mzimu wa Nyerere ndani ya mwanamke Mtwara

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
ktk jamii zote duniani tunaamini uwepo wa mizimu na madhara yake iwapo mzimu huo utakuwa na ujumbe wa kutoa na usisikilizwe. ndipo, kwa dalili zinazojitokeza wahusika huenda kwa wajuzi wakajuzwa nini kifanyike ili kuepukana na majanga yanayoikuta jamii husika. Basi mwaka jana nilisoma ktk gazeti kuwa kuna mama mmoja huko kusini mwa Tanzania anateseka na mzimu wa Mwl. Nyerere na alikuwa na ujumbe kwa Rais wetu kutoka kwa Hayati Baba wa Taifa letu. Kwa tabia ya viongozi wetu kujifanya mambo hayo hawajui huku kukicha wanayafanya naweza amini kabisa kuwa mama huyu maskini hajaweza kusikilizwa. Ushauri; wahusika hakikisheni mama huyu anakutana na rais, rais si Mungu hata aogopwe, kwanza ni mpenda watu tumeona kule Iringa amekaa chini akiongea na mama mwenye ulemavu. Huenda matatizo ya nchi hii yakapungua kama huyo mama akisikilizwa. kisha rais awaite viongozi wa dini kama Laizer, shehe mkuu, Pengo, viongozi wa waasia(inangawa hawakukumbukwa ktk kumuapisha rais) na kiongozi wa wapagani na butiama awepo kiongozi wao, asiwepo Malasusa.Kisha wa 'discuss' jambo hilo kiimani ambalo huyo mama atamwambia rais. Ikumbukwe Mwl. alikuwa na nia kuona kusini mwa Tz kunaendelea kuliko. Asanteni.
 
hata mi nakumbuka.! Ila yule mama si wa Mtwara bali kwao ni Songea mtaa wa Ruvuma chini. Alikuwa anahojiwa na Msigwa (TBC) na ndiye aliyeyaweka chini ya kapeti kwani yale maono yalikuwa na ujumbe mzito sana kwa SISEMI.
 
duh, ni wazo zuri, lakini kidogo ungetudokeza huyu mama kafanya nini, au katoa maneno gani mpaka useme ni mzimu wa Mwalimu Nyerere?? Je alikuwa anasema katokewa na Nyerere?au ni kipi muhimu mpaka aonane na Rais??na huko mtwara yupo pande zipi,??Mtwara mjini?vijijini?masasi au pande zipi..uwe specific kidogo
 
hata mi nakumbuka.! Ila yule mama si wa Mtwara bali kwao ni Songea mtaa wa Ruvuma chini. Alikuwa anahojiwa na Msigwa (TBC) na ndiye aliyeyaweka chini ya kapeti kwani yale maono yalikuwa na ujumbe mzito sana kwa SISEMI.
 
samahani sana Mtwara na Songea siku zote hunichanganya. kumbe ni songea. Mizimu, majini, malaika , vyote ni pepo (spirits). dharau zenu hizo ndo leo zinawafanya kupanga foreni kule Loliondo. Naamini JF ina lengo zuri la kuelimishana na kupeana ufumbuzi si mahali pa kujibu/kufanya upuuzi. Huyu mama alichonacho hatakisema ila tu mbele ya rais. Mdharau mwiba... Tujiulize inakuwaje nchi za E.A & central hazina matatizo kama haya tuliyo nayo wakati hapa tuna kila kitu plus waombeaji wa kimataifa wenye uwezo wa kuamuru (si kuomba) mvua nayo ikanyeesha! Mwl. alikuwa ni baba yetu, kama ndivyo yeye kurudi na kumtumia dada yetu kumfikishia mkuu wa ukoo wetu (rais) ujumbe kuna ubaya? kwa ufupi mama huyu anaujumbe kwa rais wetu toka kwa mzimu wa hayati Mwl. Nyerere.
 
I have two contributions: kwa nini mtoa mada kadai rais amusikilize huyo mama kisha aite viongozi wa dini ila asiwepo malasusa?, hivi huyu raisi wenu anayapenda/tekeleza maono ya nyerere?!
 
I have two contributions: kwa nini mtoa mada kadai rais amusikilize huyo mama kisha aite viongozi wa dini ila asiwepo malasusa?, hivi huyu raisi wenu anayapenda/tekeleza maono ya nyerere?!

