MZUNGU ana access ya siri za serikali

5,000 acres of land had been set aside for the project. It will have a University complex, a conference center, hotel complex, a golf course and an enterprise-processing center for exports.

John Nolan mwingine! Tunaingizwa mjini. Nakumbuka kuna mwingine karibu apewe eneo lote la Jangwani ati anataka kujenga mahoteli n.k. Watatuumiza na ulimbukeni wetu!
 
Jamani mambo mengine yanahitaji uchanganuzi na si ....Nendeni Gabon mkaone wazungu walivyo ktk wizara za serikali ile na angalieni uchumi wa gabon yani wale jamaa maisha yao ni standard utafikiri upo Londan.

Uchumio kukua, ama kutokuwa siyo tatizo, nadhani tatizo ni mwananchi wa kawaida ananufaika vipi na hup uchumi na pia maisha yake ya kila siku yameinuliwa vipi na so called "uchumi kukuwa"!

Ukisoma takwimu nyingi za Tz utasikia ati uchumi wa tanzania unaongoza kwa kukua, je unatusaidia vipi sisi wanachi wa kawaida? kama kwa Tz imefikia kuwa hata kwenye mishahara tunabaguliwa nyumbani kwetu, basi inakuwa ukuaji wa uchumi au maendeleo ya nchi hayajatusaidia kabisa!

Je watu wa Gabon wa kawaida wanamaisha gani?, je kuwa na majumba kama London au Paris kwao kuna manufaa gani?, Je kuna vyuo vikuu vingapi?, vichanga vingapi vinakufa kabla havijafikisha mwaka? Je Wangapi wanaweza afford vitu kama Radio, TV, PC, Internet, Medical care, Shule nk? hivyo ndivyo vya kuangalia.

Tatizo la nchi nyingi za afrika ukuaji uchumi au maendeleo yanakuwa miji mikuu tu, au zile statretegic area tu, ukienda vijijini watu bado wanaishi kama enzi za ujima. Utakuta nchi inasifiwa kwa sababu tu wazungu wanaikomba na kukwangua kila kitu kama hawana akili nzuri vile, na mzalendo hana hili wala lile je hayo ni maendeleo?, Nchi kama Botswana, South Afrika, Gabon, Namibia ndo mifano kamili ya hiyo hali ambayo viongozi wetu wamekuwa wanaiendekeza. Kwangu hayo si maendeleo hata kidogo, na kamwe sitozifia hizo nchi.

Kitu cha mwisho ni kuw Omar Bongo ametawala miaka Arobaini (ndiyo 40 years) for me thats a joke!
 
"Hivi wakenya au wa Nigeria wanaweza kukubali huu upuuzi?"
GT,
Huu upuuzi unawezekana sehemu kama hizi zetu ambazo wengi wetu tumelala kama makondoo yaliyolala tu. We angalia jinsi Nigeria wanavyowachachafya Shell na BP.
 
Hivi ninani Shadow FOREIGN AFFAIRS MINISTER wa:
CUF
TLP
NCCR MAGEUZI
CHADEMA
NAREA (hivi bado wapo hawa)?

halafu mnasema eti ohhh WAPINZANI huu ni mwaka wao

In short naweza kusema kuwa CCM ni chama pekee kilichopo madarakani na kitaendelea kukaa madarakani kama tutaendelea kuwa na wapinzani style hii

Cant blame CCM kwa hili kwani jamaa hawana hata tone la presha na nashangaa ROSTAM anahangaika kumwaga mapesa kila kona for what? Huu upinzani usio na kichwa wala miguuu?

Ni rahisi kuwalaumu wapinzani as if wao pekee ndio wanaopaswa kulinda maslahi ya nchi,na kuwasamehe hao ambao in the first place ndio chanzo cha uzembe huu.Anyway,angalau kwa kuwalaumu inaonyesha ulikuwa na imani nao.Kama wizi wa mchana alioushikia bango Zitto kuhusu Buzwagi ulipelekea kutimuliwa bungeni,itakuwaje kuhusu ishu kama hii ambayo inaendelea kinyemela?

Hivi wakenya au wa Nigeria wanaweza kukubali huu upuuzi?

They are all corrupt African states ndio maana huko Nigeria yule jamaa mpambanaji wa rushwa ametolewa kwenye post yake na leo hii tunashuhudia Wakenya wakipoteza maisha yao kwa uking'ang'anizi wa fisadi nambari wani Kibaki.

Lakini Game Theory,kama ktk post yako kuhusu Saidi Kubenea umeonekana kushangazwa na mwandishi huyo "kupuuza" matishio ya mafisadi (na ukaishia kumlinganisha na Bhutto),sasa unategemea nani angependa kuishia kumwagiwa tindikali au kuuawa kama Bhutto kwa kushikilia bango ubaradhuli wa mafisadi?
DOUBLE STANDARDS AU.....?????
 
naona humu mnachanganya maharage na mbaazi,angalieni anchofanya kwanza kabla ya kuanza kulaumu na kuja theory ambazo hata mtoto mdogo anajua ni majungu tuu,wengine mmejaribu kuhusisha failure ya uchumi wetu na watu kama hawa,hakuna cha siri ya serikali hapo inatoka kuingia kupitia kwa watu kama hawa..technically ni marafiki tuu wa Tanzania ambao wanaweza kutumwa vitu vidogo vidogo na serikali onbehalf,mnakumbuka Alex Khalid? basi ni kama hawa jamaa tuu hakuna hujuma hapo wakuu wala secret service na Kikwete akiwasikia atawacheka sana
 
cHOVEKI
Maisha ya wana gabon yapo far better kuliko ya waafrika wengi yapo karibu sana na middle class ndio utaona wataalam wengi wa bongo wasipokimbilia ulaya au marekani basi wanakimbilia huko
kwanini wakimbilie huko ??waswahili wanasema panapofuka moshi chini kuna moto.

Harafu tatizo la Omar bongo,Gadafi kuishi madarakani ni exceptional yawezekana wanavyolinda uchumi na wanachi wao ndio kisa cha kuendelea kuwepo madarakani kubadirisha viongozi kila mara kama TZ si kigezo kwamba nchi ile ina demokrasia ama maendeleo BIG NO.

Huyo mzungu wa uholanzi mimi naamini anajitolea na watz ilitakiwa kabla ya kuanza kulaumu inabidi wapate details zake kwanini amejitolea mfano nikijenga nyumba yangu sehemu iliyo na miundo mbinu bofu bofu kwa ajili ya biashara hivyo basi ili niwe na biashara ya uhakika lazima nijitolee pia kurekebisha miundo mbinu iliyopo tena kwa gharama zangu sasa ikitokea nikajitolea kurekebisha miundo mbinu hiyo harafu wanachi wa mahali pale wakaanza kunituhumu eti sisitaili maana ile ni kazi ya TANROAD ama DAWASCO mie nitawashangaa sana tena sana.

kitu kingine nani ana uhakika kuwa yule mzungu si mtanzania hivi ina maana siku hizi kazi zina enda kwa mfumo wa rangi ama sifa alizonazo muhusika.
Uchumi ulio na manufaa kwa wananchi ni wananchi wenyewe kukubali kuondokana na umasikini yani kupiga kazi usiku na mchana usipofanya kazi hata kama nchi ina uchumi mkubwa kiasi gani maisha yako bado yatakuwa duni tu,huwezi subiri maisha bora kijiweni mbona ulaya penyewe wapo omba omba ??

Hawa watu wanaokwenda ulaya na kazi wanazofanya huko ni ngumu na hakuna kulala sana sana wanaegesha tu masaa mawili ma tatu mie na uhakika hata akiwa bongo akafanya kazi kwa kasi ile bado angelifanikiwa sana wenda kuliko alikokuwa.

Hivyo siri ya uchumi ulio na manufaa kwa wananchi ni kuchapa kazi kweli kweli NO PAIN NO GAIN
 
cHOVEKI
Maisha ya wana gabon yapo far better kuliko ya waafrika wengi yapo karibu sana na middle class ndio utaona wataalam wengi wa bongo wasipokimbilia ulaya au marekani basi wanakimbilia huko kwanini wakimbilie huko ??waswahili wanasema panapofuka moshi chini kuna moto......

Wa tanzania kukimbilia huko hakumaanishi ati wameendelea!, Baadhi tu habari itakayokuonesha kuwa Gabon ni sawa na nchi nyingine za afrika;

....Gabon lacks roads, schools, and adequate health care, yet the oil-rich country has lined the pockets of its ruler, who, according to the French weekly L'Autre Afrique, is said to own more real estate in Paris than any other foreign leader. Despite his reputation for corruption and authoritarianism, Bongo has a strong national following. In July 2003, the country's constitution was changed, allowing Bongo to be reelected indefinitely; that year, he changed his name again, to El Hadj Omar Bongo Ondimba. In Dec. 2005, he was reelected for another seven-year term.
ECONOMY
Gabon's economy is dominated by oil. In spite of the decreasing oil revenues, little planning has been done for an after-oil scenario. Gabon public expenditures from the years of significant oil revenues were not spent efficiently. Overspending on the Transgabonais railroad, the oil price shock of 1986, the CFA franc devaluation of 1994, and low oil prices in the late 1990s caused serious debt problems. Gabon has earned a poor reputation with the Paris Club and the International Monetary Fund (IMF) for the management of its debt and revenues. Successive IMF missions have criticized the government for overspending on off-budget items (in good years and bad), over-borrowing from the Central Bank, and slipping on the schedule for privatization and administrative reform. In September 2005, Gabon successfully concluded a 15-month Stand-By Arrangement with the IMF. Gabon seeks a multi-year successor arrangement....

http://www.infoplease.com/country/profiles/gabon.html
http://www.imf.org/external/index.htm
 
Lakini Game Theory,kama ktk post yako kuhusu Saidi Kubenea umeonekana kushangazwa na mwandishi huyo "kupuuza" matishio ya mafisadi (na ukaishia kumlinganisha na Bhutto),sasa unategemea nani angependa kuishia kumwagiwa tindikali au kuuawa kama Bhutto kwa kushikilia bango ubaradhuli wa mafisadi?
DOUBLE STANDARDS AU.....?????

SAIDI KEBENEA tatizo lake siyo ku expose UBADHIRIFU bali tatizo lake ni njaa

Alienda kwa hao ambao kila kukicha anawaandika kwenye magazeti wakampa pesa za kumpooza mbona hakutoa kwenye gazeti kuwa alipewa RUSHWA?

Huyu mtu all of a sudden watu wanamwonea huruma lakini cha ajabu hakuna anyesema kuwa naye yuko kwenye payroll sema tatizo lake ni pale alipoambiwa apunguze eyey akaamua kuwa ataongeza kwa kisingizio hapati matangazo

walimtumia MSG kupitia gari lake hivyo yeye alishajua kuwa hana muda mrefu na zaidi angweka wazi kuwa hao wanaopinga CHANGES wanajaribu kumnyamazisha...akakaa kimya huku akiendelea kuvuta pesa sasa juzi kafarakana nao tena ndio yamemkuta haya na kusema ukweli jamaa hawataki kumwondoa kwani its not in anyone's interest kufanya hivyo

Nilimfananisha na Bhutto ambaye alijua nani wabaya wake lakini still akaamua kujiachia mpaka wakamwondoa kwa kesi ya SAIDI ni kuwa hawajataka kumwondoa lakini still ni nuisance kwa jamaa
 
