Na CEO wenu ni kama huyu wetu?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Jamani hapa ofisini kwetu, yaani kwenye institution yetu CEO amejaza watu wa kabila lake, jamaa zake, watoto wa marafiki zake, wapenzi wake, na wanawe bila kuangalia sana uwezo wao, na ni 'ngono-centric CEO i.e. womanizer' wa nguvu . Shuleni nilifundishwa kuwa mashirika ya umma yalikufa kutokana na 'undunguization' i.e. favouratism and nepotism'.

Je, dawa ya kusitisha tabia hii ya ma-CEO wengi wa Bongo ni ipi? Je, hii sio namna ya 'corruption'?
 
Peleka taarifa TAKUKURU atashughulikiwa fasta......................LOL
 
Hebu taja hiyo ofisi yenu na pia mtaje kwanza huyo CEO hapa ndio JF atapatiwa dawa tu.Usilete mambo ya vitendawili.
Inawezekana kukawa na mtu anaye-sit kwenye Board of Directors ya hiyo ofisi yenu itakuwa rahisi kumpa kubwa kwenye vile vikao vya kiutu uzima..
 
jamani hiyo kampuni iko wapi? Na Mimi nimuonge Huyo CEO kamshahara kangu ka ualimu anipe ajira hata ya umessenger. Nimechoka na chalk na kuzalilishwa
 
Acha kunifuatilia fuatilia, mimi sina upendeleo wewe umeajiriwa hapa je wewe ni ndugu yangu?
 
Jamani hapa ofisini kwetu, yaani kwenye institution yetu CEO amejaza watu wa kabila lake, jamaa zake, watoto wa marafiki zake, wapenzi wake, na wanawe bila kuangalia sana uwezo wao, na ni 'ngono-centric CEO i.e. womanizer' wa nguvu . Shuleni nilifundishwa kuwa mashirika ya umma yalikufa kutokana na 'undunguization' i.e. favouratism and nepotism'.

Je, dawa ya kusitisha tabia hii ya ma-CEO wengi wa Bongo ni ipi? Je, hii sio namna ya 'corruption'?

kabla ya kummulika ceo tuanze na wewe, je wewe umepataje ajira kama sio ndugu yake au umengonoka naye!
 
hahahah hapa kwetu ni wahaya hata ambao shule hamna eti ndo wahasibu tunawachakachua kwakweli wao wanajiona wajanjaaaa
 
Back
Top Bottom