Mzee wa upako abariki dawa ya babu

birungi

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
391
16
Habari za leo wanajamii wenzangu.
jana katika kipindi cha tutashinda cha mzee wa upako channel 10 nilimsikiliza mwanzo mpaka mwisho.kilikua ni maswali na majibu kuhusu huduma yake na mipango kiujumla maana anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa arusha.

katika maswali na majibu,mida ya saa 4:40 usiku aliulizwa swali kwamba analiongeleaje swala la dawa ya babu wa loliondo. kwanza akatolea mfano wa mfalme suleiman kwenye biblia na akasema tusiwe haraka kutoa maamuzi ya kukandia kitu au kusifia kitu,inabidi kukipa mda na kutafakari ndio mtu utamke.akaongeza kuwa kwa upande wake anaibariki dawa ya babu na atazidi kuiombea izidi kuwaponya watu,endapo tu haihusiani na ushirikina.kasema hajasikia masharti kuwa labda kainywe njia panda au rudi kinyumenyume au kupiga ramli,so iendelee kuponya watu.

pia aliongezea kuwa watanzania tusijiweke nyuma kiasi hichi.karibu dawa nyingi hata ulaya zinatengenezwa kwa mzizi. tusijiwekee fikra tu kwamba atakachovumbua mzungu ndio sahihi ila cha ngozi nyeusi ndio uongo.MUNGU ameamua kutukomboa tena kwa kupitia mwafrika. akasisitiza tunachoomba ni uzima wa wananchi maana afya ndio nguvu kazi na hitaji muhimu la wanadamu.sasa kama watu wanakunywa na kupona MUNGU na azidi kuibariki na hata huyo babu abarikiwe azidi kuponya watu alimalizia mchungaji.na pia anazidi kumuombea.atakua na mkutano arusha na amekaribisha watu waende kwa wingi kupata upako na waende loliondo kushushia dawa ya babu waponywe zaidi.maana dawa ya babu inatibu magonjwa matano ila yeye atakupa upako wa kibali kazini,kupata ajira,milango ya fedha,kuponywa mapepo,uwete na magonjwa mbalimbali.
kwa upande wangu niliridhishwa na uchambuzi alioutoa.
 
Kweli babu ni chiboko, anatibu yale akina upako wameshindwa !
 
Ukisema hivyo unakosea Mungu ana vyombo vingi vingine vya chuma, bati, gold, almasi na babu ni moja kati ya chombo chake, si lazima mtu 1 upewe vipawa vyote na, ndo maana kuna walimu, wachungaji, wainjilisti na Manabii kila mtu ana kazi yake,
 
ni kweli, tofauti ni kwamba dawa ya babu inatibu magonjwa sugu. na maombi yanatibu yote ingeneral hata ambalo sio gonjwa kama kuondolewa nuksi au kupata baraka maishani
 
mzee wa upako kajitahidi kusema vyema.
waacheni wanaoamini kwa babu waende kwani la msingi ni kupona tu
 
Ukisema hivyo unakosea Mungu ana vyombo vingi vingine vya chuma, bati, gold, almasi na babu ni moja kati ya chombo chake, si lazima mtu 1 upewe vipawa vyote na, ndo maana kuna walimu, wachungaji, wainjilisti na Manabii kila mtu ana kazi yake,

amina mkuu
 
sawasawa kabisa,si rahisi kumkuta muinjilisti akiponya,au nabii akifundisha.ni basi tu wengine kujiongezea majukumu,muinjilisti huyohuyo,nabii na shemasi huyohuyo. kwa hiyo huyu atahubiri neno la mungu na yule ataponyesha magonjwa.
 
Kazi ya Mungu huwa haihitaji credit za wanadamu. Mwanadamu huwezi pima njia za Mungu, hutatofautiana na yule aliyetaka kukausha bahari kwa kikombe na kujaza maji yote kwe kishimo kidogo alichochimba. Acheni Mungu aitwe Mungu.
 
Babu ametumwa na CCM kula muda wa kuijadili Katiba,Dowans,Kiwira,IPTL na kashfa nyingine.Hana lolote.....msanii tu
 
ni kweli mungu ana njia nyingi,kuna kipofu aliepona kwa kupakwa tope,na aliepona ukoma kwa kuoga maji baharini.
hata hichi kikombe cha dawa ya babu ni njia nyingine ya mungu.
 
