Albedo
JF-Expert Member
- Feb 24, 2008
- 5,559
- 1,452
Mbinguni kutakuwa na Mchanganyiko wa Wakatoliki, Walutheri, Wasabato, Walokole,Waanglikana, wa TAG, wa EAGT nk provided that wameyashika na Kuyaishi Maisha ya Kikristo
Jehanam kutakuwa na Mchanganyiko wa Wakatoliki, Walutheri, Wasabato, Walokole,Waanglikana, wa TAG, wa EAGT nk provided that hawakuyashika na Kuyaishi Mafundisho ya Yesu
Biblia inasema watu wataangamia kwa Kukosa Maarifa, Maarifa ya kwenda Mbinguni ni Kumtumikia Mungu kwa Moyo wako wote, kumpenda jirani yako kama unavyojipenda wewe, Kuwanyia/kutowanyia wengine mambo ambayo wewe ungependa/usingependa wakufanyie/wasikufanyie
Kukaa hapa na Kupoteza Muda wa Kubishana lipi ni kanisa na lipi si kanisa la Kistro inaonyesha ni jisni gani tulivyofilisika na namna gani tusivyojua ABC za kuurithi Ufamle wa Mungu Yohana Mtakatifu 14:6 na kuendelea!
Tusipokuwa makini Yesu atatukuta tukiwa bize kutafuta ukweli wa lipi ni kanisa lake
Mtakatifu paulo na Anasema dini iliyo ya Kweli ni kwenda kuwatazama wagonjwa nk, yaani kufanya Matendo ya Upendo kwa Wenzetu
Ndugu zangu ili muweze kuurithi Ufalme wa Mungu ni Lazima mpendane kama Yesu alivyotupenda, kama Mungu alivyotupenda hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila amwamiaye asipotee bali apate uzima wa milele
Mtakatifu Paulo anasisitiza juu ya Upendo, anasema kwama Hata nikinena kwa Lugha za Wanadamu na Malaika kama sina Upendo mimi si kitu kabisa na sifai Mbele za Bwana, hata nikiwa na Imani ya Kuhamisha Milima kama sina Upendo mimi si kitu na sifai Mbele za Bwana.
Ndugu zangu katika Kristo ikibidi hata Tuwachallenge Viongozi wetu wa Kanisa ambako wanahamisha sana juu ya Utoaji je Wanawakumbuka Vipi Ndugu zetu katika Kristo wanaoteseka Kilosa kwa Mafuriko? Au wao kuomba Utukufu kwa Serikali za Kibinadamu ndiyo Kipaumbele? Wana JF wenzangu wapendwa katika Kristu je Tumehamasika vipi kuchangia Wahanga wa Mafuriko ya Kilosa au tunakesha hapa tukishabia hizi lebbel zetu za Ukatoliki, Ulokole n.k Je Bwana Yesu anapendezwa nasi?
Tujichunguze Ndugu zangu tuone ni kwa namna tunatekeleza yale aliyotuagiza Bwana wetu Yesu Kristo, Yesu aliwafariji Wagonjwa hata Wafiwa yatupasa kufanya hivyo ili tuweze kuurithi Ufalme ambao tumeahidiwa katika Ile Sura ya 14:2-4 ya Injili ya Mtakatifu Yohane
Mwisho: Changia wahanga wa Mafuriko Kilosa ili Tuonyeshe Upendo ambao Bwana wetu Yesu Kristo amekuwa akiuhubiri katika miaka yake 33 ambayo aliishi katika hii Dunia
Tumsifu Yesu Kristo, Milele Amina