Na mama mkwe naye anataka!

SOMA neno la Mungu katika bilia utapata msaada wa kweli.
Soma kitabu cha Warumi.

Naweka kitabu hicho hapa ili uweze kukisoma.

....khaa, babuu si ungeweka mistari miwili mitatu tu... yaani nime scroll mpaka...! ... na wanazuoni wakija hapa kumwaga aya zao, au ma buddha na ma sikh wakija na vitabu vyao patatosha kweli?

Ngoja nikatambike madogoli mie, tawire tawire...
 
Babu anataka kulazimisha watu kusoma kitabu kizima! Hana huruma na wengine wanaolipia internet by kilobyte huko.
 
....khaa, babuu si ungeweka mistari miwili mitatu tu... yaani nime scroll mpaka...! ... na wanazuoni wakija hapa kumwaga aya zao, au ma buddha na ma sikh wakija na vitabu vyao patatosha kweli?

Ngoja nikatambike madogoli mie, tawire tawire...

nakwambia...duh! sijui ni wangapi watakuwa na subra ya kusoma yote hiyo...nimescrolllllllllllllllllllllllllllllllllllllllllll nikachoka, mpaka nika hit page down!!
aliyesoma atupatie summary hapa!
 
Exhaud naona "umetupestia" bible nzima watu wanaweza kusoma na kuelewa vifungu vyote hivyo kweli..!!?? ungetoa summary tu ya ulichokusudia kusema, otherwise mimi naona hii ni sawa na zile story za SHY za kutunga tu.
 
Jamaa aachane na mamamkwe! Si vizuri kutembea na mzazi wa mwenzake hata kama anampenda namna gani na ana uzuri wa malaika wa paradisini. Si utu wala maadili mema. Huyo mama kagengeuka.

Amwache hata akimwambia mtoto wake (mkeo). Ni bora igundulike kwamba katembea na shemejiye. Ina nafuuu. Si aibu ya kutisha. Ataweza kuyamaliza na mkewe kwa mazungumzo na kumwomba msamaha. Lakini akitembea na mamamkwe na kesho mkewe akaja kujua. Itakuwa mbaya sana. Ngumu kusameheka. Itamwumiza sana mkewe. Kumbe ni aheri achague "the lesser evil". Kazi kwake!
 
Kuliko kufanya kitu chochote na mama mkwe wake bora atubu kwa mke wake. Huyo mama mkwe nae inaelekea ana kiu..Sam asikubali, laana hiyo!.
 
MAMA mkwe kapenda, kaiomba eti umnyime na kama bado anadai dai kwa sura ya utu uzima, kula kwa sana mpaka achanganyikiwe, maana mpira unachezeka katika kila kiwanja bila shida. tena mpe magoli ya ukakika mpaka awe HOIIIIIIIIIIIIIIIIIII.
 
Jamaa aachane na mamamkwe! Si vizuri kutembea na mzazi wa mwenzake hata kama anampenda namna gani na ana uzuri wa malaika wa paradisini. Si utu wala maadili mema. Huyo mama kagengeuka.

Amwache hata akimwambia mtoto wake (mkeo). Ni bora igundulike kwamba katembea na shemejiye. Ina nafuuu. Si aibu ya kutisha. Ataweza kuyamaliza na mkewe kwa mazungumzo na kumwomba msamaha. Lakini akitembea na mamamkwe na kesho mkewe akaja kujua. Itakuwa mbaya sana. Ngumu kusameheka. Itamwumiza sana mkewe. Kumbe ni aheri achague "the lesser evil". Kazi kwake!

Babuyao umesema nini? Kutembea na shemeji si aibu ya kutisha?

Tuangalie katika kulaani mahusiano ya bwana na mama mkwe tusije kuya trivialize yale ya bwana na shemeji, hii ni familia moja bado, I mean huyu shemeji si hata sheji wa kirafiki -not to trivialize that either- infidelity is infidelity, and although kutembea na mama mkwe ni aibu kubwa sana, hakupunguzi uchafu wa kutembea na shemeji.
 
SOMA neno la Mungu katika bilia utapata msaada wa kweli.
Soma kitabu cha Warumi.

Naweka kitabu hicho hapa ili uweze kukisoma.
Kwa kweli si rahisi kusoma kitabu hiki kwenye kompyuta. Ilitakiwa utoe mistari michache inayoendana na mada hii. Hebu tuachane na hilo.

Kuhusu mada hii huyo jamaa asikubali kabisa kumpa mkwe anachotaka. Kama bado ni vigumu basi awaone wazee wa kanisa kama ni mkristu au kwa mashehe kama ni muislamu kisha awape kisa hicho pengine itasaidia.
 
sio zile story za IT specialist SHY?

