Naam, hivi ndivyo ilivyo - Birds of a feather fly together

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,060
22,755
Naam, ni manyang'au - huishi pamoja, huwinda pamoja na hula pamoja. Tatizo la manyang'au ni kuwa hawaaminiani kwa sababu maisha yao hutawaliwa na tabia ya ulafi. Wakikaa mkao wa kula basi kila moja ni kwa umbile lake - mwenye nguvu, mdomo mkubwa na meno makali hushiba bila taabu lakini yule mdhoofu, asiye na meno na mwenye huruma mara nyingi hulala njaa. Taabu inakuja walioshiba wanapojisahau na kuanza kuchapa usingizi mzito wakikoroma huku wenye njaa wakiulilia usingizi. Wakati mwingine wenye shibe hujisahau na kushindwa kusafisha mabaki ya vinono walivyovitafuna.

La haula, hapo kitim tim huanza na mwisho wake ni kutafunana wenyewe kwa wenyewe. Je, yawezekana tunachokishuhudia sasa hivi ni haya manyang'au ya CCM yakianza kujitafuna yenyewe kama bumbuwazi ? Je, yawezekana kuwa mwisho wa siku watakaoshinda ni wale wale wenye nguvu, midomo mikubwa na meno makali na walobaki watakwenda na maji ! Duh, Mungu atupishie mbali maanaka hapa naona si mgawanyiko bali mkakati wa ki Hitler wa kutosa wanyonge na kung'oa mizizi yote ya fitina. Jamani yeyote mwenye jeuri ya kujiita mwana CCM hivi leo, ana roho ngumu na haitakii mema hii nchi ya wadanganyika.

Jamani wote ndani ya CCM ni birds of a feather - hukusanyika pamoja, huwinda pamoja na hula pamoja - wanachotofautiana ni kiwango cha ulafi wao. Tabia ya ulafi wa wana CCM wakati mwingine huleta kizaazaa na mfarakano kama huu tunaoushuhudia lakini mwisho wa siku, tofauti na fisi, huweza kuzimwa kwa hila kwa kitu kinachoitwa muafaka. El atapeana mkono na Sitta, RA na Mwakyembe, Sophia na Kilango n.k....... Muafaka unaohusu CCM tumeushuhudia na mara nyingi ni mbinu za kufunika kombe mwanaharamu apite. CUF wana kumbukumbu ya kuuziwa mbuzi kwenye gunia - wacha nicheke !
 
Naam, hivi ndivyo ilivyo - Birds of a feather fly together Mag3
user_offline.gif
Today, 07:44 PM
- Kweli kabisa mkuu wananchi wote wa Tanzania na chama chetu tawala ambacho tumekwua tukikichagua for the last 47 years na viongozi wetu wa siasa, inasikitisha sana lakini ndio ukweli wenyewe kwamba wote tunafanana na ndege wamoja tu!

Respect.


FMEs!
 
Tuige majirani zetu Zambia waling'oa Kaunda na chama chake, Wamalawi wakamtema Banda, wakenya wakasema sasa Basi kwa KANU, It is our time, tumechezewa vyakutosha, tumefanywa matahira kwa miaka 47, Let us do it guys, Ng'oa , ng'oa , Ng'oa Ng'oa CCM na mafisadi ngo'a!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom