Mzee wa Upako ampinga Prof. Shivji suala la Muswada Katiba Mpya

My hairs! Hivi amewahi kuisoma katiba huyu mchungaji! Hawa ndio wale wanaenjoy mazingira wanayoandaliwa na waumini na fedha za sadaka, wanachojua wao ni kuwa nchi hii ni ya maziwa na asali![/QU Nimeona jambo jipya na la ajabu Duniani! Mtu wa darasa la saba kumpinga mtaluma wa ngazi ya prof!
 
lusekelo ni nani? yule anayetaka sadaka ktk tv kwa njia ya m.pesa? hv ana uelewa gani juu ya maswala ya katiba?
...ukiona hivyo ujue "K.i.w.e.te" ameisha mdumbukizia 50m kwenye hiyo account yake ya m-pesa,sasa unategemea kusikia nini kutoka kwa huyo mganga njaa aka muuza neno zaidi ya kumfuraisha mlipia zumari!?...
 
Heri na nyie viongozi wa dini mseme, maana sisi wengine tukisema tunaambiwa ni magamba. Hiki alichokisema mzee wa upako ni sahihi kabisa na ninamuunga mkono.

pamoja na katiba iliyo kuwa mbaya, inaruhu uhuru wa kutoa maoni .Tunaheshimu maoni yake, lakini hayo si maoni ya watanzania wote, ni lini alisomea uchambuzi na kuwa na ufahamu wa mambo ya katiba na siasa?aache kujipendekeza kwa magamba

 
Professor Shivji kachemsha. Ampelekee ujamaa wake mjamaa mwenzake, falsafa zake zimepitwa na wakati.
hakuongelea ujamaa alikuwa anaongelea misingi ya kupata katiba bora --- mwanzo mbovu huzaa katiba kimeo - tunaandika katiba ya miaka zaidi ya 50 ijayo - hapa hatuandiki ILANI ya uchaguzi ya CCM kwa miaka mitano ndugu zangu. nawakubusha tu msiotaka kubadilika ki mtazamo.
 
My hairs!
Hivi amewahi kuisoma katiba huyu mchungaji!
Hawa ndio wale wanaenjoy mazingira wanayoandaliwa na waumini na fedha za sadaka, wanachojua wao ni kuwa nchi hii ni ya maziwa na asali!

kukurupuka kubaya sana tena sana, ebu fikiria, jamaa anasimama anaongea mamneno kama hayo kwa lugha rahisi kama hiyo na kwa muda mfupi kama huo bila ufafanuzi wowote alafu unampinga mtu mweredi na mjuzi wa mambo ya sheria kirahisi namna hiyo bila kuwa na data zenye mashiko alafu waandishi wa habari wanaexagulate mambo kwa namna hii hatutafika, shivji was right na alilaani sheria inayomzuia mtu yoyote kuelimisha juu ya katiba isipokuwa tume na ukiangalia kwa makini unajiuuiliza hiyo tume iko wapi ina ukubwa gani kuwafikia watanzania alafu eti ukienda kinyume na hili ni kifungo miaka 3-7 au faini 5m to 15m au vyote kwa pamoja na bado watu waashadadia ujinga na upumbavu wa wanasheria uchwara kama werema, huu ni ujinga usio na kifani! kutengua maamuzi si kosa na si jambo geni kwani unaowaongoza ni watanzania sasa ukitengua kwa ajili ya watanzania kuna tatizo gani?

SHIVJI ALIENDA MBALI HADI AKASEMA WANAMSHAURI RAISI WANAKOSEA HATA NINGEKUWA NI MIMI HUO MSWADA NISINGEUSAINI KWANI HAUNA TIJA KWA WATANZANIA, NA RAIS ANA MAKOSA MAKUBWA, KIKATI ANAOWAJIB WA KUSHAURIWA ILA HAKUNA KIFUNGU KINACHOMBANA KUKUBALI USHAURI WA MTU KA ALISOMA NA AKAONA NI POA AKASAIBNI BASI UWEZO WAKE WA KUONA MABO SIO MZURI LAZIMA TUKUBALIANE KATIKA HILO!LUSEKELO HANA UBAVU WA KUBISHANA NA MTU KAMA SHIVJI HATA MBINGU ISHUKE.