Wa tanzania kukimbilia huko hakumaanishi ati wameendelea!, Baadhi tu habari itakayokuonesha kuwa Gabon ni sawa na nchi nyingine za afrika;



http://www.infoplease.com/country/profiles/gabon.html
http://www.imf.org/external/index.htm

untitled0.jpg
 
Awali nakupongeza sana ndg. Game Theory kwa kuanzisha uzi huu hata hivyo mimi ningependekeza kuwa kichwa cha habari kingekuwa
ASIYE MTANZANIA NI KONSULA WA TANZANIA UHOLANZI maana kwa kusema MZUNGU ana access ya siri za serikali, mjadala unaanza kukwepeshwa kwa kuuliza maswali kama vile je Mzungu hawezi kuwa raia wa Tanzania? na pili ni siri gani za serikali zinazotumwa Uholanzi n.k

Pili ingawa haina maana yeyote kubwa, niseme kuwa hii hoja niliianzisha mimi katika uzi mwingine ambapo Lunyungu alikuwa anatutaarifu kupitia jukwaa hili la siasa katika kichwa cha habari Hatimaye JK kutinga Holland.
Aidha alitutaka tumwandikie maswali sirini ili ayatume kwa 'vijana'wake waje mamuulize JK. ndipo nilipotoka nyikani na sauti ya unabii nikisema, najinukuu;


HAKUNA HAJA YA KUTUMA SWALI HILI SIRINI NA KAMA YEYOTE ANASOMA HAPA NA YUKO KARIBU NA PREZO AU MAMBO YA NDANI AU UBALOZI (UBELGIJI) NAWASOGEZEA SWALI HILI AMBALO NDUGU ZANGU WA HUKO WANAULIZA KILA SIKU, LIULIZWE AU LISIULIZWE RAIS AJIANDAE KUWA NA MAJIBU AU MAELEZO YA SWALI LIFUATALO:

KWA NINI MSAIDIZI WA BALOZI (KONSULA) WA HUKO NETHERLANDS NI MDACHI BADALA YA KUWA MTANZANIA???? NA NI NANI ALIYEMTEUA NA ANAWAJIBIKA KWA NANI MAANA UBALOZI WA UBELGIJI HAUKO JUU YAKE.

Hakika hilo swali langu halikujibiwa, ingawa mwenzetu alijaribu kutoa maelezo ya kuongeza maswali zaidi badala ya majibu maana sasa aliibuka akionyesha kuwa hakuna linaloweza kufanyika maana eti jamaa kesha penya kwenye siasa zetu na rasilimali, ni mfanyabiashara mkubwa na hata JK anamtegemea kwa namna moja au nyingine.
Nilipoomba ufafanuzi wa kumtegemea kivipi sikujibiwa. Anyway leo baada ya hili kuleta kwa upya katika uzi wake wa kipeee naomba kusema yafuatayo. Kutoka katika vyanzo vyangu vifuatavyo:-

1. Mfanyabiashara Mdachi sasa,aliyekuwa Mtanzania kwa kuzaliwa na akiwa mtumishi wa serikali ya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 90.
2. Mtanzania afanyaye ubalozi wa Tanzania Ubelgiji
3. wanafunzi watano wanaosoma au waliowahi soma hapo Uholanzi kupitia scholarship za NUFFIC

Ninataarifa za kuaminika kuhusu hili na ninatamka yafuatayo:-

1.Suala la yeye kuwa mfanya biashara mkubwa na Tanzania, na kuelewana au kuwa rafiki na wakubwa fulani silifahamu vizuri na wala kwangu si tija maana hakuna anayezuia Wakuu wa nchi kuwa na marafiki au kuzuia mtu kuwa rafiki ya mkuu wa nchi fulani so long as urafiki huo hauna maana ya kuleta ukiukaji au udhalimu wowote. Lakini,

2. Ni kweli kuna mwanaume asiye mtanzania afanyaye kazi kwa wadhifa wa Konsula kwa jina bwana F.J.Hakkenburg. Huyu jamaa ni Mdachi. Mara kwa mara akutanapo na kundi la Watanzania hujitahidi kuongea misimu na misamiati ya mitaani haijulikani kama huwa anafanya hivyo kwa kuipenda kweli lugha ya kiswahili toka rohoni au huwa ni mbinu yake ya kuzuga kadamnasi.

3.Ni kweli hatuna ubalozi Uholanzi, lakini ni nani anaweza kumwajiri (au kumpa kazi) mtu kuwa KONSULA WAKATI YEYE SI RAIA WA NCHI YETU TANZANIA? Eti kuna mtu humu alijitahidi kueleza kuwa hausika na mambo makubwa bali utamaduni (WA NANI SASA?) na biashara (KWA FAIDA YA NANI?). Huyu jamaa si kweli kuwa eti ana kazi ya kuwapa watu wajaze fomu kwa ajili ya visa tu, HAPANA, YEYE TOKA ZAMANI SANA AMEKUWA ANAKUSANYA FEDHA NA KUWAPA WATU WANAOTAKA VIZA HAPO HAPO OFISINI KWAKWE AMBAKO HAKIKA NI GEREJI NA DUKA KUBWA LA KUUZA NA KUNUNUA MAGARI YA FAMILIA YA VAN- VLIET (http://www.vanvliet.nl/). KWA MAANA NYINGINE HUYU JAMAA ANA MUHURI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ANAOUGONGA KWENYE PASI ZOTE ZA KUSAFIRIA ZA WOTE WANAOKWENDA TANZANIA (kwa taarifa yenu Wadachi ni miongoni mwa watalii wengi katika vivutio vya nchi yangu Tz). YEYE ALIUTOA WAPI NA NI NANI ALIYEMKABIDHI NYENZO HIYO YA SERIKALI? LABDA KAMA AMEANZA HIVI KARIBUNI BAADA YA WATU KUANZA KUULIZA KICHINI CHINI, MIAKA YOTE AMEKUWA ANAWASILIANA MOJA KWA MOJA NA MAMBO YA NDANI DAR, JE NI NANI AMEKUWA ANAMKAGUA KUWA MAWASILISHO YOTE ANAYOKUSANYA NDIYO KWELI ANAYOWASILISHA? KWA NINI AMEKUWA HAWAJIBIKI CHINI YA UBALOZI WA UBELGIJI?

4. Kuna kero nyingine moja iliyowasilishwa na vyanzo vyangu (Wanafunzi). Ok, najua kila nchi Watanzania kwa jinsi wanavyojiorganise wenyewe ughaibuni, huwa wanaungana na wenzao Watanzania kwa kusherehekea pamoja siku mbalimbali za Kitaifa. Mara nyingi ubalozi huwa unahusika/husishwa kwa namna moja au nyingine. Sasa huko Uholanzi ni huyu Mdachi wala si ubalozi wa Ubelgiji wenye kauli wala kuhusika. Mara nyingi yeye humuita jamaa mmoja Mtanzania mdhamini wa Wabongonet.nl ambaye ni mwanachama mzuri wa hii net pia na humuagiza kuwa yeye anataka Watanzania washerehekee siku ipi, wapi na saa ngapi. Sasa huwa anampa taabu sana huyo jamaa maana watu unajua tena katika karne hii, tena wasomi huwa wanamchallenge sana huyo 'kiongozi' kuhusu hayo matangazo yake. Lakini niseme kuwa labda kwa sababu ya Ubalozi wetu kukaa kimya na kwa sababu huwa huyu Mdachi anatanguliza CHANGA LA MACHO KWAMBA YEYE NDIYE ATAGHARIMIA SEHEMU KUBWA YA GHARAMA ZA SHEREHE, basi watu wananywea tu na kuchanga Euro 10 hivi na wanakutana chini ya matakwa ya huyu Mdachi. Kama kuna mtu anabisha aeleze hapa kwa nini mfano alazimishe watu kusherekea NYERERE DAY pekee NA ISIWE UHURU DAY AU MUUNGANO DAY AU SIKU ZOTE HIZO NA ZINGINE ZA KITAIFA? Je ni lini Watanzania wa Uholanzi waliazimia iwe hiyo? Zaidi ya hapo huwa hata kwa kiburi chake anaamua KUTOMWALIKA BALOZI, Je mtu ataniambiaje kuwa anawajibika kwa Balozi???

5. Wanafunzi wasomao Uholanzi walisha wahi kuuliza kuwa 'je fedha anazochangia wakati wa sherehe ni kutoka mfukoni mwake kama Mdachi awapendaye Watanzania au ni mahesabu yanayowasilishwa baadaye (labda na mazidisho) kama matumizi ya ofisi yake kutoka makusanyo ya visa kwenye serikali yangu?' Swali hili yeye binafsi hakuwahi kulijibu. Yaani analikwepa, lakini mwakilishi wake (mdhamini wa Wabongonet.nl) aliwajibu kuwa, hakika hiyo huwa anaiweka kama bill ya matumizi ya ofisi yake na kuisukumiza huko Dar. SASA HAPO NDIO KUTAMU! JE NI NANI AMBAYE HUWA ANAMUIDHINISHIA BAJETI YAKE? MAANA HAWAJIBIKI UBALOZINI? NA ENDAPO SI FEDHA ZAKE KWA NINI SASA AWAAMLIE WATANZANIA KUSHEREHEKEA SIKU NA KWA STAILI YAKE (mfano masaa matatu tu na kufukuzwa ukumbini)? Nasema kuwa kama kuna mwenye majibu ya maswali haya ajibu humu wala hatuna haja ya kusubiri eti rais aje tumuulize maana mengine yanatuhusu sisi wenyewe si kila kitu ni cha JK!

Ndg. zangu ofisi hiyo na majukumu ya Hakkenburg kama mwakilishi wa Serikali yetu kamwe hayawezi pachikwa jina la usamaria mwema au eti anatoa usaidizi kwa sababu ya umaskini wetu wa kutokuwa na mtu wa kufanya kazi hiyo! Huu utakuwa uvivu wa kufikiri maana kwa nini mfano serikali isiruhusu hata mtu mmoja tu toka ubalozini Ubelgiji aje aishi uholanzi (hakuna tofauti kubwa) na afanye kazi hizo? Pili kama ni kusubcontract kazi fulani basi kwa nini kazi hiyo isingetangazwe na sifa ya kwanza iwe ni kuwa mhusika ni lazima awe Mtanzania? Mbona kuna Watanzania kibao ughaibuni wafanyabiashara kama yeyena wenye elimu nzuri ya diplomasia ya uchumi ambao wana uwezo wao tu lakini hawajigambi?

Afterall, kuna Watanzania wengi zaidi Uholanzi kuliko ubelgiji na pia Wadachi wamekuwa na mahusiano ya karibu kwa kutoa misaada mbalimbali kwa serikali yetu kuliko Ubelgiji na Wadachi ni miongoni mwa Watalii wengi Tanzania kuliko Wabelgiji, sasa kwa nini kama ni kubana matumizi Ubalozi usihamie Uholazi na Ubelgiji ndo wawe na Konsula MTANZANIA na si Mflemishi au sijui Mdachi?

SASA MWENYE KUPINGA HII HOJA AJE HAPA NA UTHIBITISHO MADHUBUTI KUWA HAKKENBURG NI MTANZANIA NA ALIPELEKWA ROTTERDAM KUPITIA UTARATIBU WA KAWAIDA WA KUSHIKIZWA (ATTACHEE)KUTOKEA UBALOZINI AU MAMBO YA NDANI NA HUWA ANAKAGULIWA SAWIA MAKUSANYO YA MAPATO TOKA VIZA ANAZOTOA!! VINGINEVYO HILI NI SUALA LA KUSAHIHISHA KOSA HILI MARA MOJA NA KUSONGA MBELE KAMA TUNATAKA KUWA NA MWAKA WA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA, UNABII TUNAOUTEGEMEA!
 
Mkuu Nabii,Maelezo yako ni mazito na pengine Ukweli huo ulioandika haujulikani huko Foreign.Kusanya Ushahidi wa kutosha ikiwa ni pamoja na huo uloandika hapa,na moja kwa moja wasiliana na watu wa Nyumbani ni wazi kwamba suala hilo litashughulikiwa.

Wasiliana moja kwa moja na Balozi Sanga kwa #s 22 2111906 -8 au 22 2111909-11 Au wasiliana na watu wa Ubalozi Brussels ili wakupe contact ya Mama Msuya ambaye yupo huko Luxembourg kikazi,Mama Msuya ni Mkurugenzi wa Kanda ya Ulaya anaweza kukusikiliza na kutafuta Ufumbuzi wa Tatizo hilo.

Habari nzima inasikitisha lakini ndio mambo ya kwetu,Nakuhakikishia kuwa habari itafika kwa wahusika,hata kama Tatizo halitotatuliwa lakini Lazima ujumbe ufike kwenye meza zao.
 
Mwawado,
Asante Sana Maana Kweli Inauma Sana Ni Afadhali Tujaribu Kushughulikia Tatizo Kuliko Kukalia Kutoa Kasoro Tu Na Kuogopa Tu Eti Kwa Vile Sijui Mtu Ni Tajiri Hakuna Kitu! Nitafikisha Ujumbe Mara Moja
 
YEYE TOKA ZAMANI SANA AMEKUWA ANAKUSANYA FEDHA NA KUWAPA WATU WANAOTAKA VIZA HAPO HAPO OFISINI KWAKWE AMBAKO HAKIKA NI GEREJI !

Watanzania JF,

Kama hizi habari ni za kweli

Basi haya ni mambo aibu sana- hata kama nchi yetu ni maskini, NI UKOSEFU WA HESHMA NA UDHALILISHAJI WA HALI YA JUU MNO KUTUMIA GEREJI Kama Ofisi Jina na Mhuri wa Jamhuri vinapotumika nje kama Holland!

Ni bora hiyo sehemu ifungwe!

Foreign na Mambo ya ndani Mko wapi? Je haya mnayajua?

Mzalendohalisi
 
1. Consular sio lazima awe Mtanzania
2. Kama ni kweli anakusanya mapato ya Visa na then hiyo ni inahitaji monitoring ya uhakika.
 
1. Consular sio lazima awe Mtanzania


sababu gani tuna mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anapata access ya siri za serikali? Kama isues ni budgeting kwa nini tu risk NATIONAL SECURITY ili kusevu vijisenti vya kuwa na ubalozi pale?

The bottom line jamaaa si mtanzania na hiyo Tayari inanifanya ni feel very uncomfortable not only na the whole episode lakini inanifanya ni conclusde kuwa hili pamoja na catalogue zinginezo ambazo clearly zinaonyesha kuwa kuna massive SECURITY BREACHES zinanifanya niamini kuwa:

1) JK kama kamanda mkuu wa nchi CANNOT be trusted with OUR NATIONAL SECURITY japo aliwahi kuwa mwanajeshi

2) USALAMA WA TAIFA nao eidha wako overuled na IKULU au hawafanyi kazi zao ipasavyo

3) WAPINZANI nao cannot be trusted na issues zinazohusiana na NATIONAL SECURITY kwani nao ni mapopulists

4) MEDIA Tanzania nao cannot be trusted at any cost kwenye hili

4) KUNA umuhimu wa kuwepo kwa splinter group eidha nje au ndani ya serikalini amblo litakuwa ni influential katika kuput forwards our national interests kuliko kuwaachia hawa wanasiasa jukumu la kurun nchi