Babu ametumwa na CCM kula muda wa kuijadili Katiba,Dowans,Kiwira,IPTL na kashfa nyingine.Hana lolote.....msanii tu

kama ni kweli ametumwa na ccm basi wapo juu aisee. yani dawa inaponyesha magonjwa sugu live. nikigundua ni kweli ntahamia chama hicho mimi na familia yangu.
 
mnh mzee waupako kanena sasa makavirondowengine siuji wanabisha nini,et we ZUBEDA ukwapy?
 
Babu ametumwa na CCM kula muda wa kuijadili Katiba,Dowans,Kiwira,IPTL na kashfa nyingine.Hana lolote.....msanii tu
mh! sidhani kama ni kweli, kwani wagonjwa waliotoka mahospitalini walikolazwa kwa muda mrefu ndo wadau wakuu wa majadiliano ya dowans na ....? by the way babu hajamwita mtu, wanamfata wenyewe na dawa yake sio ya kutibu kuongea na kuziba midomo bali inatibu magonjwa sugu tu 'kwa mujibu wake' hivyo watu kushindwa kujadili hoja kusihusishwe na babu
 
mzee wa upako ameonesha utafauti, wenzie wameonesha uchoyo wa fadhila, lakini wakumbuke kuwa mungu hakuweka ahadi popote kuwa mwingira na kakobe hasa ndo wenye mamlaka ya kuponya na kuombea watu, kama kuna mtu ana karama ya kutoa huduma kama anayoitowa babu anatakiwa ajidhihirishe na kutoa huduma hiyo, sio wakati wa kupigama vijembe.
 
yatasemwa mengi sanaaa naona watu wameshasahau hata nini kinaendelea upande mwingine. Wakija kukumbuka deni la dowans lishalipwa zamaniii unabakia ugomvi tu aaah lililipwaje ....oooh haiwezekani......aaahg yaaani viongozi mafisadi kweli......eeeeeh Tanzania shamba la bibi. Wakati wenzao weshachukua chao zamaniiiiiiiiiii
 
Jamani tuwe makini na hawa ambao wanajipachika vyeo vya kidini. Isije kuwa ni huu mlinganyo,

Mzee wa Upako=Babu=Waumini wengi.

Hapa mtu anaweza toka kule kwa babu na kuja kwa mzee wa upako maana yeye na babu wapo sawa, lakini kwa Mwingira, tofauti, so uponyaji kwa babu hauwezi dumu kule imani inaweza teketea.
 
[Babu ametumwa na CCM kula muda wa kuijadili Katiba,Dowans,Kiwira,IPTL na kashfa nyingine.Hana lolote.....msanii tu
Duh.....! hii ni sawa na John alipoulizwa saa na Bashiri akamjibu kua si mwenyeji mmaeneo haya!
swala la UKIMWI,KISUKARI,SHINIKIZO LA DAMU, na magonjwa mengine kupatiwa tiba kwa babu kwa sh 500 linahusiana vp na SIASA??
Jamana nyepesinyepesi ambazo sijazithibitisha nasikia hata rais wetu Mh Jakaya Mrisho Kikwete nae amekwenda kwa babu sasa na Ndesapesa nae yuko njiani kweli huyu ametumwa na CCM?
Kama ni kweli basi akimaliza kazi yake babu atatumwa pia akawalipe hoa woooote!
 
mzee wa upako kajitahidi kusema vyema.
waacheni wanaoamini kwa babu waende kwani la msingi ni kupona tu

Lusekelo mjanja...kaangalia upepo unakovuma nae akaelekea hukohuko, kwasasa ukitaka ulaaniwe wewe sema dawa ya babu ni kimeo!

Lusekelo is a sort of opportunistic buddy! big up mzee wa upako...wewe ndio unajua jinsi ya kuendesha biashara ya dini kuliko Kakobe na Mwingira.
 
Lusekelo mjanja...kaangalia upepo unakovuma nae akaelekea hukohuko, kwasasa ukitaka ulaaniwe wewe sema dawa ya babu ni kimeo!

Lusekelo is a sort opportunistic buddy! big up mzee wa upako...wewe ndio unajua jinsi ya kuendesha biashara ya dini kuliko Kakobe na Mwingira.

Hiyo Red hata mimi naona hivyo hivyo!!!
 
Back
Top Bottom