Mzee wangu ananichanganya

Mzee wangu simuelewi kabisaaaaa. Mwaka wa 4 huu amekuwa akinisisitiza nitafute mwanamke mwenye sifa zifuatazo :-
- Awe na elimu isiyopungua form six, na kama ana six awe na mpango wa kusoma zaid ya hapo
- Asiwe mzungu, mhindi wala mchina
- Awe anaingiza kipato kama kazi au biashara
- Asiwe "mtoto wa mjini"
Na mbaya zaidi atataka amu-interview kama ana uwezo wa kujieleza, kabla hajaamua kumkubali. Ninacho shangaa, hajawahi kunieleza kama mapenzi ni muhimu au sio muhimu. Na kali zaidi mke wake mwenyewe (maza) kaishia la 7. Naona kama kuna mbinu za kunitafutia mke hivi . . . .

Mkuu baba kuna mambo amejifunza katika maisha yake. Hilo la mama kuishia la 7 inawezeka ndio maana anakuambia umchague mwenye elimu ilimsaidia kwenye maisha.
Huyo ni baba yako naamini anataka kukupa samaki wala siyo joka.
Una bahati ya kuelekezwa na baba, Hebu kaa naye chini akupe busara zake nawe umshirikishe mawazo na matamanio yako.

Zungumzeni kwa hisa ya TZ.
 
Kwanza kuna kitu waswahili wamesema "msema pweke hakosi"

Hivi unaamini kuwa baba yake kamwambia ende akamu interview? Naamini hakuambiwa hivyo.

Usikute kaambiwa "mlete tumuone mapema, tuzungumze nae, tuone kama tunaelewana kwa kuwa ndoa si ya wawili tu kwa mila ya kwetu"

Naona kuna watu hawajanielewa, au hawaniamin kwa vile haijawahi kuwakuta. Pengine mnadhan wazazi wote wako sawa kifikra. MZEE KANIAMBIA LIVE UMLETE HAPA HUYO BINTI NA NITAMUULIZA UMESOMA HADI WAPI NA UMESOMEA NINI. Na mbaya zaidi mzee anajitapa kwamba anajua kila kitu, so hata kama kasomea udaktari au uandishi wa habari (wakat yeye ni engineer) atamgundua tu. Sasa hiyo ndo sawa na kusema MLETE NIMUONE??
 
Sasa hiyo ndo kumu interview?

Na unaposema anajitapa hivi, anajitapa wapi?

Kaka mbona unaonekana kaa husikilizani na baba yako au kuna cha ziada tusichokijua?
 
Msema pweke hakosi ina maana anaehadithia kitu peke yake huwa hawezi kujuulikana kama kakosea kwa kuwa hakuna hadithi kutoka upande wapili.
Yeye kamchora baba yake hivyo na sisi tunaamini kwa kuwa ni msema pweke ndo hakosei :(

Soma maoni ya watu uone alivyomtukanisha kwa kuwa tu yeye mwenyewe hakuonyesha kumuheshimu.

Siwezi kukubali matusi kwa mzee wangu, pamoja na yote hayo. Na siwez kuleta hoja za kumsingizia mzazi aliyenilea mpaka sasa naweza andika hapa JF. Ni dhambi isiyosameheka kwa Mungu. Lakin pamoja na ulinzi huo kuna vitu wazazi huongea pasipo kuangalia mazingira ya halisi. Isitoshe aliniambia unatakiwa uifahamu vizuri familia na ukoo wa mwanamke, isije kuwa wana matatizo ya kufa-kufa ovyo, au hawajaelimika sawasawa, au wana maradhi ya kurithi. Ni mambo ambayo ni vigumu sana kuyajua haraka kama kuyatamka. Itachukua muda sana. Na si rahisi wakat mwingine. Ni wazo zuri lakin kuna ugumu wa utekelezaji
 
Sasa hiyo ndo kumu interview?

Na unaposema anajitapa hivi, anajitapa wapi?

Kaka mbona unaonekana kaa husikilizani na baba yako au kuna cha ziada tusichokijua?

Pengine nimetumia lugha mbaya kusema KUJITAPA. Anyway sikulenga humchafua, nililenga kumaanisha anasema anajua kila kitu, wakati uhalisia hauruhusu binadam kudai anajua everything
 
we Jaba sasa mbona kama unamdhihaki baba yako mwenyewe na sie unategemea tumfanye nini?

