Naacha rasmi kununua na kulisoma Tanzania Daima hadi wazidishe uzalendo wao kwa Tanzania

Hivi kuandika kote huku ni kutaka hiyo njozi isiyoisha iendelee kubandikwa? Unanchekesha, si umwambie akutumie nakala ya hiyo njozi?

Mbona hamsemi Mohamed Said anapoleta makala yake humu JF asubuhi, mchana inaondolewa?
Nimetoa jibu tayari. Tunahitaji njia mbalimbali kuurudisha umoja wetu unaoharibiwa na CCM. Hivyo kutumiwa mimi pekee haitoshi. Mawazo ya kizalendo yanahitaji kuenea kwa watanzania wengi, wewe hautaki wananchi waurudie uzalendo wao na kukuza utaifa wetu hadi unapendekeza isomwe na wachache?
 
Wakati wetu huu ni kipindi ambacho watanzania tunahitaji mawazo ya kuujenga utaifa wetu ambao unatishiwa na wanasiasa wa CCM. Katika mazingira haya wasomaji wa Tanzania Daima tulitegemea makala zinazotoa mawazo na hoja za kuujenga umoja wetu na kuipenda nchi yetu kwa dhati zinapewa kipaumbele kikubwa. Moja ya makala hizo ni ile ya Mwanakijiji – Njozi ya Mwanakiji iliyokuwa inatoka katika gazeti la Tanzania Daima kila Jumatano. Makala hii ilikuwa imefikia sehemu nzuri, hasa maelezo kuhusu akina Abdalah ambao Mwalimu Nyerere amewahi kufanya nao kazi. Walikuwa wameshatajwa wachache, mmoja wapo Abdallah Fundikila, Abdallah Twalipo na nilikuwa nategemea kusoma akina Abdalla wengine. Kinachosikitisha ni kuwa makala ya namna hii imesitishwa kutolewa na Tanzania Daima. Ni jambo la ajabu kama wahariri wa Tanzania Daima hawakuona umuhimu wa Makala ile. Ama huwa hawasomi na kuona umuhimu wake. Sasa jina Tanzania Daima lina maana gani ikiwa makala zinazojenga mawazo ya U-Tanzania wanazitupa kapuni?. Tayari wasomaji wametoa malalamiko yao juu ya hilo lakini hakuna marekebisho. Somo moja ninawapa Tanzaia Daima ni kuwa katika dunia ya sasa vyombo vya habari ambavyo haviwasikilizi wasomaji na wasikilizaji wake vinakosa soko. Ndiyo maana vyombo kama BBC vimebadilika badala ya wasikilizaji kusikia tu nao wanatoa michango yao na inasikika. Na kwa njia hii ndiyo maana chombo kama Jamiiforums kinawapenzi wengi kwa kuwa mawazo yao yanasikilizwa. Kwa kusikitishwa na kitendo cha Tanzania Daima kuacha kuchapisha makala inayojenga utaifa wa nchi yetu bila sababu zinazoeleweka kwa wasomaji, kuanzia Jumatano ijayo sitanunua na kusoma tena Tanzania Daima hadi mwendelezo wa habari ya Njozi ya Mwanakijiji uendelee. Uamuzi huu ni tofauti na ule nilioufanya miaka mingi iliyopita wa kuacha kusoma Uhuru, na sasa Habati Leo, Majira nalo naelekea kulitosa. Sababu za kuacha kununua na kusoma magazeti ya Uhuru, Habari Leo na Majira ni kukithiri kwao kushiriki siasa chafu za kuliangamiza taifa letu katika misingi ya ubaguzi

Inaonekana wewe si msomaji wa Tanzania Daima Jumatano. Katika toleo lililopita Mwanakijiji alieleza kuwa hakuwza kuindelza ile makala ya njozi kwa sababu kadhaa na akaahidi kuwa itaendelea baada ya uchaguzi wa Igunga. Sasa ya nini kuwalaumu wahariri wa Tanzania Daima? Nafikiri kabla ya kuhukumu muulize mwanakijiji hapa hapa atakupa majibu
 
Nanda za juu kusini tunaomba nakala za Tanzania Daima ziongezwe maana linatupa raha asiponunua huyo sie tutanunua.
 
Kwa ufupi ni kuwa mwendelezo wa makala zote ndani ya TD uko mikononi mwa wahariri na waendeshaji wa chombo hicho. Miye naendelea kuandika simulizi hili ambalo linazidi kuwa kweli kila siku iendayo mbele za Mungu. Naandika kama shahidi tu wa kile nikionacho. Kwa wale ambao wamekuwa wakisubiria wasiwe na shaka sana endapo TD watashindwa kutatua matatizo waliyonayo huko au hata wakiyatatua bado natarajia kutoa njozi hii kama Kitabu - pamoja na vitabu vingine ambavyo nafanyia kazi sasa hizi. Inshallah, tutafanikiwa.

