Mzindakaya naye akiunga mkono Chadema

Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Chrisant Mzindakaya amekitaka chama cha Mapinduzi CCM kujibu hoja za Chadema kwa kuwatumia viongozi wa mikoa ambayo Chadema wanafanya mikutano badala ya kumsubiri Waziri Mkuu au rais kujibu hoja.

"Viongozi wa CCM katika mikoa ambayo Chadema wanapita na kutoa hoja zao, wajibu kwa kuponda hoja hizo ili wananchi waelewe hali halisi na siyo kumsubiri Waziri Mkuu au Rais kujibu hoja," alisema Mzindakaya.

Amehoji iweje Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kuwa kimya muda wote kama iko likizo na kuiachia Serikali kazi ya kisiasa hasa katika kipindi hiki?

Source: HabariLeo
Kwanza nawaonea huruma ccm.
Wana mzigo wa kukisafisha chama kutokana na mavuvuzela kama Makamba Sr.
Pili wana kazi ya kujibu hoja toka kwa chadema
Wana kazi ya kujisafisha mbele ya watazania utokana na yale wanayoshutumiwa
Wana kazi ya kutekeleza ahadi lukuki walizoahidi 2005-2010

n.k, n.k, n.k..............................................

Mwacheni JK akonde......
 
Hana jipya Mzindakaya!After all heading sio reflection ya contents!Kwanza gazeti lenyewe habari leo!Nahisi kuna mpango wa kuwaweka juu baadhi ya wanaccm kwa kujifanya wanatoa matamko yaliyo against na chama ili kuipa nguvu propaganda ya CCM NI SAFI ILA WACHACHE WANAIHARIBU!Ukweli utabaki palepale CCM haina tena uwezo wa kiuongozi.
 
Ni mawazo gani ya hovyo aliyoongea Mzindakaya.

Alichoongea Mzindakaya ni jambo la kawaida kukieleza chama chake, na wala huwezi kuliingiza hilo kwenye vitendo vya kishujaa, mawazo ya hovyo ni mchangiaji kuhusisha kauri hiyo na ushujaa, labda funguweni kamusi mpate tafsiri ya neno shujaa. naomba rudi upya uisome vizuri thread.
 
Majibu ya CCM ukijifanya much know utakosa kazi, yanaenda kwa utaratibu kwa sababu kuna don't-mention nyingi sana. Unaweza kujibu ukajikuta umemgusa JK au Pinda mwenyewe hapo utaitwa utoe maelezo ndo maana watu woooote na wabunge woooote wa ccm wamekuwa waoga kuongea. CDM kinakubalika na hakuna wanachoweza kufanya kukizuia i swear !

Vp zile cheche za Tendwa zmezmwa na nin? Au zlikuwa za makaratas? Mshtuen nyie mnaoweza kumshtua ili ainue kichwa chake tumumalize! Si mzindakaya tu ata Tendwa mwnyw anatukubal, useme anaogopa kusema najiuzulu, ndo tatzo la mkwere na wenzake, vingnevyo tungekuwa tunapanga jns ya kuanzisha mirad juu ya uchmbaj wa madin yenu na s kuwaachia hao ma uncle zake na mkwere!
 
how can a president tell you something in the audience and when you see him he smiles at you like a little baby? Head of State? Please !!!!...Tanzania (by Lisa M Rockefeller)
 
Sio lazima mtu akutukane mpumbavu ndio ujue umetukanwa Mzee ametumia hekima na busara kuwataka ccm waamke na kujibu hoja za msingi na sio kuendelea kupandikiza chuki kwa wananchi kuwa chadema wanataka kuvuruga amani kitu ambacho sio kweli.
 
Ninapata shida na kichwa cha habari! Labda nakosea ni wapi ameunga mkono CHADEMA?

Labda ana maana ameisaidia CDM kwa vile CCM hawataki kusikia challenges kama hizi. Ngoja tusubiri tena 31 March, Mkwere aje kutulalamikia tena kama kawaida yake.
 
hivi kuna kiongozi gani wa ccm mwenye uwezo wa kujibu hoja za chadema? akili zao ni za mgando, hoja ya maana kwao cdm wanataka kupindua serikali kama rais anatoa sababu kama hiyo je makamba atasema nini? hali ya leo ya mtanzania ni mbaya sana hilo kwao hawalioni
 
Hata CCM walio wengi si mafisadi kwa hiyo wanapigika na mgao wa umeme na gharama za umeme kuwa juu na bei ya bidhaa mbalimbali kupanda hovyo ndio maana hawataki unafiki wa kutetea upuuzi wa mafisadi na uzembe wa viongozi walioshidwa kucontrol bei na uchumi

Ndugu yangu, Sofia Simba alisema CCM hakuna msafi, kwahiyo wote ni mafisadi, ndio maana wanashindwa kujibu hoja za chadema, huku mtaani kwetu mbolea za ruzuku zimechakachuliwa sana, wasimamizi walikuwa ni wenyeviti wa serikali za mitaa na wengi wao ni ccm.
 
Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Chrisant Mzindakaya amekitaka chama cha Mapinduzi CCM kujibu hoja za Chadema kwa kuwatumia viongozi wa mikoa ambayo Chadema wanafanya mikutano badala ya kumsubiri Waziri Mkuu au rais kujibu hoja.

“Viongozi wa CCM katika mikoa ambayo Chadema wanapita na kutoa hoja zao, wajibu kwa kuponda hoja hizo ili wananchi waelewe hali halisi na siyo kumsubiri Waziri Mkuu au Rais kujibu hoja,” alisema Mzindakaya.

Amehoji iweje Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kuwa kimya muda wote kama iko likizo na kuiachia Serikali kazi ya kisiasa hasa katika kipindi hiki?

Source: HabariLeo

Si kwamba cdm ni hovyo kwa kila jambo!!! Na si kwamba ukiwa ccm uko sahihi na upinge kila jambo kwa cdm
 
Mwanasiasa mkongwe na kada wa CCM, Chrisant Mzindakaya amekitaka chama cha Mapinduzi CCM kujibu hoja za Chadema kwa kuwatumia viongozi wa mikoa ambayo Chadema wanafanya mikutano badala ya kumsubiri Waziri Mkuu au rais kujibu hoja.

“Viongozi wa CCM katika mikoa ambayo Chadema wanapita na kutoa hoja zao, wajibu kwa kuponda hoja hizo ili wananchi waelewe hali halisi na siyo kumsubiri Waziri Mkuu au Rais kujibu hoja,” alisema Mzindakaya.

Amehoji iweje Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) kuwa kimya muda wote kama iko likizo na kuiachia Serikali kazi ya kisiasa hasa katika kipindi hiki?

Source: HabariLeo
Hoja za CDM huwezi kuziping kirahisi. Zinza ukweli unaoonekana, zina mantiki na zinatolewa kwa umahiri na umakini wa hali ya juu. Nani anaweza kuwaeleza wananchi kuwa sasa maisha ya Mtanzania ni bora kuliko miaka nane iliyopita kabla ya utawala wa JK? Ndo maana hawa viongozi wanapata kigugumizi kuzijibu!
 
Hayo maneno hawezi yasema tena maana mtoto wake kazawadiwa ukuu wa wilaya
 
Ninapata shida na kichwa cha habari! Labda nakosea ni wapi ameunga mkono CHADEMA?

Alitaka kuuza habari kwa mgongo wa CHADEMA.Eti waponde hoja???UKWELI UNAPONDEKA AU WATAKIWA KUJIBIWA KWA MAJIBU SAHIHI BILA KUPUNGUA HEKMA,UTU,BUSARA NA WELEDI WA MATENDO KWA WENYE DHAMANA?Hilo pia ni adhimu kulipata katika ngazi hizo aotazo.,Huko ni wingi wa fitna,majungu na kujipendekeza kwa wakubwa kwa tumaini la kubebana.Usiwashangae sana washa-colapse kitambo,hawajui tena waandike nini na vipi,wanatamka hata wasiyoyajua na kuyaamin,kwa ulaghai au bila ya kujua.
 
Majibu ya CCM ukijifanya much know utakosa kazi, yanaenda kwa utaratibu kwa sababu kuna don't-mention nyingi sana. Unaweza kujibu ukajikuta umemgusa JK au Pinda mwenyewe hapo utaitwa utoe maelezo ndo maana watu woooote na wabunge woooote wa ccm wamekuwa waoga kuongea. CDM kinakubalika na hakuna wanachoweza kufanya kukizuia i swear !

sio kuhojiwa tu.unawezaza ukaishia kupoteza maisha ukaacha vitegemezi vyako kuwa watoto wa mitaani.watanzania hawajamsahau kolimba.tumeishia kusema ndio mzee.matokeoyake chama kimekufa kabisa.tunategemea polisi,usalama wa taifa,mahakama kupumua.
 
Back
Top Bottom