheria dhaifu.

“Katika nchi zilizoendelea, hata kama ni mbunge, waziri au mwenye cheo kikubwa akibainika kuwa matokeo yake ya kitaaluma yana walakini anaachia ngazi,” alisema.

Anasema tafiti za mwisho za mwanafunzi zina umuhimu mkubwa kwani anapofanya tafiti hizo anajengwa katika kuibua tatizo, kulidhibiti na kulitafutia ufumbuzi. . Mhadhiri huyo anasema aliufanya utafiti wake kuanzia Juni 2011 katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee na kukamilisha sehemu ya kwanza.

Sasa yupo katika hatua ya pili itakayoangalia tatizo hilo kisaikolojia na kitabia. Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Tumaini Dare s Salaam, Godwin Gondwe alisema anakubaliana na utafiti wa Dk Sedoyeka na kwamba hiyo ni moja ya changamoto katika sekta ya elimu nchini. Gondwe ambaye ni Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano ya Umma alisema chanzo kikuu ni mfumo mbovu wa elimu tangu awali ambapo wanafunzi wengi wanasumbuliwa na lugha ya kiingereza.

Alisema sababu nyingine ni wahadhiri kuwasimamia wanafunzi wengi katika tafiti zao, jambo ambalo wakati mwingine linachangia wanafunzi kufanya vibaya. Mhadhiri huyo alisema Tanzania haina budi kuwa sera ya elimu itakayosimamia ubora na mwelekeo wa elimu nchini, ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia katika kuzipima tafiti za wanafunzi. “Tutunge sera ambazo zitasimamia sekta ya elimu kuanzia ngazi ya chini kabisa, ili wahitimu wawe na tija,” alisema Gondwe.

Hata hivyo Gondwe alisema pamoja na utafiti huo kuonyesha asilimia kubwa ya shahada zina walakini, bado Tanzania ina wasomi ambao ni lulu katika nchi za jirani, kama Kenya, Rwanda na Burundi.

Aliitaka serikali kuwekeza katika elimu ikiwemo kuweka fungu la kutosha kwa ajili ya kufanya tafiti. Dk Nandera Mhando, Mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitengo cha Sosholojia alisema amekutana na changamoto za wanafunzi kunakili tafiti zao mara kwa mara. Alitoa mfano kuwa mwaka jana aliwapa sifuri wanafunzi karibu kumi ambao walinakili tafiti zao.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa, alipotafutwa kwa njia ya simu hakuweza kupokea simu yake huku Naibu wake, Philip Mulugo akisema kuwa yupo mkutanoni na kuwa hawezi kuzungumza kwa wakati huo.

Utafiti uliofanywa na mwandishi ulibaini uwepo wa watu ambao hujipatia riziki kwa njia ya kuwafanyia wanavyuo tafiti. Mwandishi alizungumza na Kijana mmoja (jina linahifadhiwa),ambaye kazi yake ni kuwafanyia wanavyuo tafiti na aliahidi kuifanya tafiti hiyo kwa malipo ya shilingi laki tano kwa tafiti ya shahada ya uzamili. Kijana huyo alianza kwa kuuliza ni aina gani ya kozi, kiwango kipi yaani shahada ya kwanza au ya pili na alinitaka nimpe mada zisizopungua tatu ambazo ningependelea kuzifanyia utafiti.

Baada ya kumtumia mada aliniuliza ni lini ninahitaji tafiti hiyo. Aidha alinisisitiza kuwa baada ya kumaliza kazi hiyo ni lazima niikariri kwa ajili ya kuitetea kwa wahadhiri kama ada ya tafiti zote zinavyofanyika vyuoni.



 
... Ndugu blessing nakupongeza kwa uwezo wako maana si wasomi wengi-hata wenye PhD wana ari na uwezo wa ku-publish. Lakini nasikitika kwamba unawanyima wenzako nafasi ya kujifunza kwa kuwaandikia dissertation/thesis. Huu ni uhalifu wa kitaaluma, ni academic dishonest. Lengo la dissertation/thesis ya masters ni kumfundisha mwanafunzi kuwa mtafiti. Kwanin unataka kufanya kazi ya Supervisor wa mwanafunzi? Werevu tunajua lengo lako, wala hukukosea uliposema utawaandikia na wala sio kweli kwamba unafanya bure. Swali langu kwako ni hili: Je wakifika makazini, utawaandikia ripoti za kila wiki, mwezi au mwaka? You should be ashamed of yourself for this!
 
Hiyo si kazi yako. Mwanafunzi mwenyewe akiongozwa na supervisor wake ndiye anatakiwa kuandika kwa kuwa anajua alifanya nini (kwa Dissertation/Thesis au Reports) au atafanya nini (kwa proposal). Kama ulimaanisha utawasaidia ku_analyse research data au kuchapa hiyo kazi, basi upo sahihi kutangaza biashara yako.
 
Blessings kafungue ofisi pale nje ya Mzumbe(Moro na Dar), Open University, UDOM na CBE utapata vichwa mwanzo-mwisho. maana mi-wanafunzi ya mule yote vilaza haijui hata kuandika sentensi moja ya kiingereza ikaanyooka sijui wanapataje hizo Digrii au ndo digrii za Chupi?

mmmh matusi ya nini tena?.. hata UDSM, IFM na Ardhi atapata vilaza
 
Wadau nawashangaa wanabwatuka kuwa kwa nini nawasaidia watanzania wenzangu tena bure mpaka sasa nimepata response 13 zinatoka msaada hivyo ndo ujue kuna uhitaji. kama wewe huitaji kaa kimya
 
Blessings ni kweli unamaanisha bure au unatania maana mimi namjua mtu anaitwa Kamalekki 0713711540 yeye ana-edit kwa page Tsh.5,000/= so ukiwa na page 120 (5,000x120=600,000/=) na anakula vichwa mwanzo-mwisho mpaka vingine anavikimbia sometimes anazima simu wiki nzima kuepusha usumbufu wa kutafutwa na "vilaza"

Umeanza matangazo ya biashara sasa.....:spy:
 
Blessings kafungue ofisi pale nje ya Mzumbe(Moro na Dar), Open University, UDOM na CBE utapata vichwa mwanzo-mwisho. maana mi-wanafunzi ya mule yote vilaza haijui hata kuandika sentensi moja ya kiingereza ikaanyooka sijui wanapataje hizo Digrii au ndo digrii za Chupi?

joshua_ok,andrea kalima and blessings,is he/she single person or different?!
 
Pole sana, swali langu umelichukulia juu juu. Ungelitafakari na ungejijua wewe ndio kilaza mara dufu. Sasa nikufafanulie kwa mimi nikifikia stage ya kuandika abstract maana kazi ya kuandika sehemu kubwa ya ripoti imeisha au tayari nimekuwa nimeshaandika research summary ambayo nitaitumia kuandika abstract. Sasa kama unaweza kuandika abstract kwanini ushindwe kuandika ripoti. Tafakari ndugu yangu. Ingawa kama jamaa yupo tayari kusaidia watu poa tu, maana sio kila mtu ana uwezo/ au uwezo hutofautiana.

Wewe ni kilaza tu.Je na huko makazini atakuwa anawsaidia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom