Mzee Wassira shule yako dawa tosha!

Ukiacha ubishi usiokuwa na mashiko na ubishi wa jadi, Mzee Wassira leo bungeni umetoa shule yenye mashiko! Hongera sana! Umedhihirisha ng'ombe hazeeki maini na kuwa utu uzima dawa!! Hoja za mlinganisho wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano na bajeti ya serikali ya mwaka 2012/2013. Hoja za mahusiano ya bajeti na Ilani ya uchaguzi ya CCM. Hakika umetoa shule ya kutosha, asiyetaka acha asitake milele lakini shule umetoa!!
Ambao hawakumwangalia Wassira soon ntaweka mkanda wa speech yake! Lakini mnaotaka kutukana pia mnakaribishwa maana mko wengi, nitukaneni mimi lakini msimuhusishe mwingine....

Utimize hayo maneno siyo longolongo...Uweke huo mkanda wa hiyo speech..
 
Habari za leo wana JF wanamapinduzi, wana wa Tanzania wazalendo na wapenda nchi. Najua wengi wetu hapa tunaipenda Tanzania yetu na tunatamani kuiona inashamiri kiuchumi, demokrasia na kijamii. Uongozi wetu unaonyesha kushindwa kukidhi mahaitaji ya nchi kwa miaka mingi sasa. Bajeti zetu mwaka hadi mwaka zinakuwa hazionyeshi mwanga kwani ukiafanyia analysis bajeti za miaka kumi iliyopita za Tanzania hutaona mabadiliko yeyote makubwa ya vyanzo vya fedha na matumizi zaidi ya kumfanya mtanzania masikini.

Wapo wanaoona ile bajeti nzuri na wanasababu zao inawezekana wao inawanufaisha kwa kupata vitenda, posho, ruzuku, shangingi, kuiba, na safari za kila asubuhi kwenda kutalii nje zanchi. Tusisahau matibabu ya hali ya juu na kulipiwa nyumba na ahadi za kusaidiwa kushinda uchaguzi kwa kutumia fedha za wizi. Kwa matumizi hayo ya ghiliba ni lazima waone bajeti imetulia kwani wao mwananchi kazi yake ni kupiga kura na kama atakuwa hataki watampa kanga, tshirt, ama vielfu viwili kwani wana fedha zetu ili wapewe kura waondoke waende dodoma wakaseme imepita kwa 100% .

Inasikitisha hao wanaoikubali kesho yake wanaanza kulia na foleni, maji hakuna, umeme kukatika, ajira za vijana wetu, madini kutotusaidia, uwekezaji dunu kana kwamba walikuwa misukule Dodoma.

Wito NAOMBA TUSIMTUKANE NAPE WALA TUSIMBEZE TUMSIKILIZE TUJADILIANE NAYE KWA HOJA INAWEZA TUSAIDIA KUJUA HIVI WENZETU WANAFIKIRI NINI. Tusimpe nafasi ya kukimbia majadiliano yenye tija atujibu nini mawazo yao inabidi tuwashinde kwa hoja ama wao watushinde kwa hoja. ningependa Nape aweke mkanda wa Wassira the ambaye kwa sasa ndiye anaonekana roho ya CCM na mchumi namba moja ndani ya mjengo mwenye uwezo mkubwa ndani ya CCM. Ingawaje hii inamshtua kila mmoja ila hiyo ndio CCM. Kama wasira ndio mwenye akili ya uchumi na mwenye majibu kwa matatizo ya kiuchumi ya TZ na watanzania hayamkini jibu wote tunalo jahazi la uchumi chini ya rubani CCM linazama kwa kasi kubwa sana.

Nape nasubiri mkanda tuchambue hoja naomba mwacheni atetee kwa hoja nasi tujibu kwa hoja akikimbia tutajua, Nape sio Mzalendo na mwungwana.
 
Ukiacha ubishi usiokuwa na mashiko na ubishi wa jadi, Mzee Wassira leo bungeni umetoa shule yenye mashiko! Hongera sana! Umedhihirisha ng'ombe hazeeki maini na kuwa utu uzima dawa!! Hoja za mlinganisho wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano na bajeti ya serikali ya mwaka 2012/2013. Hoja za mahusiano ya bajeti na Ilani ya uchaguzi ya CCM. Hakika umetoa shule ya kutosha, asiyetaka acha asitake milele lakini shule umetoa!!

Ambao hawakumwangalia Wassira soon ntaweka mkanda wa speech yake! Lakini mnaotaka kutukana pia mnakaribishwa maana mko wengi, nitukaneni mimi lakini msimuhusishe mwingine....

Mtu yeyote makini anayemjua Wassira akisoma hayo maneno hapo juu, badala ya kuendelea kumshangaa Wassira, atalazimika kumshangaa yule ambaye anaweza kuwa hata na mawazo ya kumnukuu Wassira! Du, kweli kuna roho na roho, kuna courage na courage.

Binafsi nililazimika kumsikiliza Wassira kama ambavyo nalazimika kumsikiliza mtu yeyote hata kama sikubaliani naye au anatoa maoni nisiyopendezwa nayo, ili kujua anajua kiasi gani na anafikiria nini na kwa kiwango gani na vingine vingi. Kwa mtu makini aliyemsikiliza yule mzee aliyejichokea kifikra...Wassira added no value, to wrap up! Kama ilivyo siku zote, kama ilivyo kwa magamba wengi. Pole kwa wale walioona hata anaweza kuwa quoted.

Lakini hapo kwenye rangi ya bluu, mto hoja ameonesha UDHAIFU mkubwa. Haya.
 
Nnauye Jr ninacho kijua mimi siku zote CCM hawana maneno mabaya au ahadi mbaya, sera na mipango yao siku zote ni nzuri mfano mzuri ahadi kipindi cha kampeni 2010

tatizo linalo waua ni matendo ambayo hayaendani na mnacho kisema chama kimejaa mafisadi a.k.a magamba naanyi mpo sijui labda ni miongoni mwao

narudia tena sera zenu na mawazo yenu yanaridhisha nimemsikia waziri wa noti kaeleza vizuri utadhani siyo CCM tunao wajua siku zote
 
Kama kweli huyu aliyeandika hii thread ni Nape Mnauye basi ana matatizo, siku zote CCM wana mipango na maneno mazuri na ndiyo maana wananchi walikuwa wana wahamini tatizo ni kuwa matendo hakuna. Watu wamesubiri ahadi hazitekelezeki, sasa hata kama wasira akiongea vizuri huku mimi sina maji safi, sina barabara, huduma za afya mbovu, shule mbovu ambazo kila siku walimu wako kwenye migoma, umeme wa mashaka hayo maneno mazuri kwa miaka hamsini ndiyo mimi nitakuwa nimetimiziwa shida zangu kadanganye wajinga GAMBA wewe.
 
Napeeee! Mbumbumbu kweli. Hakuna sehemu nyingine ambako unaweza kuweka mawazo yako ambako watasoma mbumbumbu na Watumwa wa akili za wakubwa na wazembe wa kufikiri na kuchanganua mambo.

Akiri za nape bwana weka wehu hùu kwenye redio uhuru au gazeti la uhuru au kaongee na maline hasan malini asubui. Humu unajishushia hesima. Sijaona wazo ata moja linalokusapoti utumbo na ma_i tu.
 
Nape amesahau kuwa kuna nyakati mawaziri walisambaa mikoani kueleza uzuri wa bajeti wakapopolewa mawe.
Kwa mtu kama Nape ni ngumu sana kuelewa machungu ya wananchi.

Nape ni mtoto wa Nnauye na hajawahi kuonja adha ya kushinda na njaa, kutembea km 27 ukitafuta matibabu na kukuta hakuna dawa, hajui adha ya kupanga chumba kimoja baba mama na watoto na wala ahjui uzito wa ndoo ya manji achilia mbali mafuta ya taa na kibatali

Hakuna bajeti mbaya kwake kwa miaka aliyoishi duniani sasa hii ya leo itakuwaje mbaya?
Huyu ndiye anajinasibu bingwa wa kutetea wananchi na kiongozi dhidi ya ufisadi, asichokijua ni kuwa hakuna ufisadi mkubwa kupita ule wa kuwalaghai wananchi.

Nape, ni generation inayopigiwa upatu kuongoza nchi! Ni kijana. Umewaangusha vijana

Kuna wakati ni vema mtu akikaa kimya kwasababu anaweza kuongea ukatuondolea mashaka tuliyokuwa nayo juu yako
 
kama ukatibu uenezi ni huu chama linadondoka nape we subiri lowasa achukue chama uone utakavyotoa povu kwa elimu,ushawishi,umaarufu,hekima,busara pesa na elimu hymuwezi lowasa sasa utajuwa lowasa ni nani pole sana kikwete kakulengesha nenepa sana kipindi hiki utanyea bakuli 2015
 
Napeeeeh! Gamba kijana!! Nikupe taarifa tu,unapotaja wasira unatutia kichefuchefu,kwa mambo, tabia na matendo yake.
 
KUNAKUFAA ZAIDI FB MAANA KULE NDO WAPATIKANAPO MANDEZI WAKO SABURI MKUBWA WEEEE
c42e7879-0596-c950.jpg
c42e7879-05b0-5011.jpg
 
Kwenye mikutano yao wanagawa ubwabwa, naomba 2015 ije hata kesho, Nape utahama nchi wewe.

Nnauye nakufananisha nna msemaji mkuu wa Ghadafi unakumbuka alivyokuwa analopoka mbele za watu??now hajulikani alipo, so kuwa makini na wewe
 
Ukiona watu walipewa majukumbu ya kuongoza nchi wanishia kuwa wanaongea mambo ya kishabiki kama watu wa kijiweni basi ujue nchi wanayoongoza ina matatizo makubwa sana, tena ya kutisha.

Mwalimu Kichuguu,

Sijui kama unamkumbuka Mzee JJ Kamotho wa chama cha KANU enzi za Daniel Arap Moi..............!

Yule Mzee alikuwa shabiki hivi hivi lakini Upinzani ulipoingia madarakani mwaka 2002 mzee wa watu alipiga sharp U-turn.Sasa yule ni mzee nilitarajia afanye vile

Kaka yangu Nape una safari ndefu kisiasa.Wakati Mwingine Epuka mamabo yatakayokupunguzi political mileage ukiwa kijana.Hao wenzako wako kwenye political menopouse.Wao wakimaliza hii project yao waliyokufanya meneja mradi na msemaji watastaaafu na hata kukimbilia exile.

Jaribu kupata ushauri hata kwa wazee wenye heshima na wastaarabu ndani ya chama chenu kama akina Mzee Salim Ahmed Salim.Vuka hata mstari pata Ushauri kwa wakongwe Akina Augustine Mrema,Lipumba,Dr.Slaa n.k. Maudhui ya post na trend yako kisiasa siyo healthy kwako na hata kwa chama chako kinachomaliza ngwe yake ya mwisho.Kuwa makini sana hasa kipindi hiki cha Transition.Siasa za ushabiki uliovuka mpaka na kushabikia matendo yanayofanywa na wabunge wenu na mawaziri(tena kwa mtindo wa makundi) hayataliacha Taifa hili salama huko tuendako na wewe hautasalimika.Labda uwe na kipaji kama cha Tariq Aziz au The late Michaael kijana Wamalwa (Former VP) wa Kenya na chama chake cha FORD-Kenya
 
Wassira yupi huyo?? Huyu huyu au mwingine? Kama huyu huyu lini kaanza kuongea point?
Mzee Wasira huyu aliyewahi kunyooshwa ki sawa sawa na mzee Warioba kwa rushwa ya uchaguzi akapigwa ban ya miaka 5. Aikuja akaokotwa jalalani na wanamtandao ambao walimuinua na kumfikisha hapo alipo sasa.
 
Ukiacha ubishi usiokuwa na mashiko na ubishi wa jadi, Mzee Wassira leo bungeni umetoa shule yenye mashiko! Hongera sana! Umedhihirisha ng'ombe hazeeki maini na kuwa utu uzima dawa!! Hoja za mlinganisho wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano na bajeti ya serikali ya mwaka 2012/2013.

Hoja za mahusiano ya bajeti na Ilani ya uchaguzi ya CCM. Hakika umetoa shule ya kutosha, asiyetaka acha asitake milele lakini shule umetoa!!

Ambao hawakumwangalia Wassira soon ntaweka mkanda wa speech yake! Lakini mnaotaka kutukana pia mnakaribishwa maana mko wengi, nitukaneni mimi lakini msimuhusishe mwingine....

kila siku kila mwaka wanatoa Shule nzuri but sasa ni more than 50 years matunda ya Shule nzuri hizo hatuyaoni Nape sa hii cjui inakuwa ina maana gani maybe next time wafanye mbaya inaeza kutukomboa.
 
Back
Top Bottom