Nadhani Yo Yo anamaanisha kuwa hii ni Riwaya...... siyo kisa cha kweli.
Hata mimi hainiingii akilini kuwa hiki ni kisa cha kweli......
Kama ni cha kweli basi hiyo ni disfunctional family..inahitaji maombi kufukuza mapepo yanayoisumbua.MUNGU apishe mbali.
 
Inategemea huyo mama mkwe yukoje jee anatizamika?pili vipi yupo kwenye Ndowa?

Ndugu yangu...
Utahalilisha haramu kwa namna hii? HAPANA! HARAMU NI HARAMU TU.
Hebu mfikirie yule mama yako aliyekuzaa halafu pata picha kuwa huyu naye ni mama..... bado utatafuta kuhalalisha?
 
Msaidieni Jamaa yangu huyu, aliponiomba ushauri nilimwambia anipe mwezi mmoja nifikirie:
Jamaa yangu anaitwa Sam(si jina la kweli) ni kijana mwenye mafanikio kimaisha,anafanya kazi katika kampuni moja ya mafuta hapa Tanzania. Ameoa na ana watoto wawili wemye miaka 5&2. Mwaka jana alikuja kutembelewa na shemeji yake ambaye ni mdogo wa kuzaliwa na mkewe. Binti huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuja kupumzika huku akitafuta nafasi ya chuo kikuu dar baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha sita huko nyumbani kwao Tanga. Wakati fulani nyumbani kwao mkewe walipata matatizo yaliyo lazimisha mkewe kurudi nyimbani kwa wiki mbili, kipindi hiki jamaa yangu anasema shetani au ibilisi alitembelea nyumba yake na yeye na shemeji yake wakaanza mahusiano yasiyofaa. Baada ya wiki mbili mkewe alirudi na mama yake wakati huo jamaa yangu na shemejiye uhondo umewanogea. Siku moja usiku jamaa alichomoka chumbani na kukutana na shemeji yake sebuleni wakiwa katika hali mahaba mama mkwe akawaona kwa bahati mbaya hakupiga kelele wala kuwasemesha.Asubuhi yeye na mwanawe mdogo yaani yule shemeji wakaaga huku mkewe akishangaa kwa ughafla wa safari. Mamamkwe hakuthubutu kusema kwa mtoto wake kisa kilicho waondoa. Hata baada ya miezi mitatu yule binti alirudi kusoma chuo UDSM jamaa yangu alimfuata kumuuliza kilichotokea lakini yule binti kagoma hata kumuangalia na hajawahi hata kuisikia sauti yake, kifupi jamaa kabakia gizani. Hivi karibuni mama mkwe alikuja kuwa tembelea na wakati huohuo mama yake mzazi na jamaa yangu akapata maradhi kalazwa nyumbani kwao hukohuko Tanga.Kwa maana hiyo nyumbani amebakia jamaa yangu na watoto pamoja na mama mkwe. Sasa kasheshe mama mkwe anamkomalia jamaa ampe naye vitu na akikataa anamueleza mkewe kilichotokea usiku ule. Jamaa amekwisha tubu mara kadhaa na hataki kabisa kuchezea ndoa yake kwani anampenda mkewe sana. Ila mama mkwe yupo determined kabisa na mara kadhaa amekwisha mfuata bafuni uchi...Ushauri please!!!!

Uko serious kabisa unaomba ushauri au unatania? There must be something wrong with you!
 
... Ni bora igundulike kwamba katembea na shemejiye. Ina nafuuu. Si aibu ya kutisha.
Ataweza kuyamaliza na mkewe kwa mazungumzo na kumwomba msamaha.

Unajuaje ataweza "kuyamaliza na mkewe kwa mazungumzo"? Wanaume wako spoiled rotten. Una chiti halafu unadhani ni issue rahisi tu, utamwimbia imbia ngojera mwenzako, utampapasa papasa na kumfuta machozi yataisha, mazoea putrid! Hao wanawake ni wa kizamani na wanakwisha, walikuwa hawajaelimika.

Mapenzi na mama mkwe ni vibaya lakini sio kwa sababu yale ya shemeji yana ahueni. Yote ni maasi. Tena mke anaweza kuona mmewe kafanya vibaya zaidi kwa kuhadaa mtoto wa shule (shemeji ) kuliko mama, li mama zima na akili zake limem blackmail mtoto, mka mwana, amlale. Huwezi kubashiri ni lipi litasamehewa kirahisi.

Ni male chauvinism inafanya udhani ni rahisi sana kusamehewa infidelity. Wanawake ndio wamewadekeza.
 