WATANZANIA TUMEUZWA NA BADO ETI BUNGE LAKATIBA LIWE NA WAJUMBE 600?KWA NCHI KAMA YA TANZANIA KWELI NA JE KUNA VIGEZO GANI VINATUMIKA KUWAPATA?HUU NI UJINGA NA WABUBGE WA SSM WATALAANIWA HADI WAFE KWA KUWANAJISI WATANZANIA KUPISHA UJINGA KAMA HUU! UMEJADILIWA WAPI HADI USOMWE MARA YA PILI HALI YA KWANZA TU ULIKATALIWA NA KUCHANWA NA WANACHI NA NDIPO SERIKALI IKAAMUA KUURUDISHA ILI ULETETWE UPYA? NANI KATULOGA WATANZANIA,
 
Katika mahubili yake siku moja alisema Jairo ni muumini wake na alimpa fedha zilizotumika kujengea madirisha katika kanisa lake hivyo sioni kama ataweza kemea ufisadi sanasana atajikomba ili apewe fedha zaidi na hao mafisadi ambao ni rafiki zake na JK
 
Huo ni mtazamo wake kwa kiwango cha uelewa wake, kumjadili humu ni kumpa umaarufu kama alioupata kanisani kwake. Nadhani humu jamvini hastahili hicho. Kujadili ukosoaji wa Lusekelo dhidi ya Profesa Shivji ni kumdhalilisha profesa.
 
Kuna kijana alikua anataka kuurithi ufalme wa mungu akamfata yesu akamwambia,"bwana yesu nifanyaje niurithi ufalme wa mungu?" Yesu akamjibu fuata amri zote za mungu na mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe,yule kijana akamwambia yote nilishayafanya tangia mdogo,basi naye yesu akamjibu "uza mali zako zote uwagawie masikini". Swali langu hivi Mch.Anthony Lusekelo ndo yule anayetembelea HUMMER na kuna kipindi aliingiliwa na majambazi wakampora million 20 ndo yeye huyo au mwingine?
 
[h=2]Gazeti majira

27 December 2011[/h] [h=3]Jairo hana kosa, ni majungutupu-Mchungaji [/h]
Na Anneth Kagenda

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Ubungo Dar es Saama, Mchungaji Antoni Lusekelo, ameibuka na kusema kuwa sakata la Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo, na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, ni majungu na haina tatizo.

Bw. Jairo anadaiwa kuchangisha fedha za umma kwa ajili ya kugharamikia kupitisha bajeti ya wizara hiyo kinyume cha utaratibu huku Bw. Luhanjo akidaiwa kumjingia kifua.

Mchungaji Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako amesisitiza kuwa wapo viongozi wengi waliofanya kitendo sawa na ya Bw. Jairo lakini hayajulikani hivyo kutaka Watanzania kuacha tabia ya kuchafuana.

Akizungunza na waandishi wa habari Kanisani kwake jana, Mchungaji Lusekelo alisema haiwezekani mtu mmoja kupanga kuchangisha fedha za wizara bila kuwa na mtandao na viongozi wengine na kudai kuwa kilichotokea ni siri kuvuja na si vinginevyo.

"Ninachojua ni kwamba wezi wote wako mahakamani, unapoona mtu analalamikiwa kila siku wala hakamatwi ujue ni majungu tu na mambo hayo hafanyi, angefanya angekuwa selo

Ikumbukwe kwamba kuharibiana na kuchafuana kupo, mfano mimi niliwahi kuambiwa kwamba nimeenda nchini Nigeria kutafuta nguvu za giza wakati sijawai hata kuwaza kufanya kitendo cha namna hiyo,"alisema Mchungaji Lusekelo.

Aliendelea "Lazima tukiri kwamba watu wanachafuana na ndio maana ninasema hata kwa Bw. Jairo ni siri tu ilivuja na hawezi kufanya peke yake," alisisitiza.

Kuhusu maadili ya uongozi alisema anasikitishwa na kutoweka kwa desturi ya viongozi wa zamani ambao walilala na kuamka wakiwa na mawazo ya nini kifanyike tofauti na ilivyo sasa.

"Nchi imekuwa Imara, Amani na utulivu kutokana na watu fulani viongozi wa kwanza walikuwa wakiwaza na kujua kwamba kesho waamke na lipi lakini maisha ya sasa yanachangamoto nyingi na hii inatokana na uhuru wa utandawazi ambao unakuwa zaidi

"Lakini pia utandawazi huu usisababishe viongozi kujisahau na kudhani kwamba mwisho wa dunia ni 2015, bado kuna miaka mingine mingi na pia mawaziri na wabunge wasipende kujilimbikizia mali na kuwasahau wananchi wake," alisema Mchungaji Lusekelo.

Akizungumzia janga la mafuriko ya hivi karibuni alisema viongozi ndio watuhumiwa wa kwanza na kwamba wakati wananchi wanajenga mabondeni wanawaona na kuwanyamazia.

"Mvua ilikuwa ya kawaida sana ila tatizo ni watu kujenga sehemu ambazo siyo stahiri na huu ni uzembe wa watu.

Pia watu wanaambiwa wahame nao wanakaidi amri zinazotolewa na kusema kuwa hawaondoki mabondeni na wanataka walipwe fidia, fedha zitatoka wapi,"alihoji.

Aliwashangaa watu wanaobeza mafanikio ya miaka 50 ya Uhuru wa nchi na kusisitiza kuwa wengi wa wanaobeza maendeleo ya nchi ni vijana lakini ukweli ni kwamba Tanzania imepiga hatua kubwa kwa kipindi hicho.

Kuhusu vurugu ya kisiasa, alisema migogoro ya kisiasa ilikuwepo hata kabla ya miaka 50 ya uhuru na kwamba siyo mipya hivyo kuwataka viongozi kufanya kila liwezekanalo kukabiliana nayo.

Aliwataka wanasiasa na kila mtanzania kumshukuru Mungu kwa ajili ya amani ya nchi na kuweka wazi kuwa kila mzalendo anapaswa kuwa adui na anayechezea amani ya nchi.

Tayari Bunge imetoa azimio la kuitaka serikali kumchukulia hatua za kinidhamu Bw. Jairo na Bw. luhanjo.

Hata hivyo baadhi ya wanasheria waliwai kuiambia gazeti hili kuwa kuna uwezekano mdogo kwa watendaji hao wa serikali kuchukuliwa hatua kama ilivyoamriwa na bunge.
 
Mzee Wa Upako amuunga Mkono Babu wa Loliondo

Na Mwandishi wetu

Mzee wa Upako, Mchungaji Anthony Lusekelo (pichani) amemtibulia kupata wateja Mchungaji Ambilikile Masapile baada ya kuweka kambi katika Jiji la Arusha ambako aliibuka akiwa na maji na mafuta ya upako.

Kutibuliwa kwa Babu kulishuhudiwa na mwandishi wetu hivi karibuni baada ya kushuhudia wagonjwa wengi ambao walikuwa na mpango wa kwenda kijijini Samunge kupata kikombe kukatiza safari zao na kwenda katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid au katika Jengo la Sinema la Metropole kupata upako wa Mchungaji Lusekelo.

