N.E.C Imuondoe Kikwete Kukinusuru CCM

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Aliingia madarakani kwa kauli mbiu ya “Ari Mpya Nguvu Mpya. Kasi Mpya” wengine walimuona kweli “Chaguo la Mungu” Kaulimbiu iliyogeuka kuwa janga la taifa na chama chetu tukufu CCM. Katika kipindi chake cha uongozi, Rais Kikwete amegeuka kuwa mzigo na aibu kwa taifa; amekumbatia udini, amejenga makundi ndani ya chama chetu.

Ametumia cheo chake kukifedhehesha taifa. Amekuwa rais wa kwanza kuongwa suti nchini Tanzania. Rais wetu hajui kwa nini watanzania maskini, na wala hajui Ikulu anafanya nini. Hii ni kwa sababu meli za Iran zinasajiliwa akiwa safarini marekani bila yeye kujua

Ameifanya CCM kuchukiwa kila kona ya nchi. Amekuwa rais wa kwanza kupigwa mawe na wananchi. Hivi kweli tunaelekea wapi? Mh. RAIS. Utakosa nini ukiyaacha madaraka kukinusuru chama na Taifa!

Rais Kikwete amekumbatia ufisadi na mafisadi. Hapa namaanisha EPA, Richmond, mabillioni uswisi nk. Katika uongozi wake, uonevu wa polisi umepitiliza. Raia wanatekwa na kuuwawa kinyama. Mahakama zetu zimekuwa za kulinda maslahi ya viongozi. Urasimu, rushwa, kugawana vyeo vimezidi.rasilmali za nchi zinayeyuka, umasikini umekithiri huku huduma za jamii zote zinatoweka. Aibu kwa CCM.

Ili kukinusuru chama chetu mama (CCM) N.E.C lazima ifanye mpango wa kumuondoa Kikwete haraka iwezekanavyo. Hatuwezi tena kujidanganya kwamba chama chetu kinapendwa. Vinginevyo tusubiri kihama 2015 huku mkiyaweka kwenye kumbukumbu huu waraka wangu

MTOTO WA CCM
 
haya mkamwambie atekeleze kwa vitendo dhana ya kujivua gamba yaani mkamwambie yeye ndiyo gamba!Mbona wenzenu ANC walimtoa sped Mbeki?
 
Hapo naona bla bla bla tu,huna point mzee, naona umetuma huu ujumbe ukiwa unajisaidia choo cha bar.
 
nadhani umeupokea ujumbe ndo maana umejibu. Mfikishie Rais ujumbe. Kama wewe ndiye rais, hapo sana nitaelewa majibu yako
 
NO NO NO NAOMBEA KIKWETE,NAPE,MUKAMA WABAKI KWANI HUU NI MTAJI MZURI KWA CHADEMA MAANA ANGEKUWEMO LOWASSA NI KICHWA ANGEPOKEA USHAURI WA CHADEMA LAKINI HAWA WALIOBAKI HUMO HAMNAZO :israel:
 
Aliingia madarakani kwa kauli mbiu ya "Ari Mpya Nguvu Mpya. Kasi Mpya" wengine walimuona kweli "Chaguo la Mungu" Kaulimbiu iliyogeuka kuwa janga la taifa na chama chetu tukufu CCM. Katika kipindi chake cha uongozi, Rais Kikwete amegeuka kuwa mzigo na aibu kwa taifa; amekumbatia udini, amejenga makundi ndani ya chama chetu.

Ametumia cheo chake kukifedhehesha taifa. Amekuwa rais wa kwanza kuongwa suti nchini Tanzania. Rais wetu hajui kwa nini watanzania maskini, na wala hajui Ikulu anafanya nini. Hii ni kwa sababu meli za Iran zinasajiliwa akiwa safarini marekani bila yeye kujua

Ameifanya CCM kuchukiwa kila kona ya nchi. Amekuwa rais wa kwanza kupigwa mawe na wananchi. Hivi kweli tunaelekea wapi? Mh. RAIS. Utakosa nini ukiyaacha madaraka kukinusuru chama na Taifa!

Rais Kikwete amekumbatia ufisadi na mafisadi. Hapa namaanisha EPA, Richmond, mabillioni uswisi nk. Katika uongozi wake, uonevu wa polisi umepitiliza. Raia wanatekwa na kuuwawa kinyama. Mahakama zetu zimekuwa za kulinda maslahi ya viongozi. Urasimu, rushwa, kugawana vyeo vimezidi.rasilmali za nchi zinayeyuka, umasikini umekithiri huku huduma za jamii zote zinatoweka. Aibu kwa CCM.

Ili kukinusuru chama chetu mama (CCM) N.E.C lazima ifanye mpango wa kumuondoa Kikwete haraka iwezekanavyo. Hatuwezi tena kujidanganya kwamba chama chetu kinapendwa. Vinginevyo tusubiri kihama 2015 huku mkiyaweka kwenye kumbukumbu huu waraka wangu

MTOTO WA CCM
Du!
Hili ni scud!
Mao aliwahi kusema," bombard the headquarters"
 
306541_3996124057983_1535558347_n.jpg
morogoro mjini2015
 
NO NO NO NAOMBEA KIKWETE,NAPE,MUKAMA WABAKI KWANI HUU NI MTAJI MZURI KWA CHADEMA MAANA ANGEKUWEMO LOWASSA NI KICHWA ANGEPOKEA USHAURI WA CHADEMA LAKINI HAWA WALIOBAKI HUMO HAMNAZO :israel:

Mwambie ajitahidi huko Canada, US na UK aliko akirudi atakuta kazi imekamilika. Anajitahidi sana awe rais japo kwa wiki moja, ndio maana anaona 2015 mbali.
 
NO NO NO NAOMBEA KIKWETE,NAPE,MUKAMA WABAKI KWANI HUU NI MTAJI MZURI KWA CHADEMA MAANA ANGEKUWEMO LOWASSA NI KICHWA ANGEPOKEA USHAURI WA CHADEMA LAKINI HAWA WALIOBAKI HUMO HAMNAZO :israel:

nepi yuko busy either anapaka karolight, au anamponda mzee lowasa
 
Ili kukinusuru chama chetu mama (CCM) N.E.C lazima ifanye mpango wa kumuondoa Kikwete haraka iwezekanavyo. Hatuwezi tena kujidanganya kwamba chama chetu kinapendwa. Vinginevyo tusubiri kihama 2015 huku mkiyaweka kwenye kumbukumbu huu waraka wangu

Umesema kweli Mkuu. Lakini unasahau jambo moja. Tanzania si kama South Afrika kwamba chama kinaweza kikam-recall raisi kama walivyomfanyia Thabo Mbeki. Uchaguzi wa Tanzania wananchi wanampigia kura raisi sio chama. Hivyo kwa sasa JK amechaguliwa na wananchi sio CCM. Kwa mtaji huo NEC ya CCM haiwezi kumwondoa JK madarakani, raisi aliyechaguliwa na wananchi, wanachama wa CCM na wasio wanachama wa CCM. (Labda kama unataka kwenye katiba mpya watu wachague chama badala ya raisi, ili chama kiwe na uwezo wa kumbadilisha raisi kabla ya uchaguzi mkuu).

JK anaweza kutoka madarakani kwa kuondolewa na kura ya kukosa imani nae ya Bunge. Hapo uchaguzi mkuu mpya utaitishwa. CCM hawawezi hata siku moja kukubali hili.

Ikiwa JK atajiuzuru kwa utashi wake au suala la afya, au kukumbwa na mkasa wa kifo, basi Makamu wa Raisi, Dr. Bilali, ndiye anachukua madaraka ya uraisi. Sasa hapo chekecha mwenyewe, maana isije ikawa kuruka maji kukanyaga tope.
 
Back
Top Bottom