Mzee Yusufu: Wake Zangu Marufuku Kutumia Instagram

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145
218e8__MZEE-YUSUPH-1.jpg


Udaku News

WAKATI wanawake duniani kote leo wakiadhimisha siku ya wanawake duniani, wake wa mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu, Mzee Yusufu, Leila Rashid na Chiku wamekatazwa kutumia tena mtandao wa Instagram.

Wanawake hao wamekatazwa kutumia mtandao huo na endapo watatumia kwa siri mume wao huyo amewaeleza kwamba ndiyo itakuwa talaka yao.

Mzee Yusufu amechukua uamuzi huo baada ya hivi karibuni kuzuka kwa majibizano ya wake zake hao kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo Whatsap na Instagram.

Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi cha taarabu kinachorushwa na Redio Clouds, Mzee Yusufu, alisema mtandao huo ndio chanzo kikubwa cha kukuza mgogoro huo.

“Nimewatoa wake zangu wote kwenye mtandao huu ambao ndio nimeona umekuza sana mgogoro huu na mimi pia nipo njiani kutoka katika akaunti hiyo ili ibaki kwa ajili ya kazi tu na endapo nitagundua yeyote ana simu ya siri ambayo anaitumia kuingia kwenye mtandao huo ndiyo itakuwa talaka yake.

“Hivi tunavyozungumza wake zangu wote hawana akaunti za Instagram, zinazoendelea kusambaza maneno ni majina feki na ndiyo nimeshaamua hivyo,” alisema.
 
Back
Top Bottom