Uko serious kabisa unaomba ushauri au unatania? There must be something wrong with you!

Let's give Sam the benefit of a doubt! Ukisoma sentensi zake mbili za mwisho utaona kwa hakika anahitaji ushauri wa jinsi ya kujitoa kwenye hiyo situation.

Kuna watu wanajaribu kubeza kwamba ni kisa cha kutunga (may be in this case its true) lakini haya mambo (ya in-laws) yanatokea sana hata kama siyo kwa kiasi hiki cha mama mkwe kukufuata bafuni akiwa uchi.

Ushauri wangu ni kwa bwana Sam kutafuta wakati na mahala mafaka kuongea na mkewe kuhusu kadhia hii nzima ili kupata msimamo wa pamoja. Lakini kwanza ni lazima amuombe radhi mkewe kwa yeye kusababisha hii tafrani (kutembea na shemeji yake). Wakishakubaliana na mkewe, huyo mama mkwe hata kuwa tena na 'object' ya kuitumia kum blackmail na hivyo ndoa hiyo itabaki salama na haitakuwa chukizo kwa Mungu.
 
Last edited:
kweli huu mjadala ni mkali sana.......lakini kama angekuwa ni mkweli na amejutia dhambi zake basi angekuwa tayari kashamweleza mkewe na wameshasameheana muda mrefu....ila nahisi kama vile huyu mtu ameshatoa dozi kwa mkwewe ila hapa hii mada hapa inalenga sana kumpa sapoti ili asijione mdhambi....but ukweli ni kwamba amekosa sana tena sana kwani hata maandiko matakatifu yasema hivyo na yakataza hivyo.
 
Ushauri: Mweleze mkeo ukweli kwa yaliyowapata wewe na shemejio na kisha umuombe radhi, huyo mama mkwe wako mwambie tu"UTAJIJU!"
 
Ushauri wangu ni kwa bwana Sam kutafuta wakati na mahala mafaka kuongea na mkewe kuhusu kadhia hii nzima ili kupata msimamo wa pamoja. Lakini kwanza ni lazima amuombe radhi mkewe kwa yeye kusababisha hii tafrani (kutembea na shemeji yake). Wakishakubaliana na mkewe, huyo mama mkwe hata kuwa tena na 'object' ya kuitumia kum blackmail na hivyo ndoa hiyo itabaki salama na haitakuwa chukizo kwa Mungu.

Nilipo mueleza kuhusu kumuambia mkewe yeye mwenyewe aliniambia amejaribu kupima madhara yanayoweza kutokea katika ndoa yake na familia ya mkewe ameona ni bora akatafuta njia kulimaliza hili la mama mkwe bila kufufua la shemeji. Hebu fikiria ana mtoto wa miaka 2, iwapo atamwambia mkewe akichukua uamuzi utakao weza kuathiri ndoa yao huyo mtoto mdogo itakuwaje? Na kwa upande wa familia ya mkewe ndio mambo magumu kabisa kifupi mkewe amezaliwa na huyo mdogo wake tu, kwa maana nyingine familia ya mkewe ina watu sita tu yeye, mumewe, watoto, mama yake na mdogo wake, iwapo hili litajulikana atagombana na familia yake hivyo kubakia yeye peke yake.Hapo ndipo ugumu wa kumueleza mkewe ulipo.
 
Mh kweli dunia imefika ukingoni.......... badala ya mama kuwa mwongozo wa ndoa njema ndo mharibifu!! Shemeji mwambie tu dada kuwa mama simwelewi kabisa ananifanyia manyang'unyang'u nisiyoyaelewa (amweleze kabisa kuwa anamtokea uchi sasa sijui ana maana gani) Jihami shem, maana akianza mama kusema hutaaminika. Hii itakusaidia kwani ukishasema unamtolea uvivu mama tena wamwambia ntakusemea kwa mwanao afu aende akashtaki we utakuwa tayari ushasafisha njia-

Kama wifi ataambiwa na mama mkwe kuwa ulitoka na binti kuwa mkali tena mshutumu kwa kukukosea heshima tena mchimbe mkwara kuwa akiendekeza mambo ya uwongo utamfungasha arudi kwao. USIKIRI kuwa umetembea na mdogo mtu lol kosa la jinai hilo ndugu yangu huwa halitoki ndani ya mioyo yetu, ni ndugu huyo na si shoga (ya shoga haiumi kama ya ndugu)

Lakini nawe shem umeshindwa kumpunga shetani wako (mbona revola zimejaa madukani jamani?) Ona sasa umejitia matatani......... pole
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom