Mzungu Omba Omba ndani ya Dar

Wazungu nao njaa tuu!..inaonesha mtoa mada unawaona wazungu kama hawana shida sana eeeh!..mbona hujaandika juu ya wale vikongwe wa Dodoma wanaonyoosha mikono kuomba hata kama basi lipo katika 180 speed?au sio tukio hilo?
 
Wazungu nao njaa tuu!..inaonesha mtoa mada unawaona wazungu kama hawana shida sana eeeh!..mbona hujaandika juu ya wale vikongwe wa Dodoma wanaonyoosha mikono kuomba hata kama basi lipo katika 180 speed?au sio tukio hilo?

Wapo kilimatinde singida road pale. Wale wana ukoma.
 
nilikuwa najaribu kusoma huu uzi niweze kuona hoja zetu juu ya jambo hili, nimesikitika kuona kwamba swala la utoaji bado ni janga la kitaifa, kwa uzoefu wangu najua kwamba watanzania wengi kwenye maeneo yetu ya kazi tuasifiwa kwa kuwaomba omba wazungu misaada... na imefika mahali kwamba wazungu wengi wametoa misaada mpaka wamechoka, sasa inakuwaje shida kwa mzungu huyu kukuomba wewe msaada? hayo ni majaribu tu mungu amekuletea ili akuone wewe ni mtu wa namna gani.. hukupaswa kuangalia rangi yake kwakuwa ni mweupe na kumuhukumu? na je ulujuaje kama haikuwa kweli kwamba account yake imekuwa blocked?na je kwanini aliamua kukuomba wewe na si mtu mwingine? think twice....
 
Duuh huyu jamaa kweli ni omba omba maana mimi nilishakutana naye kama miezi mitatu iliyopita pale Kisutu ilipokuwa stand ya mabasi... Nilikuwa kwenye gari namsubiri jamaa yangu mmoja akaja akanigongea dirisha... Nikamfungulia, akanisalimia na kuniuliza kama nazungumza kizungu, nikamjibu ndio... Akanipa story kama ya jamaa alivyosema kuwa cards zake sijui za Bank of America zimekuwa blocked ilibidi awasiliane na bank huko USA...
Kwa kuwa alijitambulisha anatoka USA na mimi ndio nimerudi toka huko sio muda mrefu sana nikamuonea huruma... Bahati mbaya siku hiyo ilikuwa ni holiday huko USA kwa hiyo na Embassy yao hapa imefungwa... Aliniomba buku 10 au 15 for some few days mpaka dada yake ametumie hela... Nikampa buku 5 ingawa nilikuwa na mashaka sana... Kumbe jamaa ni zuuuuga.... Nitakutana naye tuuu siku nyingine nitamtoa nishai...

mkuu kama kweli ulikuwa marekani hukuona ombaomba? mbona wako wengi tu? shuda haichagui rangi ya mtu... ulifanya vizuri kumsaidi usijilaumu na wala huna haja ya kumtoa nishai? wewe hujawahi kuishiwa?
 
haha mi nakumbuka 2010 nipo mi taa ya far east Beijing ...kipindi cha Olympic kile, mtasha alinipiga mzinga alinipa story hizohizo .. ila yeye alidai kaibiwa .. sikumuamini but niliamua tu kumsaidia

good kutoa ni moyo....
 
labda ni mmoja wa wale wanaotembea kuzunguka dunia na wanategemeaga kupata vibarua ili kuji sapoti sasa inawezekana hapa nchini kwetu mnajua tena vibarua ni mmmmhhh. so kwa mie siogopi na sioni nini umuhimu wa kusema vibaya wazungu etc sababu umeobwa pesa.

ningekuwa mie ningemsaiia na sio kuwa na hasira eti mzungu wakina dada tusi.... haina maana hasira weka pembeni kwani huyo kakuambia ni masikini unaweza kuta anajaribu maisha around the world kama kawaida zao na ni tajiri kuliko wewe

oyaaaaa acheni zarau ya wazungu sijui wanini sababu ndugu zetu wa kike wanatoka nao.

naunga mkno hoja..
 
mwingine alikuwepo pale makongo juu ila siku hizi simuoni alikuwa na mizinga huyo balaa
 
Wazungu watu kama sisi wanaomba na wapo maskini wakula la chini ya madaraja, wapo wanaogongwa kwa njaa zao hasa wakijua we mgeni wanajua una cash .
 
ha ha ha wadau leo nimekutana na mzungu akanipiga mzinga ili aweze kusukuma siku hadi j5 ambapo dada yake atamtumia hela kutoka marekani kwa madai eti account yake imeblockiwa,nikamtell live kwamba sina kitu kwa kumsaidia tu nikamwambia nenda ubalozi wa marekani pale watakusaidia tu kwa kuwa ni raia wao,wadada kuweni makini sio kila mzungu ana hela ili mkaringishie nao u-turn wengne ni magumashi tu,matapeli ha ha ha ha ha ha

usidanganyike hilo ni tego la mashushu wanausalama wa obama, bado wana nusa nusa huku na kule
kama kuna watu waliokuwa wana mvizia rais wao
 
That was a ----ing CIA,ndo tabia zao,ungemchapa makofi! he was trying to fool you!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom