mzungu na Muafrica

Washawasha

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
16,652
13,077
Waafrica 2mekuwa wa2 wa kujirudisha nyuma cc wenyewe.je? Unakubaliana na usemi huu....Mzungu akienda porini anaenda fanya research,Muafrika anaenda kujisaidia haja kubwa
 
Waafrica 2mekuwa wa2 wa kujirudisha nyuma cc wenyewe.je? Unakubaliana na usemi huu....Mzungu akienda porini anaenda fanya research,Muafrika anaenda kujisaidia haja kubwa
Hayo ni mawazo hasi ambayo chanzo chake ni lack of confidence, kama wewe mwenyewe hujiamini kwamba u binadamu kamili sawa na binadamu mwingine yeyote yule kokote kule lazima udharaulike kwa sababu wewe mwenyewe unajidharau.
sote tuko sawa tunatofautiana rangi! nashangaa watu wanaibeza rangi yao nyeusi wanajichubua wakati hao weupe kipindi cha joto wanajianika juani kufifisha weupe!
 
Kweli kabisa watu wengi wanaitetemekea rangi nyeupe, utafikiri wana tofauti sana na sisi!
 
Kuna wazungu kibao wanaokuja kufanya kazi na makampuni mbali mbali nchini who do not have the qualities and knowledge ya kazi wanazofanya, utakuta waofanyana hizo kazi ni subordinates wao lakini wao ndo hupata credits. very disapointing.
 
Tunasema msemo huu kutokana na mazingira tu ya wao kuwa wakija huku basi wanapenda kutembelea sehemu mbalimbali ambazo huko kwao wanakuwa hawana,kwa mfano misitu huku kwetu ni mingi na kwa mwenyeji ni jambo la kawaida kumkuta akienda hata kujisaidia humo na haoni kama kuna jambo la ajabu ila kwa mgeni yeyote ambaye hajawahi ishi katika mazingira yale ni dhahiri atashangaa na kuonekana anafanya research.
Hivyo sikubaliani na usemi huo.
 
Jamani, mbali na ukweli kuwa nyumba zetu nyingi za vijijini hazina vyoo ama havitoshi kwa idadi ya watu wanaoishi katika nyumba hiyo, sioni vibaya mtu kujisaidia porini. Zaidi ya hayo, haja, hasa haja kubwa, haina mzungu wala nani. Niliwahi kuona filamu ambapo Rambo alilishwa haluli, akasahau ubabe wake na kuingia porini kwenda ku-"download" vitu.

Lakini pia tukubali kuwa sisi wenyewe tunajidharau. Ukiwa uzunguni, mzungu hatokufikiria kuwa unaenda kujisaidia akikuona unaingia msituni, sasa kwa nini mwafrika mwenzako umfikirie hivyoM
 
Back
Top Bottom