Ebo!! Utasemaje mzazi wako anajitapa?
U sound like u r nt in good terms with your father!
 
Kwani ulishaona wapi baba mkwe analazimika kujua elimu ya mchumba wa mtoto wake kabla ya kukubaliwa? Kwanini asiulize cha msingi ambacho ni upendo wa kweli??? Elimu itanisaidia nini kama mwanamke hana upendo??
 
Nadhani I have to apologize for using the word KUJITAPA coz maana yake imeshapelekwa isipo. Nimerekebisha. Rudi ktk mada.
 
hakuna mzazi asiyependa mazuri kwa mwanae...inawezekana baba yako hataki ufanye makosa aliyopitia..kumsaili mtu ni kumjua kama anafaa kuwa na wewe au hapana....ila honest mie ningempotezea baba yako,ningehakikisha namletea mkwe na mimba juu...kwi kwii
 
muombe muda na ukae nae chini muombe akueleze kwa nini ana masharti hayo. ni mzee wako muheshimu lazima ana nia nzuri. na pia ataweza labdakukueleza experience yake na mama yako. ila usikasirike.
 
Kwani ulishaona wapi baba mkwe analazimika kujua elimu ya mchumba wa mtoto wake kabla ya kukubaliwa? Kwanini asiulize cha msingi ambacho ni upendo wa kweli??? Elimu itanisaidia nini kama mwanamke hana upendo??

Sikiliza mkuu, wewe si wa kwanza mwenye baba 'mgumu'

Tatizo ni namna unavyoelezea na maneno unayotumia.

Hoja yako ulivyoiwasilisha imewapa watu chance ya kusema watakavyo.

Nafikiri ungesema tu watu wakupe ushauri wa kudeal na baba wa namna yako na sio kuwapa watu chance ya kusema anamtaka mkeo

Tubadilishe lugha tunapozungumzia wazee wetu
 
hakuna mzazi asiyependa mazuri kwa mwanae...inawezekana baba yako hataki ufanye makosa aliyopitia..kumsaili mtu ni kumjua kama anafaa kuwa na wewe au hapana....ila honest mie ningempotezea baba yako,ningehakikisha namletea mkwe na mimba juu...kwi kwii
Roselyne hahaaaaaaaa....
Nasubiri komenti ya klorokwin tu hapa basi.

Jaba umeeleweka! Sasa kama wewe una vigezo vyako basi jichagulie, naamini hata wewe hutakuwa mbali sana na mshua wako lakini vigezo vya mchumba huwezi pangiwa na mtu maana mwisho wa siku wewe ndo utaishi na mkeo.
Unajua upendacho, kwa hiyo si kila ushauri lazia ufuate.
 
Pole jaba. Mzee wako anakupenda na anakutakia mema. Ameshaona madhaifu ya mama yako ambae ameishia la saba.
Lakini suala la interview tena jamani!!
Zungumza nae muelewane.
 
Katika uliyoambiwa fata unaloweza usiloweza puuza tu wala msitafutane maneno.

Naamini hata ukipata aso vigezo vyote hivyo, baba atasusa, mwisho atajirudi tu.

Usiumize kichwa kwa jambo hilo
 
Pole jaba. Mzee wako anakupenda na anakutakia mema. Ameshaona madhaifu ya mama yako ambae ameishia la saba.
Lakini suala la interview tena jamani!!
Zungumza nae muelewane.

Gaijin lakini asuse kivipi? Huyo baba atakuwa na lake jambo basi!
 
Gaijin lakini asuse kivipi? Huyo baba atakuwa na lake jambo basi!

Wazee wa style hiyo wapo. Madhali vigezo vyake havikufatwa ataona kadharauliwa na atasusa lakini mwisho wa siku ataelewa kuwa uchaguzi wa mke wa mwanawe si wake na I hope atajirudi
 
Wazee wa style hiyo wapo. Madhali vigezo vyake havikufatwa ataona kadharauliwa na atasusa lakini mwisho wa siku ataelewa kuwa uchaguzi wa mke wa mwanawe si wake na I hope atajirudi

Sasa hapo kama na yeye alichaguliwa wake basi.

Na hivi najiuliza huko kuwa injinia/mtaaluma ndo kuwa mke/muke mkamilifu? Mbona ndoa nyingi za wasomi zina suasua .....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom