Nduka
JF-Expert Member
- Dec 3, 2008
- 8,552
- 2,360
Msaidieni Jamaa yangu huyu, aliponiomba ushauri nilimwambia anipe mwezi mmoja nifikirie:
Jamaa yangu anaitwa Sam(si jina la kweli) ni kijana mwenye mafanikio kimaisha,anafanya kazi katika kampuni moja ya mafuta hapa Tanzania. Ameoa na ana watoto wawili wemye miaka 5&2. Mwaka jana alikuja kutembelewa na shemeji yake ambaye ni mdogo wa kuzaliwa na mkewe. Binti huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuja kupumzika huku akitafuta nafasi ya chuo kikuu dar baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha sita huko nyumbani kwao Tanga. Wakati fulani nyumbani kwao mkewe walipata matatizo yaliyo lazimisha mkewe kurudi nyimbani kwa wiki mbili, kipindi hiki jamaa yangu anasema shetani au ibilisi alitembelea nyumba yake na yeye na shemeji yake wakaanza mahusiano yasiyofaa. Baada ya wiki mbili mkewe alirudi na mama yake wakati huo jamaa yangu na shemejiye uhondo umewanogea. Siku moja usiku jamaa alichomoka chumbani na kukutana na shemeji yake sebuleni wakiwa katika hali mahaba mama mkwe akawaona kwa bahati mbaya hakupiga kelele wala kuwasemesha.Asubuhi yeye na mwanawe mdogo yaani yule shemeji wakaaga huku mkewe akishangaa kwa ughafla wa safari. Mamamkwe hakuthubutu kusema kwa mtoto wake kisa kilicho waondoa. Hata baada ya miezi mitatu yule binti alirudi kusoma chuo UDSM jamaa yangu alimfuata kumuuliza kilichotokea lakini yule binti kagoma hata kumuangalia na hajawahi hata kuisikia sauti yake, kifupi jamaa kabakia gizani. Hivi karibuni mama mkwe alikuja kuwa tembelea na wakati huohuo mama yake mzazi na jamaa yangu akapata maradhi kalazwa nyumbani kwao hukohuko Tanga.Kwa maana hiyo nyumbani amebakia jamaa yangu na watoto pamoja na mama mkwe. Sasa kasheshe mama mkwe anamkomalia jamaa ampe naye vitu na akikataa anamueleza mkewe kilichotokea usiku ule. Jamaa amekwisha tubu mara kadhaa na hataki kabisa kuchezea ndoa yake kwani anampenda mkewe sana. Ila mama mkwe yupo determined kabisa na mara kadhaa amekwisha mfuata bafuni uchi...Ushauri please!!!!