Mzee wa Upako atoa amri mvua kunyesha nchini na imenyesha

Kwa nini Kamati ya Nishati isimfuate ili aamuru mvua inyeshe maeneo yanayozunguka Mtera ili kuondoa tatizo la umeme?
 
Tumuogopeni na tumpe mwenyezi Mungu nafasi yake. Leo binadamu eti anauwezo wa kuamrisha mvua inyeshe, kesho atakuja na ipi? Ya Rab tusamehe na utunusuru!
 
jamani sasa hivi tunamatatizo makubwa zaidi ya hayo bibilia inasema mungu huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki na kwawakati wake ata eliya aliomba mvua isinye juu ya nchi kwa 3na nusu mpaka kwa neno lake tena so akuna jipya na jua limewai kusimamishwa so akuna muujiza mpya ata petro alitembea juu ya maji mpaka alipotia mashaka akaanza kuzama so tunaoomba watumishi wa mungu waliopo tz kama kinalusekelo wasimame kwa neno la bwana kwamba mafisadi wote wanaowaibia watanzania kwa kila aina ya wizi kwa epa, dowans, mikataba mibovu,wizi waa kura nk, wafe kwa jina la yesu ndio inawezekana yamefanyika mungu mwenyewe alikuwa akiwaamuru mfalme sauli na mfalme daudi
 
sikilizen jamani mzee wa upako mkubali msikubali n noma !!
kama kweli uko makini utaona kabisa jamaa hata anavoongea kwenye luninga n mtu wa kujiamini na anayofanya , kwa ufup habahatishi mambo yake!

mtumien ktk mambo yenu ya kiroho na kimwili mtasaidikika
 
Ulikuwa 'guest' lakini ukiangalia mahubiri!!" lol...
nawewe acha ushamba na mawazo ya kizamani hii ni karne nyingine ya kufunguka ubongo na kuelewa mambo kwa mapana wenyewe wanasema u must view things in 3dimension, sikiliza ndugu kwenda gest si lazima ufanye yale unayoyafikiria - mtu anaweza kwenda gest kama nyumba ya kupumzikia wageni. upo hapo man!

HATA WEWE SIKU MOJAMOJA UKIONA NYUMBANI PANAKUZINGUA WE NENDA GEST KATULIZE KICHWA KWA MSONGO WA MAWAZO OK?
 
MCHULUSEKELOGPL.jpg

Juzi nilikuwa guest fulani naangalia tv....nikavutiwa na mzee wa upako Antony Lusekelo akifanya mahojiano na chanel 10...alisema aliamuru katika mikoa baadhi akaitaja Singida,Dar nk mvua inyeshe tarehe 9....

...akasema sasa hivi Dar mawingu yameshaanza kutanda....na kweli nasikia Dar mvua imenyesha juzi 10/feb 2011...pia alisema kwa anaebisha ajitokeze kama yeye kwenye TV na ataamuru ukame utokee...kasema ana uwezo huo...

Mzee wa Upako ni asset kubwa kwa Watanzania....tumtumieni wakuu...
watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Samahani mkuu hivi kumbe manabii wanatakiwa wawe makada wa vyama vya upinzani?

NABII hana itikadi ya chama cha siasa. Itikadi yake ni matakwa ya Mwenyezi Mungu. Sikumbuki kumsikia akikemea mafisadi na uporaji wa raslimali za taifa.

Hili la mvua Aaaaaagh sanaa tupu kama Nigeria vile! Au ndiyo maana mvua ilileta maafa siku hiyo?. RIP Prof. Kamuzora. Hata Edo angetuletea mvua tu kama angepewa nafasi.
 
nawewe acha ushamba na mawazo ya kizamani hii ni karne nyingine ya kufunguka ubongo na kuelewa mambo kwa mapana wenyewe wanasema u must view things in 3dimension, sikiliza ndugu kwenda gest si lazima ufanye yale unayoyafikiria - mtu anaweza kwenda gest kama nyumba ya kupumzikia wageni. upo hapo man!
HATA WEWE SIKU MOJAMOJA UKIONA NYUMBANI PANAKUZINGUA WE NENDA GEST KATULIZE KICHWA KWA MSONGO WA MAWAZO OK?

Msamehe bure tu hapo ndiyo utaona akili yake ilikolala. Hata hana haja na thread
 
Imeandikwa, Kwa hiyo akawaita wanafunzi wake kumi na wawili na kuwapa mamlaka juu ya roho wachafu, ili wawafukuze na kuponya kila namna ya ugonjwa na kila namna ya udhaifu.

Hivyo mzee wa upako anayo mamlaka!
 
danganya toto tu hizo hakuna lolote, mwizi wa mawazo ya watu tu. Mbona hakuyaona mabomu ya mbagala na gongo la mboto akaambia mapema waumini wake.

Hawa siku hizi ni kama waganga ya kienyeji, toka lini kanisa likatangazwa kwa gharama za juu na watu kufatwa na magari vituoni, biashara hiyo.

hawa ndo manabii wa uongo waliotabiriwa toka enzi. Wanachofanya ni kushindana kwa miujiza feki kutafuta wateja, pole kwa wafuasi wao, wengine mnawachangia wanunue HUMMER nyie kwa ngondi na kusukumizana kwenye daladala, kweli WAJINGA NDO WALIWAO.
 
Pia alisema kwa anaebisha ajitokeze kama yeye kwenye TV na ataamuru ukame utokee...kasema ana uwezo huo...

Sasa huyu anataka sifa au anataka kutafuta wafuasi kwa njia za ujanjaujanja, sasa anataka ligi na nani?
kuna manabii kama yesu walifufua hadi wafu lakini hawakujisifu wala kujikweza.

Mi nadhani huyu mzee wa upako yupo kimaslahi zaidi.
 
Back
Top Bottom