MZIMU WA LOLIONDO! ni kweli au?

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,458
Nilipokuwa kijana, nilisikia watu wakisema (kipindi kile cha utawala wa mwinyi) kuwa mwinyi ameuza mbuga ya LOLIONDO. hadi leo hii sielewi kama ni kweli au la. kuna miaka ya hivi karibuni, hapa jf mtu aliweka picha za waarabu wengi wanafanya pikiniki kule loliondo na kuifanya kama ile loliondo ni mbuga yao, bila shaka yule alikuwa mtoto wa mfalme wa saudi kama sikosei...naombeni mwenye ufafanuzi kamili aniambie, hivi ukweli ni upi kuhusu Loliondo, na wale waliofika pale, ni mbuga au ni pori la hifadhi tu, na je, ni kweli mwinyi aliuza kwa watu binafsi ile mbuga au alibinafsisha au alifanya nini, na je, wale waarabu wanaokujaga kufanya pikiniki kule ndo hao walionunua au ni wengine..

NB; by specifying race here, sina maana ya kuwanyanyapaa wawekezaji wasitoke uarabuni, tz tunahitaji uwekezaji toka dunia nzima hata zimbabwe kama wanaweza...nataka kujua ukweli tu. asante.
 
Hata mimi nisikia hicho kitu umenikumbusha mbali sana.
 
Utafanyaje ndugu yangu NCHI IKISHAGEUZWA SHAMBA LA BIBI!
Mkijadili sana mtaambiwa ni UDINI.
Mwandishi mmoja alikufa akifuatilia hilo. Alikuwa mwandishi wa gazeti la MFANYAKAZI na alithibitishwa LOLIONDO ILIUZWA. Ninamkumbuka kwa jina moja tu "KATABALO"
 
kama iliuzwa, mbona haliwekwi wazi tujue, na wale wananchi wanapambana kila wakati, wananchi wanaoonekana ni kero huko loliondo waliuzwa pia? wasijekuwa nao waliuzwa pamoja na shamba/mbuga...hahaha.
 
haa! Wakuu ndio mmejua leo? Mbona warabu washapewa miaka mingi mbuga hiyo?wanasafirisha panya, mijusi na wanyama mbalimbali huko kwao, wameanzisha zoo na pia wanapata pesa nyingi ktk utalii kupitia wanyama waliotuibia. Jamani inauma sana, na jinsi warabu walivyo washenzi na dharau, ni mbaguzi na siwapendi weupe wote.wanaendelea kutunyonya.
 
Habari zenu Ndugu!

Loliondo....Ninavyojua mimi ni kwamba hiyo nafasi wameuziwa waarabu kwa muda wa miaka kadha..wazungu wanasema LEASE...inaweza ikawa ya miaka 10, 20 na hata 99. Nilivyosikia mie ni kwanba ni lease ya miaka 99. Tatizo hapa ni kwamba hawa Waarabu wana mkataba kabisa ulio sainiwa na Kisheria wako kwenye eneo lao mpaka muda wa lease hiyo utakapo kwisha...ni kama wewe umenunua eneo ukajenga halafu ukazungushia uzio ili watu wasipite...sema tatizo ni kwamba Serikali yetu haituambii ukweli wa hili jambo...kama wameuza, ni kwa kiasi gani na hizo hela ziko wapi? zimetumika wapi? na kama waliahidi kutupatia msaada fulani in exchange for that land tuambiwe na huo msaada tunaliopaitwa uko wapi tujue..

Lakini kitu kinachoniudhi ni kwamba inasemekana hawa watu wanasafirisha wanyama nje ya nchi kunyume cha Sheria..Kama ni kweli mbona Serikali haijachukua hatua zozote?? Kwanini hao watu wanaruhusiwa kuwa kiwanja chao binafsi cha ndege na Wageni wao wanaingia moja kwa moja bila ya kupita uhamiaji au kupitia Viwanja vyetu vya ndege??

Na wewe Bruse Lee mbona unakuwa mshamba hivyo? Watu weupe wanatunyonya nini? Ni sisi ndio tunaojiuza kwao..kitu kikiwepo sokoni watu watanunua lakini kama hakipo watu watakuwa hawana time nacho....na Bruce Lee mwenyewe alikuwa Mweupe...tujadili kuhusu hili suala hapa na sio kuleta chuki binafsi...
 
Mh hata miye juzi niliambiwa kitu hichohicho.je wanamiliki loliondo nzima au?nimesikia mpaka wana kaairport kao huko
 
Huu mzimu unaendelea mpaka leo. Sijui hatma yake ni nini!
damu ya mtu haipotei bure.
Hapo Marahemu Stan Katabalo wa gazeti la Mfanyakazi alipoteza uhai wake, kisa kulipoti kwa undani kilichokuwa kikiendelea na wakati huo uelewa wa wananchi wa kawaida walijua serikali haiwezi kuwasaliti kamwe.
Miaka kama 20 baadae mzimu wake bado unasumbua 'wabaya' wake na ukweli utajulikana tu mwishowe.

shit , sasa wakuu naomba hili swala tulivalie njuga litangazwe kwa masocial network yooote watu wajue kelele ziongezeke.
 
kama iliuzwa, mbona haliwekwi wazi tujue, na wale wananchi wanapambana kila wakati, wananchi wanaoonekana ni kero huko loliondo waliuzwa pia? wasijekuwa nao waliuzwa pamoja na shamba/mbuga...hahaha.
Waliuzwa kwa sababu watalii wakija wanafurahi kuwaangalia na wao kama viumbe wanaoishi mbugani.
 
Back
Top Bottom