5)FOREIGN inatakiwa ifanyiwe top down revamp na tunatakiwa tujue vilivyo jinsi wanavyospend pesa zao ni akina nani ambao walipeleka recommendations kama hizi kwa MKAPA
 
Mimi naendelea kuwashangaa wa Tanzania, jamani kwani mzungu kuwa na access ya siri za serikali ni ajabu kwa hapa kwetu? Kwani hamjui awamu ya kwanza, awamu ya Nyerere, kuwa personal secretary wake alikuwa ni mama wa kizungu, huyo mama alikuwepo toka kijana mpaka kazeekea Ikulu kwa Nyerere, Jee ni nani mwenye access ya siri nyingi na nzito? huyo mzungu wa ubalozini au yule mzungu wa Nyerere? Jamani nyinyi mnategemea nini? wakati system ni ileile? au hamfahamu system ni nini?
 
watu humu ni kichekesho sana as if mnachoongea ni kweli na mnajua kumbe pumba tupu,hamuulizi hata utaratibu uko ndani kisheria au laa,mmeanza tuu kurusha mawe,mmenikumbusha zamani watu wakiona mzungu kashika camera basi wanajua jasusi,naona consipiracy za salender Bridge zinaendelea humu....you guys grow up!
 
Nabii
Tatizo unatumia hisia zaidi ya uhalisia ,
Ninavyofahamu mie Viza hua haigongwi mhuri ila inaandikwa habari mhimu za msafiri na balozi Na hua inagongwa mihuri airport sasa we hizi habari za mihuri unazitoa wapi?? labda nieleweshe zaidi Viza za TZ hua zinagongwa mihuri na balozi?? na kama ndiyo wewe huoni kuna uwezekano hua zimegongwa mihuri tayari anapokabidhiwa??

Pili mapato yepi yakaguliwe?? mapato ya kukusanya fedha za VIZA?? hebu acheni vichekesho
kwani huyu jamaa pia ana machine ya kutengeneza viza za tz?? kama ndiyo basi unauhalali wakusema akaguliwe lakini kama hana machine hiyo basi unachosema kukaguliwa hakiingii mkichwa kwani kama anapelekewa idadi fulani ya viza na bei ya viza ni constant and not variable basi amount inajulikana mkaguzi tena wa nini ktk swala rahisi kama hilo???

Kuhusu kuchangia pesa ktk sherehe ebwana huyo jamaa mbona anafanya good work Sie tumeomba balozi wetu yule paleeeee ujerumani aje tu ktk siku ya TZ day bila mchango wowote sie ndio tunachanga zaidi ya miaka mnne kila mwaka anagomaaaaaa haya tuma hata mwakilishi kagomaaaaaaa ok kama ndivyo basi tuchangie basi angalau vijisenti fulani kagomaaaaaaa.

Mbaya zaidi si unajua ule ubalozi unahudumia nchi nyigi yani cheki,poland,yani nchi kibao ktk hili sakata la kubadirisha passport wanafunzi wakaomba atoke basi ofisa mmoja hapo ujerumani azunguke ktk nchi hizi achukue hizo figure print wamegomaaaaaa
Eti wanataka mtu utumie zaidi ya EURO 400 yani kama laki sita hivi uende tu pale ujerumani ukachukuliwe figure print wakati huo huo wanajua kabisa kamkopo wanakopata wanafunzi ni kiduchuuuuuu tena kukapata kwa kuandamanaaaaa na bado wanataka kateketee kwa kuchukua vidole tu sasa kwanini wasitume mtu azunguke na gharama wazisukumie serikali kama huyo mholanzi afanyavyo??????
Mind u walio ujerumani ubalozini ni watanzania na si wajerumani
 
mkamap/Koba,

well said guys....................in addition

1. Fact: Si kweli kwamba Consular huyo huandaa sherehe ya Nyerere day pekee.........
 
Back
Top Bottom