Naamini; ccm haiwezi kukubali katiba mpya.

Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,399
255
Kuna ushahidi uliowazi kuwa ccm haiko tayari kuja na katiba mpya. Yanayojiri sasa ni danganya toto. Nasema hivyo kwa kutumia uzoefu wangu unaotokana na mambo yafuatayo:
1. CCM imejitahidi kusambaza sumu kwa wananchi kuhusu kujivua gamba ambalo nadhani si kama wanavyosema in reality, baadala ya kuzungumzia suala la KATIBA mpya.

2. Rais, m/kiti wa CCM, siku ya mei mosi alisikika akishambulia wanaharakati et. wamejichukulia suala la katiba mpya kama ajenda yao na hawataki kuona watu wengine wanachangia au kutoa maoni yao.

3. CCM inajua kuwa Wandanganyika wengi hawana elimu na ni masikini wanaolia na njaa na hawajui nini maana ya katiba mpya na hivyo kuchukulia dhana hiyo kuwa mswada au mjadala hurudishwe kwa wanchi. Hii ina maana nyingi,


  • kwanza iwe rahisi kuchakachua
  • ili wachezee na kuzunguka akili ya wasomi na wanaharakati vikiwemo vyama vya siasa kama ambavyotulishudia kwenye kuanzishwa kwa vyama vingi
  • nafasi rahisi ya kurubuni na kutoa kitu kidogo wkt wa ukusanyaji maoni
4. wamelewa madaraka na hivyo hawako tayari kwa gharama yoyote kuachia ata punje ya madaraka yao.

Wadau, najua tunasubiri mswada urekebishwe ili mjadala huanze tena ila nawahakikishia utarudi bila kuwa na tija wala marekebisho ya msingi kinyume na mahitaji ya Tanzania ya sasa.

Rais lazima ataendelea kuwa na nguvu kupita kiasi yaani kwenye vipengele vya msingi ikiwa ni pamoja na kuteua makada mbalimbali wa CCM na kuwa na nguvu kurekebisha baadhi ya vipengele

CCC hawana mapenzi na nchi ila wanatufanya MISUKULE ili tuendelee kuwa ngazi ya kupandia kwa maana waendelee kushikilia uchumi wetu. Nawasilisha.

 
Uloyaandika yaweza kuwa kweli...mfano kwenye part ya madaraka,unajua mtu akiwa kiongozi kwa muda mrefu anafind himself wierd to be a normal person...that is so open...they have been ruling us since independence,do you think it is possible for them kuachia madaraka easily like that?lkn pia umenifungua macho,mayb ni kweli wanatufunga macho but to be honest i cant judge them although i doubt that they might be fooling us in one way or another......:israel:
 
Unayosema ni kweli. Swala la katiba mpya wala haikuwa agenda yao, hata marekebisho hawakuyataka maana walishapata maoni mengi kutoka kwenye tume walizounda wenyewe lakini wakatia kapuni. Lakini kwa huu upepo uliopo kwa sasa, kuuzuia ni kujiletea maafa. They cant stop or trick us any more maana vichwani mwetu hakuna tunachokitaka tena kwa sasa zaidi ya katiba mpya. It is the only hope we have kutupatia Tz yenye nafauu!
 
Katiba mpya si ya CCM, ni ya watanzania ambao wamechoshwa na udhaifu mkubwa wa katiba iliyopo kiasi cha kusababisha kutawaliwa na mtu ambaye hakuchaguliwa na Watanzania walio wengi, ikitokea CCM wakatumia hila ili kusipatikane katiba mpya nadhani watalazimishwa na Watanzania wenyewe kupitia nguvu ya umma, hakuna kitu hatari kama kuendelea kumkandamiza mtu uliye mkandamiza kwa miaka mingi na amelijua hilo na amechoshwa na kukandamizwa. CCM lazima wakiri kwamba nchi imewashinda haiwezekani uchumi wa nchi unaporomoka kila kukicha. Kiongozi wa nchi anatumia mda mrefu katika kukisafisha chama na badala ya kujikita katika kubuni mbinu za kuuokoa uchumi.
 
Kiongozi wa nchi anatumia mda mrefu katika kukisafisha chama na badala ya kujikita katika kubuni mbinu za kuuokoa uchumi.


moja kati ya mapendekezo yangu kuhusu katiba mpya ni kumtenganisha mtendaji wa serikali na siasa. Yaani ukiteuliwa/kuchaguliwa kutumikia serikali unajiuzulu wadhifa wadhifa zote kwenye chama. Au ukichaguliwa kwenye chama bazi unaondoka serikalini. Hii itaondoja tatizo ulilolizungumza hapo juu na mengine mengi kama hayo. Nadhan tupige wote debe!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom