Mzozo wa abiria na askari baada ya madereva wa magari Iringa kusimamishwa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
ABIRIA wanaosafiri kuelekea mikoa ya kusini na nchi za kusini mwa Tanzania jana wamefanya vurugu kubwa katika eneo la ukaguzi wa magari (Check Pint ) Igumbilo mjini Iringa ikiwa ni pamoja na kuifunga kwa muda barabara kuu ya Tanzania, Zambia na Msumbiji (TANZAM ) na kuwapiga madereva wakorofi kama njia ya kupinga hatua ya askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani hapa kuwakamata madereva sita wa mabasi waliyokuwa wamepanda.

Tukio lilo ambalo lilidumu kwa zaidi ya masaa manne na kupelekea jeshi la polisi kuingilia kati kumaliza utata huo kwa kuwapa dhamana madereva hao, lilitokea majira ya saa 8 mchana baada ya madereva wa mabasi hayo kuendesha bila kinyume na sheria ya sumatra.

Wakizungumza kwa niaba ya abiria wenzao kuhusiana na tukio hilo abiria Chriss Kashillila , Cleva Mlungu na Salima Mwakasyela walisema kuwa wanashangazwa na hatua ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuwakamata madereva wa mabasi hayo zaidi ya sita kwa madai ya kufika mapema zaidi eneo hilo pamoja na kuendeshwa na dereva mmoja wakati toka walikotoka jijini Dar es Salaam na kupita mikoa zaidi ya miwili askari wa usalama barabara wamewaacha wapite bila kuzuiwa...
 
Back
Top Bottom