Mzungu apigwa visu UDSM

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
Wana JF,
Nimeona ni muhimu kupost thread hii ya kusikitisha kuhusu mwanafunzi wa kigeni aliyevamiwa na kuchomwa visu UDSM juzi.

Kitendo hiki kimetokea katika taasisi nyeti ya elimu, mahali ambapo wanafunzi wengi wa kigeni hufika kila mwaka kwa vipindi tofauti kupitia exchange programme baina ya vyuo mbalimbali duniani kikiwemo UDSM.

Zaidi sana tukio hili limetokea mahali ambapo kuna kitengo maalumu cha ulinzi na usalama katika kampasi (auxilliary police) ambao wanawajibika kuwalinda wanafunzi na wafanyakazi.

Je, wahalifu hao wanapitapita je na kuwafikia wanachuo tena katika vyumba vyao?


Mzungu apigwa visu Jijini

2008-10-22 18:23:23
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Mzungu mmoja wa kike ambaye ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amejikuta akijeruhiwa mwilini baada ya kupigwa visu viwili na mtu aliyemvamia chumbani kwake kwa nia ya kumpora kompyuta yake ndogo `laptop`, pesa na vitu vyake vingine kadhaa vya thamani.

Tukio hilo la kusikitisha, linadaiwa kutokea mishale ya saa 6:00 mchana juzi, pale kwenye jengo la hosteli mojawapo ya kampasi ya Mlimani, lijulikanalo kama `Hall Three` almaarufu kama Extension Block, chumba namba 792.

Imedaiwa kuwa mdada huyo ni wa Kimarekani na anatoka LCCT Group na yuko chuoni hapo kupitia mpango wa ubadilishanaji wanafunzi (exchange programme).

Mashuhuda wamedai kuwa mtasha huyo amekutwa na masahibu hayo juzi wakati akiwa chumbani mwake.

Wanadai baadhi ya mashuhuda kuwa, katika mida hiyo ya mchana, binti huyo alistukia amevamiwa na jamaa mmoja aliyeshikilia bisu na kujaribu kumtisha ili ampatie fedha na vitu vingine alivyokuwa navyo.

Inadaiwa kuwa baada ya kuona hivyo, mdada huyo wa Kizungu akakataa kutii amri kabla ya kuanza kupambana na lijamaa hilo lililokuwa na bisu kubwa, akitumia ujuzi wa kareti na judo alioupata kwao kwa nia ya kujilinda na mashambulizi kama hayo.

``Palitokea purukushani kali... mwanadada alipambana vilivyo na kumfanya mporaji ashindwe kutimiza dhamira yake.

Hata hivyo, tayari mwanadada wa watu alishachomwa kisu sehemu za kichwani na mkononi kabla ya kuwahishwa katika zahanti ya chuo na kutibiwa,`` akasema mmoja wa watu waliodai kuwepo katika eneo la tukio.

Hata hivyo, imeelezwa zaidi kuwa cha kusikitisha, licha ya askari wa chuoni hapo almaarufu kama `auxillary police` kuwepo muda wote kwa ajili ya ulinzi, bado lijamaa hilo lenye kisu liliweza kutokomea kusikojulikana na kumuacha dada wa watu akiendelea kutaabika na majeraha aliyoyapata.

Mwandishi hakuweza kumpata Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ili kuelezea tukio hilo baada ya asubuhi ya leo kushindwa kumpata kwenye simu yake ya mkononi.

Hata hivyo, jitihada za kupata maelezo zaidi toka kwa uongozi wa chuo hicho kuhusiana na usalama wa wanafunzi wake wakiwemo hao wa Kizungu na mali zao, zinaendelea kulindwa.

Aidha, imedaiwa na baadhi ya wanafunzi chuoni hapo kuwa hivi sasa, matukio ya wanafunzi wa Kizungu kuvamiwa ndani ya vyumba vyao na kuporwa pesa na mali yamekuwa ya kawaida na kwamba cha kusikitisha, hakuna hatua zozote zinazoonekana kuchukuliwa.

``Hii si mara ya kwanza... wanafunzi hawa wa Kizungu ambao hulipa pesa nyingi za Kigeni, wamekuwa wakiandamwa mara kwa mara na vibaka.

Wezi huvamia vyumba vyao na kuiba mchana kweupe, tena nje ya jengo kukiwa na askari wa chuo walio na sare na silaha za moto... inasikitisha sana,`` akasema mmoja wa wanafunzi waliozungumza na mwandishi wa habari hii.
• SOURCE: ALASIRI
 
Zaidi sana tukio hili limetokea mahali ambapo kuna kitengo maalumu cha ulinzi na usalama katika kampasi (auxilliary police) ambao wanawajibika kuwalinda wanafunzi na wafanyakazi.

Kuna haja ya hao auxilliary police kufanya kazi na si kukaa pale post kunywa chai. Wakati mwingine huwa najiuliza, kwa nini huwa hawawazuii watu wanaowatilia mashaka na kuwahoji kabla hawajafika ktk mazingira ya chuo? Si kitu cha ajabu kukutana na kichaa anakatiza kwenye macorridor huku akiimba au kupiga kelele. Cha ajabu kila utakapotaka kuingia UDSM kuna geti linalolindwa, yaani I mean kila entrance kuna geti na askari wasiopungua wawili, lakini vichaa wanapita hapo hapo kuingia ndani. Sasa unategemea wawasuspect vipi vibaka iwapo vichaa tu wanaoonekana dhahiri hata kwa mtu yeyote wanaruhusiwa kuingia?
 