1. Kikwete hates Nyerere big deal!!!
2. Is it suggested ... we depend and work on those type of informations ...from that woman????? for something objective???
 
ktk jamii zote duniani tunaamini uwepo wa mizimu na madhara yake iwapo mzimu huo utakuwa na ujumbe wa kutoa na usisikilizwe. ndipo, kwa dalili zinazojitokeza wahusika huenda kwa wajuzi wakajuzwa nini kifanyike ili kuepukana na majanga yanayoikuta jamii husika. Basi mwaka jana nilisoma ktk gazeti kuwa kuna mama mmoja huko kusini mwa Tanzania anateseka na mzimu wa Mwl. Nyerere na alikuwa na ujumbe kwa Rais wetu kutoka kwa Hayati Baba wa Taifa letu. Kwa tabia ya viongozi wetu kujifanya mambo hayo hawajui huku kukicha wanayafanya naweza amini kabisa kuwa mama huyu maskini hajaweza kusikilizwa. Ushauri; wahusika hakikisheni mama huyu anakutana na rais, rais si Mungu hata aogopwe, kwanza ni mpenda watu tumeona kule Iringa amekaa chini akiongea na mama mwenye ulemavu. Huenda matatizo ya nchi hii yakapungua kama huyo mama akisikilizwa. kisha rais awaite viongozi wa dini kama Laizer, shehe mkuu, Pengo, viongozi wa waasia(inangawa hawakukumbukwa ktk kumuapisha rais) na kiongozi wa wapagani na butiama awepo kiongozi wao, asiwepo Malasusa.Kisha wa 'discuss' jambo hilo kiimani ambalo huyo mama atamwambia rais. Ikumbukwe Mwl. alikuwa na nia kuona kusini mwa Tz kunaendelea kuliko. Asanteni.

Imani yangu inakataza kusikiliza mizimu hivyo kiongozi wangu hatahusika.

Itashangaza kama Srikali itaanza kuskiliza ndoto za kila mtu na mizimu yake!
siafiki hili hata kidogo
 
Watu wako nyuma sana enzi za early stone age. Munaamini mizimu sio? Nyerere ni kafiri tu hana lolote. Na si baba wa taifa lkn ni baba wa wakristo.
 
Be careful- hizi ni propaganda za kipagani za vatikani na Jesuits. Wanatafuta basis za kumwita Nyerere Saint. Usidanganyike, simple.. "Muhubiri 9:5 watu waliokufa hawajui neno lolote, hawana ijara tena." Shetani amekuwa akijitokeza ktka sura za watu waliokufa zamani na kueneza uongo wake kwamba...hautakufa hakika ila utafanana na Mungu, Mwanzo 3.

Usidanganyike, ukisikia Mariamu katokea wapi cjui, Nyerere kamtokea nani cjui, ni majini katika sura za watu. Kimbia, Mtu akifa hakuna cha Mzuka wala nini hizo ni propaganda za kishetani Wakristo mnabeba tu!!
 
Unajua 2kianza kuamini mambo hayo hii nchi itaelekea kubaya, mambo ya mizimu,maono ni mambo ya kiimani kwa hiyo asikilizwe kiimani na km kikwete anataka kumsikiliza amsikilize akiwa amevaa kofia ya iman na c ya rais hii nchi aiendeshwi na mizimu wala maono
 
Askofu Malasusa bado ni kijana mdogo ku-handle jambo hili. Labda mzee wake. Kwanini viongozi wazee? kwa sababu wazee wetu ktk vikao na rais wetu wote hutoka Dar, na kukutanishwa pale Karimjee kisha kuelezwa na rais badala ya wao kujadiliana na rais. ktk biblia kuna wafu wa aina nyingi kama Samwel, Mifupa ya Elisha, na kadhalika. piga ua kama ujumbe upo, upo tu dawa ni kuusikiliza. mara ngapi wosia usiofatwa huleta shida za maisha.
 
ndugu zangu mbona mmekuwa wasomi kuliko hata wasomi wenyewe. Mzimu (spirit) mnasema ni mambo ya stone ages. Kila leo tunakimbilia nchi za kizungu kutafuta pesa huko (si maisha), mnadhani walisoma tu wakapata? kwa taarifa zetu wao uheshimu sana mizimu, someni historia ya wakuu wa Rome Italy kisha jiulizeni kwa nini rais Obama anatumia mzimu wa hayati Lincolin. Karagabao...
 
Back
Top Bottom