Baadhi ya wagonjwa waliozungumza na mwandishi wetu akiwemo Suzan John, walisema kwa nyakati tofauti kuwa, waliambiwa kwamba Mzee wa Upako yupo jijini hapo, na kwa kushawishiwa na baadhi ya wagonjwa waliokwenda kwa Babu na kutopata nafuu waende kwa Mzee wa Upako kuliko kuendelea kungoja foleni ya kwenda Samunge.

"Mimi kuna mtu aliniambia matatizo yangu yanaponywa na Mzee wa Upako, hivyo nikaamua kukatiza safari ya Samunge nikaenda Metropole Sinema na kweli nilipoombewa tatizo langu likatoweka," alisema Suzana aliyedai kutoka Bunda.

Mwandishi wetu alishuhudia wagonjwa wengi kutoka mikoani wakiacha safari ya kwenda kwa Babu na kuhudhuria maombi ya Mzee wa Upako ambaye alitangaza wazi kuwa, kwake kuna uponyaji wa kweli wa Mungu.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu juzi (Jumapili), Mchungaji Lusekelo alikiri kuwa ni kweli aliweka kambi Arusha na kuokoa watu wengi ambao walitaka kwenda kwa Babu na hata wale waliokwenda na kutoponywa.

"Kwanza siku hiyo kulikuwa na mvua nyingi sana, nikaikemea na ikaacha kunyesha, upinde wa mvua ukakunjika katikati ya uwanja, watu walishangaa sana.

"Lakini pia kulikuwa na wagonjwa, kwa mfano mama mmoja alikuwa mjamzito na alikuwa hajifungui, kuna mzee mmoja alikuwa amevimba miguu na baadhi yao walipata kikombe lakini hawakupona, niliwaombea na wakapona," alisema Mzee wa Upako.

Alipoulizwa njia anayotumia kuponya watu alisema:"Ninatoa maji ya uzima ambayo nayabariki kwa mikono yangu na yanatibu magonjwa sugu tofauti na hicho kikombe kimoja wananchi wanachokikimbilia huko Loliondo," alisema Lusekelo.

Akaongeza kuwa, anaamini maji hayo anayotoa ni zaidi ya kikombe cha Babu wa Loliondo na amewaomba wananchi kuyanywa kwani yanaponya magonjwa sugu.
Alitamba kuwa, alilitikisa anga la Mkoa wa Arusha baada ya kupata mapokezi makubwa licha ya kuwepo kikombe cha Babu huyo.

SERIKALI YA KIJIJI KUSITISHA HUDUMA
Wakati hayo yakiendelea, habari zaidi zinasema uongozi wa Kijiji cha Samunge, umeiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuwaondoa maofisa wake wanaokusanya ushuru wa magari na helikopta zinazopeleka wagonjwa kijijini hapo kupata tiba inayotolewa na Mchungaji Masapile, vinginevyo itasitisha utoaji wa huduma ya tiba.

Uamuzi huo ulifikiwa wiki iliyopita katika Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Samunge, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nanenane na kuhudhuriwa na maofisa kadhaa wa serikali, akiwemo mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngorongoro, Bakari Gaima.

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji hicho, Michael Lengume alisema katika mkutano huo kuwa, serikali yao inamtaka mkurugenzi kuwaondoa maofisa wanaokusanya ushuru wa magari na helikopta katika eneo hilo na kazi hiyo sasa ifanywe na wakusanya ushuru wa kijiji.

"Kama halmashauri itakaidi agizo hilo, tutasitisha utoaji wa huduma ya tiba katika kijiji hiki baada ya kukutana na Mchungaji Masapile na tutayazuia magari kuingia hapa," alisema na kufanya baadhi ya wagonjwa waliosikia kauli hiyo kunyong'onyea.

VIONGOZI WA KIMILA WAPINGA
Naye Kiongozi Mkuu wa mila wa Kabila la Wasonjo (Mwanamiji), Peter Dudui,
alisema viongozi wa mila wanapinga utaratibu wa halmashauri wa kukusanya mapato yote bila kueleza kijiji kitanufaika vipi na ujio wa maelfu ya watu hapo kwao.

"Vyanzo vya maji vimechafuliwa, mashamba yameharibiwa kutokana na kutupwa takataka mbalimbali kama chupa za maji, mifuko ya plastiki na magari yanaegeshwa mashambani, njaa itakuja. Je, nani atawasaidia hawa wananchi?" Alihoji Dudui.

Tangu Mchungaji Masapile aanze kutoa tiba ya magonjwa mwanzoni mwa mwaka huu, wastani wa magari 500 yanafika Samunge kwa siku na kutozwa shilingi 2,000 geti la kuingilia na shilingi 5,000 geti la kutokea, huku helikopta ikifanya safari zake kwa wiki mara nne hadi sita.

Akijitetea, Gaima aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, alisema haijapora mapato ya kijiji, bali wanatekeleza uamuzi wa kikao cha wakuu wa mikoa inayopakana na Ngorongoro na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Gaima alisema kikao hicho kiliamua kuwa, halmashauri ikusanye Sh 5,000 kwa kila gari na kati ya hizo Sh 3,000 zitapelekwa kusaidia vituo vya kuratibu magari yanayokwenda Samunge, vya Bunda, Arusha, Longido na Babati na nyingine Sh 2,000 zitabaki halmashauri.

WANAJESHI WAMWAGWA
Wakati huo huo, wanajeshi ambao ni wahandisi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambalo lipo chini ya Mkuu wa Majeshi, Jenerali David Mwamunyange, tayari wamefika Samunge kwa ajili ya kuainisha maeneo ya kuchimba vyoo ili kuimarisha usafi kwa kuwa huduma hiyo ni mbaya kijijini Samunge kwa Babu na Loliondo.
Wanajeshi hao tayari wamepewa kikombe na Babu kabla ya kuanza kazi.

HUDUMA KUSITISHWA PASAKA
Mchungaji Masapile amesema kuwa atasitisha tiba yake hiyo kwa siku mbili, Ijumaa Kuu na Jumapili ya Pasaka ili kupata muda wa kusali.
 
[h=2]30 March 2011[/h] [h=3]Mzee wa upako aibuka akimfagilia JK [/h]
Na Edmund Mihale

MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' amesema kuwa wanaompinga, Rais Jakaya Kikwete katika utawala
wake wapo katika ushindani lakini hawatashinda katika vita hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kile alichokiita Afya ya Amani, Umoja, Upendo na Uvumilivu, Mchungaji Lisekelo alisema kuwa ili nchi iwe na afya inahitaji matunzo na si kelele za kulaumiana.

Alisema kulaumiana kumeshika kasi tangu Rais Kikwete ashike madaraka kwa miaka mitano lakini mazuri aliyoyafanya hayasemwi bali mabaya ndiyo yanayozungumzwa hata kama yamejificha.

Kauli za Mchungaji Lusekelo zimekuja kukiwa na malalamiko ndani ya jamii, kuhusiana na utendaji kazi wa serikali ya awamu ya nne, hasa kushindwa kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa muhimu na kupunguza umaskini.

Lakini yeye alisema, "Unapojenga afya ya kitu chochote ni lazima ujue misingi ya nchi ni lazima tuheshimu na kuwapenda viongozi wetu tuliochagua na kuwapigia kura. Hata katika maandiko kiongozi anatakiwa aonywe kwa hadhari, heshima na hekima na si kwa makelele.

"Utawala ni mamlaka inayowekwa Mungu lakini inaashiria wazi kuwa tumeanza kuondoka katika misingi hiyo na sasa mtu yeyote anasimama na kumsema Rais Jakaya Kikwete anavyotaka. Hapana. Hili jambo halipendezi mbele ya Mungu," alisema Mchungaji Lusekelo.

Alisema imejengeka tabia kuwa ukimsema Rais Kikwete ndiyo unaonekana kuwa jasiri na mzalendo, utamaduni ambao ni mbaya.

"Hatupo tayari kumpongeza kiongozi akiwa hai, watu wanasifu maiti kuliko mtu akiwa hai hizi ni fikra za kishetani na hazipaswi kunyamaziwa.

"Mfano Mwalimu alipokuwa hai hakuwa na sifa hizi tunazoziona sasa, walisema wazi wamechoka na 'unyerere' leo hii tunamasifu kwa kila nderemo. Watu wamebadilika wanasifu viongozi wanapotoka ndani ya madaraka.

"Inakuwaje Rais Kikwete tunayemfahamu aliingia madarakani akiitwa Masia na chaguo la Mungu leo ni adui wa kwanza. Hili linatokana na wachache wanaomsaidia rais kukiacha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa na nguvu na kikaacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa dhaifu. Hivi sasa kukitokea tatizo kama la kutonyesha mvua basi lawama atatupiwa rais," alisema

Alisema kuwa ana imani kuwa rais atakayekumbukwa maishani ni Rais Kikwete hivyo aachwe atekeleleze mchakato wa katiba kupunguza mfumko wa bei na kujenga barabara za hewani.
 
Ataumbuka muda si mrefu kwa propaganda zake anazoeneza,alafu ni bora aweke wazi kwamba na yeye ameshakuwa mwanasiasa, tena siasa uchwara.
 
mwingira.jpg

VIONGOZI WA DINI WANA ANGALIA MASLAHI
[h=3]Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)[/h]
 
Uzao wa nyoka huo.. tabia za uzao huo ni kujisahau mara unapofanikiwa iwe kwa njia yoyote ile, mchungaji sasa amefanikiwa anasahau waumini wake ndio wamemfikisha hapo alipo hata kama anawadanganya, hajali wanaumia vipi katika utawala huu..
 
Mzee wa upako usitupumbaze, tuna hoja za kumweleza Kikwete




Abdul Juma​
amka2.gif

NAWASHUKURU wasomaji wangu wote ambao mliniandikia kunipa maoni yenu kuhusu makala yangu ya juma lililopita yaliyosomeka: "Kuyavumilia haya ni kujiongezea matatizo."
Hakika nimeguswa sana na michango yenu. Na kusema kweli ni vigumu kuandika kila alichokisema mtu, yawezekana nisimalize.
Lakini katika mengi mazuri lipo zuri kupita yote. Naomba kunukuu ujumbe wa msomaji wangu mmoja kutoka wilayani Kahama.
"Kaka wewe ni chemchem ya fikra mpya, hakika unatufungua macho na napendekeza kolamu yako iitwe ‘fikra mpya'," ndivyo ulisomeka ujumbe huo.
Kweli nimehamasika na kufurahishwa jinsi wananchi wamepata mwamko wa kusoma na kusikiliza vyombo vya habari ili kujua mustakabali wa nchi yao.
Hivyo katika utangulizi wangu wa leo, naomba kuwafahamisheni kuwa uwanja wetu huu utajulikana kwa jina jipya la "Fikra mpya". Kweli mawazo yenu ndiyo yatafanikisha fikra hizo.
Mada yangu leo itamhusu mtumishi wa Mungu maarufu kama Mzee wa Upako, ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo.
Sikuwa na mpango wa kumjadili kiongozi huyu wa kiroho ila kauli yake ya karibuni imenisukuma kujitokeza kumpa neno kuwa aache kutupumbaza, kwani tunazo sababu za kumlaumu Rais Jakaya Kikwete.
Sina hakika kama mchungaji anajua kuwa Kikwete si Mungu bali ni binadamu kama sisi ambao tumempa jukumu la kutuongoza, hivyo akishindwa ni lazima tumhoji ilikuwaje?
Mungu hatumjui, maana hatujawahi kumuona bali tunaamini tu kuwa yupo. Tumejikuta tulivyoumbwa na huyo Mungu wala hakuna aliyemfikia na kuomba aumbwe, kwa hivyo hatuwezi kuhoji hilo.
Lakini kwa Rais Kikwete ni tofauti, yeye alijitafakari akahisi anaweza kutuongoza, hivyo kupitia chama chake cha CCM alikuja kutuomba tumchague atimize yale aliyoahidi kufanya.
Sasa kuna kosa gani ikiwa wananchi wanahoji ahadi zao Rais? Mchungaji Lusekelo anataka tuseme tu ameni kama kanisani ilihali tunaona mambo ni magumu?
Kwa kuwa huyu ni mtumishi wa Mungu basi naomba apime kauli zake upya kwa kutumia ‘busara'. Tafsiri ya neno busara ni akili au werevu wa kuweza kufikiria na kuamua kutenda jambo linalofaa.
Kweli tuamini kuwa busara ya mchungaji Lusekelo ni kuwaona Watanzania wakiimba nyimbo na mapambio ya kumsifu Rais Kikwete wakati wakiogelea kwenye dimbwi la kero zisizo na ukomo?
Kwa akili ya kawaida na pengine kwa kumsaidia mchungaji Lusekelo ni kwamba Rais akichaguliwa tunamtegemea atende mazuri, hivyo hatupaswi kumsifia bali kumkumbusha pale ambapo amekosea.
Lakini mwanzoni mwa wiki hii, mchungaji Lusekelo aliibuka kwenye vyombo vya habari akisema eti wanaompinga Rais Kikwete katika utawala wake wapo katika ushindani lakini hawatashinda katika vita hiyo.
Katika kile alichokiita Afya ya Amani, Umoja, Upendo na Uvumilivu, Mchungaji Lisekelo alisema kuwa ili nchi iwe na afya inahitaji matunzo na si kelele za kulaumiana.
Alisema kulaumiana kumeshika kasi tangu Rais Kikwete ashike madaraka kwa miaka mitano lakini mazuri aliyoyafanya hayasemwi bali mabaya ndiyo yanayozungumzwa hata kama yamejificha.
"Unapojenga afya ya kitu chochote ni lazima ujue misingi ya nchi ni lazima tuheshimu na kuwapenda viongozi wetu tuliochagua na kuwapigia kura.
Akaongeza kuwa hata katika maandiko kiongozi anatakiwa aonywe kwa hadhari, heshima na hekima na si kwa makelele.
"Utawala ni mamlaka inayowekwa Mungu lakini inaashiria wazi kuwa tumeanza kuondoka katika misingi hiyo na sasa mtu yeyote anasimama na kumsema Rais Kikwete anavyotaka," alisema Mchungaji Lusekelo.
Akahoji, inakuwaje Rais Kikwete tunayemfahamu aliingia madarakani akiitwa Masia na chaguo la Mungu leo ni adui wa kwanza?
Kwa mahaba yake, anaamini kuwa hali hiyo inatokana na wachache wanaomsaidia rais kuiacha CHADEMA kuwa na nguvu na kuiacha CCM kuwa dhaifu.
"Hivi sasa kukitokea tatizo kama la kutonyesha mvua basi lawama atatupiwa Rais. Nina imani kuwa rais atakayekumbukwa maishani ni Rais Kikwete," alisema Mchungaji Lusekelo.
Hivyo ndivyo anavyoamini kiongozi huyo ambaye hataki tumwambie rais wetu kuwa giza limetuchosha, ufisadi unatukera chukua hatua, bei za bidhaa zimepanda kuliko kipato chetu.
Afya ya amani, upendo, mshikamano anayoihubiri Mchungaji Lusekelo haiwezi kupatikana katika taifa ambalo lina matabaka makubwa mawili ya wenye nacho na wale wasio nacho.
Nakubaliana na Mzee wa Upako kuwa anayo haja ya kutukataza tusimlalamikie Rais matatizo yetu kwa kuwa yeye si sehemu ya matatizo tunayokabiliana nayo.
Yeye hatembei tena kwa daladala akaona uchungu wa kupanda kwa nauli, kipato kinachotokana na kazi yake ni kikubwa kiasi kwamba maumivu ya gharama za mahitaji muhimu hayapati kama sisi.
Lakini kwa upeo wake alionao Mchungaji Lusekelo, sikutegtemea kama anatoa kauli tata kama ile.
Mara anasema kipindi cha Kikwete lawama zimezidi, hatutashinda vita hiyo na eti wasaidizi wa Rais waiacha CHADEMA itanue na CCM imedhoofike.
Hapa ni bora Mzee wa Upako angejitambulisha wazi kuwa ni mwana-CCM maana si dhambi. Kama alikuwa na hoja angepaswa kujihoji ni kwanini alaumiwe Kikwete kati ya marais wanne waliopita?
Kwa kujihoji swali hilo, falsafa yake asingeitumia kututisha kuwa hatutashinda vita ya kumlalamikia Rais Kikwete bali angetutia faraja na hamasa kuwa tumwombee atimize ahadi zake bila kuogopa mafisadi.
Kama kuimarika kwa CHADEMA kunamtisha na kumuuma Mchungaji Lusekelo, inafaa awe shujaa wa kukisaidia chama chake cha CCM kijirudi na kujivua udhaifu ili kirejeshe mvuto kwa wananchi.
'Kioo cha mtu ni mtu' wanasema wahenga. Kumbe sisi tunaoona udhaifu wa Rais Kikwete na kumweleza wazi ni waungwana kuliko unafiki anaotaka tufanye Mchungaji Lusekelo wa kupongeza kila kitu.
Kanisani tunasema ameni kwa kila kitu kwa kuwa ni imani zaidi lakini kama tungepewa mamlaka ya kuhoji,basi sadaka zingehojiwa zaidi. Kwenye siasa hakuna ameni wala ndiyo mzee tena. Tafakari.




Niachie ujumbe: 0788452350 au mpyafikra@yahoo.com

 
Lusekelo anafikiri anajua kila kitu. Yeye huyo ana kipawa cha uponyaji, yeye anajua masuala ya ndoa, yeye ni mtaalama wa katiba kuliko Prof. Shivji. Unawezaje kumlinganisha Prof. Shivji na Lusekelo katika masuala ya sheria hasa katiba, kwa lipi hasa?Lusekelo abaki kanisani kuombea wagonjwa. Nakumbuka siku moja nilinunua gazeti la Jambo kama mwaka 1 uliopita, nikakuta makala yake akiuteta utawala wa bwana mkubwa mpaka nikashangaa, anatetea uozo.
Tuwe makini na hawa viongozi wetu wa dini. Tuwaheshimu lakini si kila kitu wanachozungumza ni sahihi
 
Kuna kijana alikua anataka kuurithi ufalme wa mungu akamfata yesu akamwambia,"bwana yesu nifanyaje niurithi ufalme wa mungu?" Yesu akamjibu fuata amri zote za mungu na mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe,yule kijana akamwambia yote nilishayafanya tangia mdogo,basi naye yesu akamjibu "uza mali zako zote uwagawie masikini". Swali langu hivi Mch.Anthony Lusekelo ndo yule anayetembelea HUMMER na kuna kipindi aliingiliwa na majambazi wakampora million 20 ndo yeye huyo au mwingine?

Ndo huyo huyo waumini wake wanajinyima na wengine wanashindwa kupeleka watoto wao shule kwa kumtolea yeye sadaka alafu yeye anaishi maisha ya anasa kweli kuina mbingu ni ni kazi kwelikweli. Hawezi kupambana na prof. yeye huyo mchungj ni kibaraka tu
 
Back
Top Bottom