Pole sana mdada.
Hili tukio linasikitisha sana na linatia doa la aibu katika taasisi hii nyeti ya elimu hapa nchini.
Kitengo cha ulinzi chuoni hapo pamoja na jeshi la polisi hawana budi kuhakikisha ulinzi kwa hawa wanafunzi wa kigeni na wanafunzi wote kwa ujumla.
 
extension block pana historia ya uvamizi wa aina hii toka enzi hizo, sijui kwa nini hapatiliwi mkazo katika ulinzi. Enzi hizo ilikuwa usishangae ukarudi chumbani ukakuta mali zako hazipo mf radio, fridge ndogo, jiko na hata sufuria. Hawa polisi wawajibike, sio mara ya kwanza tukio kama hilo kutokea.
 
Yawezekana na hao askari wana mkono wao katika hayo matukio. Inawezekana vipi saa 6 mchana mtu anavamiwa mhanga anapambana nae bila shaka alikuwa akipiga kelele pia kuomba msaada na hakuna msaada aliopata na mtuhumiwa anapotea kirahisi hivyo.

Hawa polisi huenda wanapanga njama makusudi na wao wanapata mgao wao kama zoezi linafanikiwa.

Ndio matatizo ya kuendekeza njaa haya...
 
Kuna rafiki yetu kutoka UK nayeye aliporwa juzi katika maeneo ya chuo kikuu mlimani na jamaa mmoja aliyekuwa na kisu, tuliripoti kwa auxilairy lakini mpaka sasa hakuna kilichopatikana. Jamaa alipoteza kadi za benki, visa, passport, laptop pamoja na documents zake.

wizi ulifanyika wakati akisubiri daladala katika mojawapo ya vituo vya basi ndani ya chuo...hii inanipa picha kuwa kuna mtandao mkubwa wa wizi na inawezekana hata wakawa wanashirikiana na wenyeji ndani...tuwe waangalifu...
 
Kuna haja ya hao auxilliary police kufanya kazi na si kukaa pale post kunywa chai. Wakati mwingine huwa najiuliza, kwa nini huwa hawawazuii watu wanaowatilia mashaka na kuwahoji kabla hawajafika ktk mazingira ya chuo? Si kitu cha ajabu kukutana na kichaa anakatiza kwenye macorridor huku akiimba au kupiga kelele. Cha ajabu kila utakapotaka kuingia UDSM kuna geti linalolindwa, yaani I mean kila entrance kuna geti na askari wasiopungua wawili, lakini vichaa wanapita hapo hapo kuingia ndani. Sasa unategemea wawasuspect vipi vibaka iwapo vichaa tu wanaoonekana dhahiri hata kwa mtu yeyote wanaruhusiwa kuingia?


Ah hao auxillary police kazi yao kubwa ni kudhibiti vifaa vikubwa kama furniture, TV kubwa n.k zisitoke nje kwani bila kuwa na kibali toka pale kamwe hupiti getini kutoka nje....... ingawaje kuna njia nyingi za mkato ambazo watu na magari yanaweza kupita na kutokomea (njia ya changanyikeni kutokea Ubungo Msewe)

Sishangai hao wezi wadogo wadogo kuwepo wakati hata magari yanaibiwaga pale. Mbaya zaidi si Auxillary peke yao wapo pale hata wale police kabisa si kuna kituo kidogo cha police pale Hill Park??...... kazi yao hawa sijui ni nini labda kuandikisha report ya vitu vilivyopokea.

Pole mzungu ... Mlimani si swari wala salama kama inavyodhania vibaka wanaovunja majumba kule kileleni wapo wengi ukiachilia mbali wanaokwapua nguo kambani na viatu milangoni
 
Kunahitajika kuwepo askari binafsi na wapelelezi wao naamini hao wataweza kufanya kazi inayotakiwa

niliwahi kushuhudia wezi wakiiba mafuta ya transformer kule hall 6 na umeme ukakatika hao polisi walipigiwa simu , wakafuatwa hawakuweza kufika katika eneo la tukio mpaka kesho yake usiku ndio wakaanza kujifanya wana track watu hao .

Pia kuna ile njia ya kwenda msewe kupitia hill park ile njia ni hatari sana , hukai wiki bila kusikia mtu kapigwa chupa kaporwa vitu vyake njia ile hawapiti askari wala kufanya jitihada zozote za kuhakikisha usalama unakwepo eneo lile .

Mwanzoni mwa mwaka huu kuna kijana alikamatwa ndani ya chuo kwa wizi yule kijana alijaribu kujiokoa kwa kuruka toka gorofani mpaka chini ila alivunjika mguu tuu alichukuliwa na askari haieleweki kesi yake iliishia wapi sasa watu kama hawa inabidi wajulikane
 
Duh bonge la aibu UDSM madesa matupu, hawa police nadhani ndio vibaka
wenyewe hawa au kama sio vibaka basi wanapewa kitundogo na hawa haiwezekani mtu avamiwe mchana na police jukumu lao nikuhakikisha usalama unakuwepo muda wote na kama wamewekwa kwaajili yakulinda mali zinazoingi anakutoka basi ipo haja yakuweka police wakuwalinda hawa wanafunzi na malizao tu.
 
Back
Top Bottom