Mzee wa Upako ampinga Prof. Shivji suala la Muswada Katiba Mpya

Nimesikia mzee wa Upako akikemea siasa za Chuki ndani ya CCM wakati yeye alijitangaza kuwa Kampeni manaja wa Jk 2010.Hata hivyo yeye Mzee wa Upako anachuki kubwa na Askof Mwasata katibu mkuu PCT.Askof Mwasota ndiye aliye mchukua mzee wa Upako Mby baada ya maombi ya mama yake .Mwasota alimfundisha Mzee wa upako kozi ya Uchungaji na kufungua tawi la Kibangu.Baada ya kupata sadaka nyingi Mch.Lusekelo akampindua Askof Mwasota na kujiita Mzee wa upako na kusajili upya.Hadi leo Mzee wa Upako haelewani na Askof Mwasota.Mwaka 2010 Mzee Upako akiwa kampenia Jk alifanya njama na kumuweka ndani Askof Mwasota kwa kisingizio kuwa amemuibia Tsh20m, Kwa kutuma majambazi.RPC alituma watu wake na kufanya uchunguzi ikabainika kuwa ni chuki
Za kidini na Madaraka yalitokana yalitokana

duh ni kweli ndugu yangu hayo!? basi tuendako ni kubaya kuliko tutokako
 
Nimesikia mzee wa Upako akikemea siasa za Chuki ndani ya CCM wakati yeye alijitangaza kuwa Kampeni manaja wa Jk 2010.Hata hivyo yeye Mzee wa Upako anachuki kubwa na Askof Mwasata katibu mkuu PCT.Askof Mwasota ndiye aliye mchukua mzee wa Upako Mby baada ya maombi ya mama yake .Mwasota alimfundisha Mzee wa upako kozi ya Uchungaji na kufungua tawi la Kibangu.Baada ya kupata sadaka nyingi Mch.Lusekelo akampindua Askof Mwasota na kujiita Mzee wa upako na kusajili upya.Hadi leo Mzee wa Upako haelewani na Askof Mwasota.Mwaka 2010 Mzee Upako akiwa kampenia Jk alifanya njama na kumuweka ndani Askof Mwasota kwa kisingizio kuwa amemuibia Tsh20m, Kwa kutuma majambazi.RPC alituma watu wake na kufanya uchunguzi ikabainika kuwa ni chuki
Za kidini na Madaraka yalitokana yalitokana

Hii Post ni kitambo kweli, lakini kama ambavyo literrature haiozi, as well IMENIFUMBUA MACHO!
Bwana aturehemu
 
Mzee wa Upako siyo credible source. Hana uwezo wa kuchambua maoni ya Prof. Shivji. Mtu mwenyewe ni darasa la saba ataweza kuchambua katiba. Anarukia tu kama wachimba mchanga wanavyorukia gari la mchanga!
Mzee wa Upako aka Mch Antony Lusekelo amesema kwa kuwa Rais Kikwete amesha saini mswaada wa katiba mpya kinachotakiwa sasa ni kuaminiana tu hakuna haja ya kuupinga!.Amewataka wananch na wadau mbalimbali kujitokeza na kuunga mkono Mswaada huo kwa kuchangia mawazo.Amesema Katiba iliyopo sasa haina makosa mengi ya kurekebisha! Source :gzt Mwananch leo
 
Acha chuki ndugu yangu Shivji ni profesa aliyebobea katika masuala ya sheria na ikiwamo mambo ya katiba. Kwa hiyo mchango wake ni muhimu sana katika taifa letu. Ni magamba aka mabwepande pekee yao kwa sababu ya kuwa mbumbumbu hawajui umuhimu wa michango ya Prof. Shivji.
kelele zote za shivj anataka awe miongoni mwa wajumbe wa tume ndiyo maana kila cku anakosoa. Sasa hz kelele zake aziendeleze tuu huko nje tuzichambue maana na cc tunaona mapungufu katika mapendekezo yake na mawazo yake ni ya kwake binafsi asiseme anawasemea watanzania wote.
 
lusekelo anaropoka sana ukimsikiliza kama una akili timamu utajua hata uchungaji wake una walakini maan mtumishi wa mungu wa kweli mungu humpa busara na hekima hata katika maongezi utayaona haya lusekelo msanii tu
 
prof shivji anajua anchosema hata hivyo katika elimu yake ameegemea katika swala zima la katiba kisheria.hivyo tutumie vizuri ujuzi wake hakurupuki
 
lusekelo aliwambia waumini wake nini nyie msiogope freemasons ni kikundi tu cha wafanya biashara huko marekani.
huyu ndio lusekelo
 
Mzee wa upako, iwapo ni kweli, ashauriwe badala ya kuwa mtetezi wa magamba, kwa nini asichukue form zao za uongozi? Mwisho kuchukua fomu ni kesho, jumamosi, aache kulazimisha agenda za kisiasa kwa kofia ya dini. Achukue fomu magamba, watu wamuelewe.
 
