Naamini Serikali Imelala usingizi

Mess

JF-Expert Member
Mar 2, 2009
661
181
Majuzi nimesikia wizara ya afya ikisema hawamtambui yule daktari wa vidonda vya tumbo pale buguruni Dr. Lubago. Kuwa dawa zake hazijathibitishwa na wizara, cha kushangaza ni kwamba yule mama ameenda bungeni zaidi ya mara mbili akipewa nafasi ya kuongelea dawa zake na amekuwa akisema zimethibitishwa. Sasa kwa miaka yote hiyo amekuwa akitibu then kama kuna madhara si amedhuru watu wengi? ndo yale yakusema hatuna taarifa ya wanyama waliosafirishwa kwenda nje, wakati wamepita airport hapo hapo.

Serikali hii sina ya kuifananisha nayo.
 
Hata madiwani wa chadema Arusha walipofukuzwa mkuchika alisema hawatambui,alakini baada ya kupambana mwishowe alisema sema anakubali kutotambuliwa kwao.hivyo usipo pambana hata hiyo dawa yako haitotambulika.pambana ndungu yako watu wapate tiba na dawa yako itatambuliwa.
 
Mambumbumbu wote wamejazana serikalin!hivyo hivyo kwa babu wa loliondo mwishowe wanataka kumshitaki!hi nchi inaendeshwa kwa mahisia zaidi kuliko utaalam!
 
Yaani kwa kweli serikalini hakuna uwajibikaji kabisaaa, wakati ameenda bungeni kwa mara ya kwanza ilikuwa kipindi cha mwakyusa na alimsikia akisema kuwa dawa hiyoi ipo inaendelea kutibu watu na imethibitishwa kwa nini asingefuatilia kujua ukweli? Sasa ukiingia ndani kwa yule mama unakuta picha alizopiga na watu kibao akiwa bungeni na waheshimiwa, ni ujinga kabisa huu.
 
Back
Top Bottom