injala mbibí
Akimsifia ujinga lazima tumnange. hapa hakuna kuangalia cheo wala sura ya mtuVipi kama angemsifia Dr Slaa? Mngemsakama na kumnanga? SHAME ON YOU
Mchungaji huyu namheshimu sana lakini nadhani yeye haoni hali halisi jinsi ilivyo mtaani. Amesahau jinsi watu wanavyofanya madudu kupitia cheo cha urais, namkumbusha mzee wa upako kuwa aache kuingia kwenye siasa inaweza kumshusha hadhi haraka sana na si yeye tu bali viongozi wote wa dini.
Mchungaji huyu namheshimu sana lakini nadhani yeye haoni hali halisi jinsi ilivyo mtaani. Amesahau jinsi watu wanavyofanya madudu kupitia cheo cha urais, namkumbusha mzee wa upako kuwa aache kuingia kwenye siasa inaweza kumshusha hadhi haraka sana na si yeye tu bali viongozi wote wa dini.
>>"Unapojenga afya ya kitu chochote ni lazima ujue misingi ya nchi ni lazima tuheshimu na kuwapenda viongozi wetu tuliochagua na kuwapigia kura. Hata katika maandiko kiongozi anatakiwa aonywe kwa hadhari, heshima na hekima na si kwa makelele.
"Utawala ni mamlaka inayowekwa Mungu lakini inaashiria wazi kuwa tumeanza kuondoka katika misingi hiyo na sasa mtu yeyote anasimama na kumsema Rais Jakaya Kikwete anavyotaka. Hapana. Hili jambo halipendezi mbele ya Mungu," alisema Mchungaji Lusekelo.
Alisema imejengeka tabia kuwa ukimsema Rais Kikwete ndiyo unaonekana kuwa jasiri na mzalendo, utamaduni ambao ni mbaya.
"Hatupo tayari kumpongeza kiongozi akiwa hai, watu wanasifu maiti kuliko mtu akiwa hai hizi ni fikra za kishetani na hazipaswi kunyamaziwa.
"Mfano Mwalimu alipokuwa hai hakuwa na sifa hizi tunazoziona sasa, walisema wazi wamechoka na 'unyerere' leo hii tunamasifu kwa kila nderemo. Watu wamebadilika wanasifu viongozi wanapotoka ndani ya madaraka.
"Inakuwaje Rais Kikwete tunayemfahamu aliingia madarakani akiitwa Masia na chaguo la Mungu leo ni adui wa kwanza. Hili linatokana na wachache wanaomsaidia rais kukiacha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA):hug:kuwa na nguvu na kikaacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa dhaifu. Hivi sasa kukitokea tatizo kama la kutonyesha mvua basi lawama atatupiwa rais," alisema
Alisema kuwa ana imani kuwa rais atakayekumbukwa maishani ni Rais Kikwete hivyo aachwe atekeleleze mchakato wa katiba kupunguza mfumko wa bei na kujenga barabara za hewani.<<
Teh teh hata mimi nilisikia juu ya hili ila sikujua kama wapakwa mafuta wa bwana nao wamo , teh inapungua na kupanda kama CD4?Niliwahi kumsikia mtaalamu mmoja wa afya ya akili akisema karibu watu wote tuna matatizo vichwani, isipokuwa kiwango cha matatizo ya akili ndicho kinafanya wenzetu kuwehuka na sisi kujiona wazima. Huyu mchungaji nahisi kiwango kinaongezeka kwa kasi.........
Kwanza, naona huyu mchungaji ni kibaraka! Kuheshimu mamlaka ni pamoja na kuikosoa (kuisaidia) mamlaka ili uwazi na uwajibikaji uongezeke. Kuna njia nyingi za kuwajibisha mamlaka. Njia mojawapo ni kupitia kura na nyingine ni kukosoa (constructive criticism) - kusema namna gani kitu fulani kingeweza kufanywa kwa namna bora zaidi. Yohana Mbatizaji alifanya hivyo kwa watu mbalimbali. Mafundisho ya Yesu nayo yalilenga hayo mamlaka - kubadilisha/kuboresha mfumo wa utawala ili haki itendeke zaidi kwa watu wa kawaida. Sasa huyo mchungaji yeye mafundisho yake anayatoa wapi kama siyo kwa Yesu?
Pili, huyo mchungaji uwezo wake wa kuchambua maandiko matakatifu unatia shaka! Kwa nini Musa alutumwa kuwakomboa Waisrael Misri kutoka kwa utawala dhalimu kama kutii mamlaka ni kukaa kimya na kukubali uovu wa wawatawala uendelee?
Tatu, kama anachokisema kina 'logic' basi kwa nini watu ambao Mungu aliwaumbwa "na tazama kila alichoumba ni chema" leo kuna magenge ya mafisaidi, wauaji, wabakaji, wachakachuaji... nk? Si tungeamini tu kuwa kila alichoumba Mungu ni chema na hivyo hakuna maovu duniani? Watu wanaweza kuchaguliwa na Mungu lakini Mungu huyohuyo kawapa utashi wa kuchagua mema na mabaya. Mtu akichagua kutenda mema tutamsifia. Akichagua vibaya, tutamkosoa. Hii yote ni kutaka tusonge mbele. Kwa mawazo ya huyo mchungaji kwa vile mtu ameumbwa na Mungu, kwa hiyo hakuna namna anayoweza kutenda mabaya. Sasa yeye huwa anawahubiria watu walioumbwa na nani kama siyo Mungu?