Mkuu nakubaliana nawe kabisa.

Lusekelo ameonesha kuwa ni mtu wa chuki, hasira na kisasi. Vilevile ni muongo, mroho wa pesa na Tapeli kwa waumini wake. Hivi vyote viko kinyume na UPAKO!

He is not clean at all, na amejileta mwenyewe kwenye darubini achambuliwe.


Rejeeni makala hii:


1 Oktoba 2011

TUKIO la hivi karibuni la kuvamiwa kwa Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Utashinda, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako (pichani) na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi limechukuwa sura mpya baada ya watumishi wawili wa Mungu kuhojiwa.

Waliohojiwa katika tuhuma hizo nzito za kuvamiwa kwa Mzee wa Upako na kuibiwa mamilioni ya shilingi ni Askofu David Mwasota na Mchungaji Frank Chacha ambao wanatoa huduma kwenye kanisa la Naioth Gospel Assembly lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam.

Vyanzo vyetu vya habari vilidai kwamba Mchungaji David Mwasota alikamatwa na polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa 6 katika Kituo cha Mbezi jijini Dar es Salaam kuhusiana na tukio hilo na kutakiwa kumfikisha katika kituo hicho Mchungaji wake Frank Chacha.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, inadaiwa kuwa mara baada ya Askofu Mwasota kumfikisha kituoni hapo, Mchungaji Chacha alihojiwa kwa siku mbili mfululizo bila kupata dhamana kwa madai kwamba kama angeachiwa haraka angevuruga upelelezi wa polisi.


�Baada ya Askofu Mwasota kumfikisha Chacha kituoni hapo, Mchungaji huyo alishikiliwa kwa muda wa siku mbili akihojiwa,� kimoja cha chanzo chetu ambacho tunakihifadhi jina lake kilisema.

Iliendelea kudaiwa kwamba Mzee wa Upako alihisi kuwa Mchungaji Chacha alihusika na tukio hilo kutokana na ujumbe mfupi wa maneno (SMS) aliomtumia, hivyo akaamua kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

Inadaiwa kwamba ujumbe uliotumwa kwenda kwa Mzee wa Upako ulikuwa ni wa kumpa pole kuhusiana na tukio la kuvamiwa na majambazi kisha kuporwa mamilioni ya pesa usiku wa kuamkia Septemba 27, mwaka huu.

Hata hivyo, vyanzo hivyo vilisema kwamba ujumbe aliotumiwa Lusekelo haukuwa na nia mbaya ila aliutilia mashaka kwa kuwa ulimuuliza kama alimkosea Mungu kutokana na kukumbwa na balaa hilo.

�Hilo la kuambiwa kwamba amemkosea Mungu ndilo lililomfanya mtumishi huyo kuona kama vile alikuwa akifanyiwa dhihaka katika tukio hilo la kuibiwa pesa,� kilidai chanzo chetu.

Inadaiwa kuwa Mzee wa Upako alishindwa kuelewa maana ya ujumbe huo na kuhisi kufanyiwa dhihaka na mtumishi mwenzake Chacha ambaye hakuwa na lengo baya.

Aidha, chanzo hicho kilisema kwamba hii ni mara ya pili kwa Mzee wa Upako kumtuhumu Mchungaji Chacha ambaye zamani alikuwa anatoa huduma katika kanisa lake kabla ya kutokea hali ya kutoelewana ambapo alihamia kwa mlezi wake Askofu Mwasota.

�Inawezekana ana bifu na Mchungaji Chacha kutokana na kuondoka katika huduma yake ndiyo maana ameamua kufanya hivyo, ni jambo la kusikitisha watumishi kupelekana polisi na haya siyo maadili ya kitumishi kabisa,� kiliendelea kusema chanzo hicho.

Kwa upande wa Askofu Mwasota alisema kwamba baada ya kutoka kituoni kesho yake (Jumanne) alimfuata Mchungaji Chacha na kumpeleka Kituo cha Polisi Mbezi ambapo alikaa kwa muda wa siku mbili ndipo alimtoa kwa dhamana.

�Mzee wa Upako ni mwanangu na sijagombana naye na sina matatizo naye, ila sijui kwa yeye na Mchungaji Chacha wana matatizo gani kwa sababu walikuwa watu wa karibu, nitaongea naye vizuri nijue tofauti zao,� alisema Askofu Mwasota.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alipopigiwa simu siku ya Jumapili kuzungumzia sakata hilo alisema bado analifuatilia na tulipomtafuta kabla ya gazeti hili kuingia mitamboni simu zake zote hazikupatikana.
Mzee wa upako na chuki kwa Ask Mwasota
 
Back
Top Bottom