I hope watu wanasoma gazeti hilo kwa sababu nyingine zaidi vile vile na siyo kwa sababu ya makala kama ya kwangu tu.
 
Duh !!! JF sasa kuna mambo .Eti makala ya nani ambayo unataka gazeti lifungiwe ?
 
Nawafahamisha kuwa nimeanza kusoma tena gazeti la Tanzania daima kuanzia wiki ya jana baada ya kuona Njozi ya Mwanakikji imechapishwa. Leo tena Njozi ipo na gazeti nimenunua linalo. Njozi ya leo inasomo zuri sana kuhusu namna ya kupambana kwa hoja na kundi la watu linalotaka kuandika historia ya Tanganyika kwa hisia. Nawapongeza Tanzania Daima kwa kuanza kusikiliza maoni ya wasomaji na nawashauri waendelee kusoma kwa makini njozi hii ni muhimu sana kwa kuweka sawa masuala yanayohusua historia ya nchi yetu na namna na kujikinga na maandishi yenye lengo la kuwagawa Watanzania kibaguzi. Pia TD watafakari sana kuhusu maandishi wa wachangiaji kabla ya kuamua tusitisha. Ukishaamua kutoa makala au andishi fulani, wasomaji wake wanapatikana mara. Kusitisha kuna maana ya kuwavunja moyo kama ilivyotokea kwangu. Ni kweli niliacha na nisingerudia tena kusoma na kununua Tanzania Daima kama njozi ya Mwanakikijiji isingerudishwa. Asanteni Tanzania Daima kwa kuweka mambo sawa.
 
Nilisoma Njozi zake kuanzia mwanzo hadi mwisho, nikaridhika kuwa ilikuwa na mawazo mazuri sana na hoja za kupambana na wanaoharibu utaifa wetu. Nishasema awali mwanakijiji alishasema wazi kuwa yeye ameendelea kuandika njozi yake kama kawaida lakini Tanzania Daima hawazichapishi.

Tanzania daima limenunuliwa na mafisadi,njia nzuri nikuliacha kulisoma tu,hwa pamoja na clouds lao ni moja
 
Wakati wetu huu ni kipindi ambacho watanzania tunahitaji mawazo ya kuujenga utaifa wetu ambao unatishiwa na wanasiasa wa CCM. Katika mazingira haya wasomaji wa Tanzania Daima tulitegemea makala zinazotoa mawazo na hoja za kuujenga umoja wetu na kuipenda nchi yetu kwa dhati zinapewa kipaumbele kikubwa. Moja ya makala hizo ni ile ya Mwanakijiji – Njozi ya Mwanakiji iliyokuwa inatoka katika gazeti la Tanzania Daima kila Jumatano. Makala hii ilikuwa imefikia sehemu nzuri, hasa maelezo kuhusu akina Abdalah ambao Mwalimu Nyerere amewahi kufanya nao kazi. Walikuwa wameshatajwa wachache, mmoja wapo Abdallah Fundikila, Abdallah Twalipo na nilikuwa nategemea kusoma akina Abdalla wengine. Kinachosikitisha ni kuwa makala ya namna hii imesitishwa kutolewa na Tanzania Daima. Ni jambo la ajabu kama wahariri wa Tanzania Daima hawakuona umuhimu wa Makala ile. Ama huwa hawasomi na kuona umuhimu wake. Sasa jina Tanzania Daima lina maana gani ikiwa makala zinazojenga mawazo ya U-Tanzania wanazitupa kapuni?. Tayari wasomaji wametoa malalamiko yao juu ya hilo lakini hakuna marekebisho. Somo moja ninawapa Tanzaia Daima ni kuwa katika dunia ya sasa vyombo vya habari ambavyo haviwasikilizi wasomaji na wasikilizaji wake vinakosa soko. Ndiyo maana vyombo kama BBC vimebadilika badala ya wasikilizaji kusikia tu nao wanatoa michango yao na inasikika. Na kwa njia hii ndiyo maana chombo kama Jamiiforums kinawapenzi wengi kwa kuwa mawazo yao yanasikilizwa. Kwa kusikitishwa na kitendo cha Tanzania Daima kuacha kuchapisha makala inayojenga utaifa wa nchi yetu bila sababu zinazoeleweka kwa wasomaji, kuanzia Jumatano ijayo sitanunua na kusoma tena Tanzania Daima hadi mwendelezo wa habari ya Njozi ya Mwanakijiji uendelee. Uamuzi huu ni tofauti na ule nilioufanya miaka mingi iliyopita wa kuacha kusoma Uhuru, na sasa Habati Leo, Majira nalo naelekea kulitosa. Sababu za kuacha kununua na kusoma magazeti ya Uhuru, Habari Leo na Majira ni kukithiri kwao kushiriki siasa chafu za kuliangamiza taifa letu katika misingi ya ubaguzi

Labda ameshaamka toka usingizini.
 
Nawafahamisha kuwa nimeanza kusoma tena gazeti la Tanzania daima kuanzia wiki ya jana baada ya kuona Njozi ya Mwanakikji imechapishwa..
Mi naona ulikua unatuyayusha tu.
Ungeionaje hiyo Njoz
i imepostiwa kama hukulisoma?
Ina maana ulikua ukilisoma kuchunguza kama Njozi imepostiwa ndio ununue.
 
Siyo lazima waandike tu kile unachotaka wewe,ulitarajia kuona akina abdala wengi tu una maana gani, mbona tanzania daima wako vizuri tu, kama vipi rudi kusoma uhuru
 
Wakati wetu huu ni kipindi ambacho watanzania tunahitaji mawazo ya kuujenga utaifa wetu ambao unatishiwa na wanasiasa wa CCM. Katika mazingira haya wasomaji wa Tanzania Daima tulitegemea makala zinazotoa mawazo na hoja za kuujenga umoja wetu na kuipenda nchi yetu kwa dhati zinapewa kipaumbele kikubwa. Moja ya makala hizo ni ile ya Mwanakijiji – Njozi ya Mwanakiji iliyokuwa inatoka katika gazeti la Tanzania Daima kila Jumatano. Makala hii ilikuwa imefikia sehemu nzuri, hasa maelezo kuhusu akina Abdalah ambao Mwalimu Nyerere amewahi kufanya nao kazi. Walikuwa wameshatajwa wachache, mmoja wapo Abdallah Fundikila, Abdallah Twalipo na nilikuwa nategemea kusoma akina Abdalla wengine. Kinachosikitisha ni kuwa makala ya namna hii imesitishwa kutolewa na Tanzania Daima. Ni jambo la ajabu kama wahariri wa Tanzania Daima hawakuona umuhimu wa Makala ile. Ama huwa hawasomi na kuona umuhimu wake. Sasa jina Tanzania Daima lina maana gani ikiwa makala zinazojenga mawazo ya U-Tanzania wanazitupa kapuni?. Tayari wasomaji wametoa malalamiko yao juu ya hilo lakini hakuna marekebisho. Somo moja ninawapa Tanzaia Daima ni kuwa katika dunia ya sasa vyombo vya habari ambavyo haviwasikilizi wasomaji na wasikilizaji wake vinakosa soko. Ndiyo maana vyombo kama BBC vimebadilika badala ya wasikilizaji kusikia tu nao wanatoa michango yao na inasikika. Na kwa njia hii ndiyo maana chombo kama Jamiiforums kinawapenzi wengi kwa kuwa mawazo yao yanasikilizwa. Kwa kusikitishwa na kitendo cha Tanzania Daima kuacha kuchapisha makala inayojenga utaifa wa nchi yetu bila sababu zinazoeleweka kwa wasomaji, kuanzia Jumatano ijayo sitanunua na kusoma tena Tanzania Daima hadi mwendelezo wa habari ya Njozi ya Mwanakijiji uendelee. Uamuzi huu ni tofauti na ule nilioufanya miaka mingi iliyopita wa kuacha kusoma Uhuru, na sasa Habati Leo, Majira nalo naelekea kulitosa. Sababu za kuacha kununua na kusoma magazeti ya Uhuru, Habari Leo na Majira ni kukithiri kwao kushiriki siasa chafu za kuliangamiza taifa letu katika misingi ya ubaguzi

Wewe hujui tu kwa nini makala hio imesitishwa. Inaelekea kuelezea ukweli juu ya wapiganiaji halisi wa uhuru wa nchi hii, tena watu wenyewe ni wa dini fulani! teh teh! Mzee wa lower ameiban makala hiyo, wala sio mhariri wa gazeti.
 
Hivi kuandika kote huku ni kutaka hiyo njozi isiyoisha iendelee kubandikwa? Unanchekesha, si umwambie akutumie nakala ya hiyo njozi?

Mbona hamsemi Mohamed Said anapoleta makala yake humu JF asubuhi, mchana inaondolewa?
bila neno " unachekesha '' hauwezi kusomeka ??
 
Back
Top Bottom