Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzumbe University Is Best?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by falesy, Oct 9, 2006.

 1. f

  falesy JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2006
  Joined: Mar 15, 2006
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kutokana na competence ya staff na ubora wa degree za mzumbe; imepewa ruzuku (exemptions) ya mitihani ya ACCA baraza la juu kabisa duniani la mitihani ya uhasibu.

  UDSM, IFM wameomba wamepigwa chini, na kwa taarifa fupi ni kwamba kitakuwa ni chuo cha kwanza na cha mwisho Tanzania kufundisha review Classes za ACCA siyo CPA(T) ni ACCA.

  sasa wanaoibeza mzumbe wana nini??????????????
  kama untaka kuw professional accountant kasome Mzumbe wewe usisikilize majungu hayo yaani ACCA waikubali mzumbe waikate UDSM bado ung'ang'anie mzumbe feki basi weqwe mwenyewe hata akili yako ni feki.


  The exemption awards listed below apply to the following criteria.
  Institution: MZUMBE UNIVERSITY
  Programme: BACHELOR OF ACCOUNTING
  Assessment: BACHELOR OF ACCOUNTING
  (Graduates 01/01/2006 to 31/12/2007)
  Level of Completion: FULL COURSE COMPLETION

  --------------------------------------------------------------------------------
  ACCA Qualification: Professional Examination Route (PER)

  --------------------------------------------------------------------------------
  This programme is acceptable for registration on PER
  PLUS
  Exemption on the basis of FULL COURSE COMPLETION:

  Paper 1.1 - Preparing Financial Statements
  Paper 1.2 - Financial Information for Management
  Paper 1.3 - Managing People
  Paper 2.1 - Information Systems
  Paper 2.2 - Corporate and Business Law
  PLUS

  Paper 2.4 - Financial Management and Control on the basis of COST & MANAGEMENT ACCOUNTING (ACC271) Plus MANAGERIAL FINANCE (ACC251)
  Paper 2.4 - Financial Management and Control on the basis of COST & MANAGEMENT ACCOUNTING II (ACC222) Plus MANAGERIAL FINANCE (ACC251)
  Paper 2.5 - Financial Reporting on the basis of FINANCIAL ACCOUNTING II (ACC202) Plus FINANCIAL ACCOUNTING III (ACC203)

  --------------------------------------------------------------------------------
  ACCA can take no responsibility for courses undertaken on the basis of the information contained within these web pages. Students are strongly advised to obtain written confirmation of their exemption status from ACCA before embarking on any course of study.
  Students are advised to monitor this database regularly as ACCA's exemption policy is subject to change and assessments may be added or revised without prior notice.

  Exemption will be confirmed at the time of a student's initial registration with ACCA.

  Exemption will only be considered on provision of a student's completion certificate, academic transcript (and official English translations, where appropriate).


  --------------------------------------------------------------------------------
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2006
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,556
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 48
  Exemption will be confirmed at the time of a student's initial registration with ACCA.

  Falesy, Mimi nina ACCA. mshkaji sijui umri wako ila unahitaki kupigwa msasa wa nguvu mnooooooooo!

  ACCA wanatoa exemption kwa kuangalia pia working experience apart from cheti. Kwahiyo mnaweza kuwa na cheti sawa mkaanza kwenye level tofauti.

  Sitochoka kukupa shule kijana. Unakaribishwa kuuliza maswali.

  FD
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Oct 10, 2006
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,661
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 63
  Dah! FD balaa... Yangu mie macho!
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Oct 11, 2006
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 8,058
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 48
  Kinachonikera kuhusu mzumbe ni kutokana na walimu wake wengi kuwa na digrii za kuokoteza kutoka vyuo uchwara uchwara kama Commonwealth Open University na Pacific Western University; utashangaa kuwa hata Vice Chancellor wa Mzumbe ana Ph.D. ya namna hiyo hiyo ya kuokoteza. Hilo tu ndilo tatizo langu kuu kuhusu Mzumbe. Miaka miwili tu iliyopita kuna mwalimu mmoja wa Mzumbe alikuwa aksioma Ph.D huko ulaya ikamshinda, akaamua kwenda kununua moja kutoka Commonwealth Open University kwa $5600 papo kwa papo. Sasa kama walimu wenyewe wanashindwa shule halisi na kukimbilia za mkato, kuna kila sababu kwa watu kushuku uwezo wao wa kufundisha.
   
 5. m

  mTz JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2006
  Joined: Aug 20, 2006
  Messages: 407
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hao "vigogo" wa Mzumbe wanaruin kabisa reputation ya hicho chuo. Kitu mbacho nimeshinwa kuelewa ni kwa nini serikali inakodolea macho tu hili? hala hala MU nayo isije kuwa one of the degree mills!
   
 6. f

  falesy JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2006
  Joined: Mar 15, 2006
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni kweli inaangalia experience ya kazi lakini for thjis case Mu has been granted. conglats fikiraduni kwa kuwa na ACCA. huo ndo ukweli.
   
 7. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 8. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 599
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 18
  Kuna huyu mtu anaitwa Dr.KOMUNTE pale Mu hicho ndo kichwa cha Accounting na ndo alipewa jukumu la ACCA Bongo na hiyo haifanyi MU kusafishika kwa Uozo uliopo pale,kuna mengi sana yanayoendelea na huwa nashangaa serikali iko wapi,Hata leo hii ukienda kwa Wakurugenzi wa NSSF watakwambia,jinsi walivyokosa nafasi ya kujenga Hostel na hadi leo Mu wanaendelea na Mfumo wa kusepetua mihula.
   
 9. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #9
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 655
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 18
  Falesy hujui unachoongea.

  Ni ukweli kuwa Mzumbe wanapewa exemption 7 huku UDSM wanapewa exemption 5 au 4 lakini sababu uliyotoa si ya kweli.

  UDSM wanatumia sylabus tofauti sana na ACCA katika accounting. UDSM wanatumia style ya kiamerika iliyokuwa modified ili kukidhi matakwa ya ndani ya Tanzania zaidi kitaaluma wakati ACCA body ni ya UK.

  Sababu kubwa ni kwamba UDSM hawajataka kufuata sylabus iliyopendekezwa na ACCA tofauti na Mzumbe ambao sylabus yao yote ni copy and paste ya ACCA.UDSM hawajawahi kuomba watumie mtaala wa ACCA ili wanafunzi wao wawe wanapewa exemption zaidi. Hivyo ni UONGO kusema UDSM waliomba wakakataliwa.

  Pia UDSM hawajawahi kuomba kufundisha ACCA Tanzania kwani wao wamejikita katika kuzalisha wanataaluma ambao baadae wanaenda kufanya professional examinations baada ya kumaliza Bachelor zao. Kufundisha ACCA chuo kikuu ni mradi unaojitegemea ambao hauhusiani na Degree programs. Mfano mradi wa ACCA pale Mzumbe ni mradi wa kujinufaisha wachache (ambao pia umedoda kwani value for maoney haipo,bei kubwa walimu vilaza).

  Kwa taarifa yako hata vyuo vya vichochoroni vimepewa kibali cha kufundisha ACCA duniani kote na hata Tanzania kama FTC karibu na CBE pale na A3 professional studies karibu na CCM vijana building. Hivyo Mzumbe kufundisha ACCA hakukipi chuo hichi ubora kwani ACCA wanatoa kibali kwa chuo chochote ilimradi una walimu ambao wako qualified(Mzumbe wanao na UDSM wanao). HIVYO MZUMBE HAKITAKUWA CHA KWANZA WALA MWISHO KUFUNDISHA ACCA.

  ACCA ni association ya wahasibu na ni member wa IFAC (International Federation of Accountants) na NBAA ni member pia. NBAA inatoa CPA(T) ambayo inatambulika na IFAC kama ACCA.

  Mzumbe wao ni watu wa short cut,kama chuo kikuu huru ni udhaifu kuwa kinatumia mtaala wa bodi ya UK ili tu wanafunzi wao wapate shortcut hata kama mtaala huo haukidhi matakwa ya ndani ya nchi. Wahasibu sasa tunatumia IFRS lakini IFRS lazima zikidhi matakwa na mazingira ya TAnzania dniyo maana NBAA imepewa jukumu na IFAC kufanya regulation ya compliance of IFRS na pia kutoa interpretation in case kuna tatizo katika application.

  Shortcut hizi zinawafanya wanafunzi wa Mzumbe wawe na GPA ambazo hawaendani nazo. Mzumbe inajulikana kwa kutoa first class za bure bure. Kuna mifano mingi sana. Mfano kuna jamaa zangu wawili ambao walidisco mlimani lakini mzumbe wamemaliza na first class. Naomba unipe mfano mtu aliyesoma Mzumbe akadisco akaja akapata first class mlimani.

  Pia kama ukilinganisha matokeo ya o level,advance na chuo kwa mtu aliyesoma mzumbe university utakua mara nyingi hakuna consistency kitu ambacho si cha kawaida. Utakuta mtu mara nyingi ana Div 3 o level, Div 3 advance,chuo first class. Ndiyo maana hata big four accounting firms (PwC, Deloitte,E&Y na KPMG) wanaangalia matokeo kuanzia form four hadi chuo ili wajue uko real au unatoka chuo feki.

  UDSM ukichukua matokeo ya mtu ana first class chuo,huna haja ya kuuliza o level na advance alipata ngapi,lazima tu alikuwa na div one tena za point kali sana. Consistency ni kubwa sana kwenye matokea ya NEC na UDSM.

  Mzumbe siyo chuo kibaya ila siyo chuo kizuri kama kinavyojiuza. Mzumbe mnajiuza sana (Kizuri......Kibaya......). Professional firm moja iliajiri watu kwa kuangalia matokeo ya chuo pekee,watu walivyofika kazini hata fixed asset register hawajui ni nini.

  ACCA watu wa UDSM wanamaliza pamoja na Mzumbe japo Mzumbe wanafanya masomo 7 na UDSM 10. Mara nyingine unakuta wa UDSM wanamaliza mitihani 10 kabla ya watu wa Mzumbe walioanza nao hawajamaliza 7. Hii inaonyesha ubora wa wanafunzi wa UDSM.

  Mfano mimi nimemaliza ACCA huku nimewaacha jamaa wa Mzumbe tulionza nao hata mmoja hajamaliza. Pia hata watu wengi waliomaliza mbele yetu bado wanasota na masomo saba. Kama hizo first class ni halali na wote tunafanya kazi mazingira yale yale mbona hawa jamaa wanasota sana?

  Biashara matangazo,ukitaka shortcut nenda Mzumbe,ila ukitaka elimu kwa hapa Tanzania,wewe mwenyewe unajua kwa kwenda.

  Hata MBA yao hadi imepoteza sifa. Imekuwa kibiashara zaidi,wanachotaka ni hiyo ada yako tu wala hawataki kutoa MBA kwa wanaostahili kuipata.
   
 10. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #10
  Jan 26, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 974
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ACCA is not a big deal again.Ni money making machine,hasa kwa wanafunzi wa Asia,afrika na sasa big player China.Ni chombo cha waingereza(UKOLONI MAMBOLEO).
  Huwezi kupata Mzungu wa say Sweden,Norway etc anasoma ACCA.Kila nchi huwa na chombo chake,hata sisi tungeweza kuwa na strong CPA kama tungekuwa professional enough.

  Tatizo la ACCA unaweza kujisomea nyumbani bila hata kufanya kazi.Waingereza wazawa wana CA,hasa graduates.UK wanathamini CA,kidogo CIMA.Wazungu wanajua kabisa ACCA ni yawakuja,hawana experience ya kazi.

  CPA ya marekani ni bora,kwa sababu hawaiuzi kama ACCA,utafanya mitihani ukiwa state tu.Kwa hiyo ACCA ni money making machine kwa sasa,kama vilevile vyuo mediocre ambavyo vinafanya ubia na vyuo vingine kutoa MBA kama za Wales etc.

  Kwa hiyo Mzumbe ni mediocre waliyonayo ,sio deal sana kupata exemption.Huhitaji degree kumaliza ACCA,lakini you need degree kumaliza engineering au medicine!!!!
   
 11. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #11
  Jan 26, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 655
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 18

  Mmakonde mwambie huyu jamaa hajui anenalo
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,597
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 38
  Asante mkuu kwa ufafanuzi! oooooooooh Mzumbe oooooo Mzumbe ooooooooooo Mzumbe! Umeelewa wewe Muanzisha thread
   
 13. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #13
  Jan 26, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,455
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 48
  Lakini kwa swala la waalimu hutegemeana na lecturer mwenyewe, wapo wenye sifa za chini katika vyuo vingine lakini wanafundisha vizuri, na wengine wana Phds lakini wakikufundisha wanakuacha na viporo kibao. Pia kama ilivyo kwa kila mtu darasani kuwa na uwanja wake kimasomo, kila chuo/taasisi huwa na eneo lake la kutanua kutokana na sifa na umakini wa waliokabidhiwa maenoe hayo. Hivyo mimi bado naamini kuwa pamoja na MU kutoridhisha katika maeneo fulanifulani, pia huenda kuna fani zinazofaa kuchukua pale. Japo ni kweli kabisa kuwa kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza, hivyo uonapo taasisi zinazojitangaza sana, uwe makini maana huenda wako dhaifu.
   
 14. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #14
  Jan 26, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,119
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 38

  daaah we jamaa ni waukweli kinoma, hawa jamaa wa mzumbe feki sana sio kwenye fani ya accounting tu hata sheria, IT yani wengi ni feki sana... mimi nina mdogo wangu ambae alipata div 3 lakini alipenda sana accounting so aliamua kwenda BAF mzumbe kupitia private sponsorship scheme...dogo alikua anafumua kupita kiasi akaja siku moja akaniambia hivi bro inakuaje wale ninao wakubali kama wewe wa udsm hamfanyi mambo kama ninayofanya mzumbe??? nikamwambia kumbe umekua eeeh.......dogo final gpa alipiga 4.6 na anakwambia hakua mwenyewe almost half of the class walipiga first class....wakati mlimani first class hawakuzidi 15 kati ya wanafunzi 600...lakini ukienda kwenye ajira au proffesional certification kama cpa ndo utajua ufeki wao, kama mnabisha nendeni pale mlimani kwa watu wanaopiga school of law...utaona wanaoongoza kwa stress ni kina nani...wakitoka mzumbe kwa ufeki wanafwata tumaini univ....

  mlimani kitabaki kuwa chuo kikuu cha ukweli forever, ukicheki udom ambacho ni kipya ndo utaishiwa nguvu kabisa, yani watu waliopata EEE(flat E) wamekua enrolled, haya niambie mnategemea kupata watu wa namna gani??? je taifa linajengwa au linabomolewa??? ukienda mlimani hawaangalii ufaulu/ufeli wa wanafunzi kwa mwaka husika, wenyewe wanastic kwenye cutting points tu...kuna kipindi wanafunzi wa science walifaulu kuwazidi wale wa arts, sasa watu wengi wakaaply law wakitegemea watapata kutokana na ile hali ya kutofanya vizuri kitaifa...u know what happened?? kitivo cha sheria kili-enroll wale tu waliofit cutting points zao(div 1.3-1.6) only....

  udsm is the best huwezi kulinganisha na mzumbe hata kidogo....hapo hujazungumzia engineering kwenye fani yangu....
   
 15. m

  madule JF-Expert Member

  #15
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kupata Division one au two form six sio kigezo cha kwamba utafanya vizuri chuo kikuu, hapo tunakosea saana maana ukiangalia hilo utagundua nyingi sio za halali, tumeona watu wameingia chio na divisonIII ya form six na wakamaliza na first class chuo kikuu, na kudhihirisha kuwa sio ya kubabaisha na sasa wapo nchi za watu ambako tunaamini kiwango chao cha elimu ni zaidi yetu na wanafanya vyema pia!! hivo kuingia uDSM na hiyo cut point kama kigezo ni kujidanya kama wahusika wanjiona wao wana kiwango bora kuliko wengine. Kwa ujumla style ya kuchanganua nani anafaa kuingia chuao kikuu na criteria zipi zizingatiwe mbali ya hiyo cut point inabidi kuangaliwa upya au laa system ya mitihani ikarabatiwe ili mitihani iwe fair kwa wote na hiyo cut pint itakuwa na maana. Vinginevo mtaendelea kujisifu tuuu Ooooooh UDSm ndio chuo pekeee, wakati huenda ww mwenyewe haijakupeleka kokote.
   
 16. A

  Amwanga JF-Expert Member

  #16
  Jan 26, 2010
  Joined: Jan 11, 2009
  Messages: 295
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 18
  Udsm is the best but ina decline kwa kasi mbaya kwa sababu nyingi sana
  1. Kuongezeka kwa wadesaji
  2. walimu wenye ubinafsi na roho mbaya
  3. Walimu kuweka ligi na wanafunzi
  4. Walimu na nadhani wanao bakishwa sasa hivi kwa vigezo za GPA si competent as they where supposed
  5. Wana claim wanatoa wanataaluma watakao fanya tafiti mbalimbali but it is not real, kwani graduate wengi hata jinsi tu ya kuanza research hawajui, just to make literature survey hawajui, this is a big problem and is killing. Kwa hiyo unapo mlinganisha gratuate wa udsm na mzube au other related colleges ataonekana yupoyupo tu kwa sababu something is miss, MU wao tangu mwanzoni wanaandaliwa kinadharia na vitendo, so kwa kua tatizo la kitaaluma linatafuna vyuo vyote yeye ana advantage kuwa na skill so whe adsorbed to the industry ataonekana anajua kazi kuliko wa udsm.

  Mimi bwana ni Engineer from FOE, lazima tuwe wakweli tuache ushabiki, vyuo vyote lazima vibadilike otherwise tunakwisha, nashukuru na exposure kidogo na vyuo vya NORDIC, naona jinsi wanavyowaanda vijana wao, usije ukashangaa mzungu Diploma aka deliver kuliko B.Sc wetu simply because wanajua wanaandaa nn.

  Let we stop kujisifiasifia kwa vijimambo vidogo tukaacha kuwa wawazi. Walimu wengi sasa vyuoni wanabakizwa walikua wadesaji, what do you expect?

  Mbaya zaidi, GPA inalenga ulivyokua unakokotoa regardless ulikua unakariri au la, GPA is good creteria but I dont think kama hamna usimamizi thabiti inafaa kutumika. Of cause kuwa na Div. za NECTA nayo is challenge, kwa sababu carricula ya NECTA si researchable is relying on how someone think.
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Jan 26, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,822
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  falesy Member
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  Join Date: Wed Mar 2006
  Posts: 46
  Thanks: 7
   
 18. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #18
  Jan 26, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 3,360
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 48
  Duh! ZionTz na manazi wengine wa Mlimani (UDSM) taratibu basi.

  Ubora wa Mlimani ni upi hasa? Kulindwa na wanasiasa? Ubora hupimwa kwenye matokeo. Na matokeo ninayoongelea hapa ni utendaji wa graduates kazini. Mh! Hapo mbona kazi kubwa.

  BTW: Huko Ulaya kuna ranking ya ubora wa MBA. Kikubwa walichoangalia ni idadi ya wahitimu kupata ajira haraka na mshahara mnono.
   
 19. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #19
  Jan 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 968
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 18

  Kumbe na wewe wa Mzumbe! Duh! Mimi yangu mimacho tu.
   
 20. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #20
  Jan 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri kuangalia idadi ya graduates waliopata ajira haraka napo sio kigezo kizuri sana. Mfano Mzumbe tokea zamani walikua wanapenda sana kuenroll privately sponsored students then wanafuata wale waliokosa nafasi UDSM na SUA(Division 3 au two za mwishomwisho). Sasa hawa wanaojisomesha wengi wao ndio wale wenye maGod father(usikatae) na usijeshangaa hata mwenye performance nzuri darasani huko Mzumbe anaweza akakosa job na kilaza fulani toka MU hiyohiyo akapata kazi ya kufa mtu(Know who)kabla hata ya graduation mjini hapa. Kwahiyo kigezo cha nani kaanza kupata ajira haraka zaidi ondoa kabisa bongo hii,unless unaenda kufanya hiyo survey PWC,KPMG,Ernst&Young, lakini sehem nyingi zilizobaki hasa kwenye mashirika yetu mazuri hapa mjini utaanzisha skandali upya bure na uchaguzi huu!!!!!!
   

Share This Page