Mzee wa LIWALO NA LIWE asita kutoa tamko.

MDAU JR

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
451
82
Serikali yasitisha kutoa tamko juu ya madaktari leo

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Waziri Mkuu Mizengo Pinda ametangaza kusitisha Serikali kutoa tamko lake kuhusu mgomo wa madaktari, ambao ulitakiwa kutolewa leo kama alivyoahidi jana Bungeni.Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Waziri Mkuu, Pinda, alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, aliyetaka kujua Serikali ina mipango gani ya dharula ya kuumaliza mgomo huo. Alisema kwa hivi sasa, Serikali imechukua dharura, kwa kuwaita madaktari wastaafu kwenda kwenye baadhi ya Hospitali za Serikali kushika nafasi maeneo ambayo madaktari waliogoma. Vilevile Serikali imewataka wananchi waende kuhudumiwa kwenye hospitali za Jeshi, ikiwemo Lugalo.

Kuhusu Dkt Stephen Ulimboka, Mhe. Pinda ameseama kuwa hata yeye alipopokea taarifa kuwa Dkt. Ulimboka ametekwa na kupigwa na kwamba alisikitika sana, na anamuombea apone haraka ili waendelee na suluhisho la mgomo huo wa madakatari.

Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya ndani kuunda jopo la wataalamu kuchunguza kwa haraka kuhusu tukio
hilo.


Wakuu kwenye red me nina mashaka, vp wenzangu?
 
Tusingependa kufika huko

LIWALO NA LIWE!
Na tazama, hata ilipotimia mwezi wa Juni wa mwaka, Barazalile la saba lilikutana tena kwa ajili ya Baraza la nane. Nao wakakutanakuzungumzia mustakabali wa taifa teule la wana wa nchi. Nchi ya nadharia yaasali na maziwa. Ni kwa namna gani asali na maziwa vigawanywe sawa sawiamiongoni mwa wana wan nchi.Ndipo aliposimama msimamizi mkuu wa fedha za wana wan chiakiwa na mkoba wenye makadirio ya namna gani asali na maziwa vigawanywe. Nayehuyu ni mrithi wa msimamizi wa awali ambaye kwa mujibu wa Jemedari Mkuualiwatabiria, yeye na wahanga wenzake ya kuwa ile dhoruba ingewapitia mbali,lakini haikuwa hivyo. Naye mwana wa mkulima, akiwa ndiye mkuu wa mawaziri wa Taifala wana wa nchi, Yule ambaye wana nchi katika Baraza la saba hawakuaminialichowafanyia, kwa upole wa mamba aliyeshiba, alifuatilia hatua kwa hatua yaleyote yaliyoletwa mbele ya Baraza. Na kwa unyenyekevu uliofunikwa kwa ngozi safiya mwanakondoo, aliyapatia maelezo masuala yote yale yaliyoelekezwa katikauwanda wake. Alitamalaki mimbarini kwa mbwembwe na madaha. Nao wanabaraza walio upande wake kinasaba wakammiminia sifana kumpelekea maombi kwa njia ya vinubi na vinanda na vigelegelena kusihi,wakiwa chini ya nyao zake kwamba awakumbuke wana wa Kaya zao ya kwamba nao wanasihi kwa unyenyekevu wa nafsi na rohona mwili, ya kuwa wakumbukwe kwa namna itakavyompendeza Jemedari Mkuu, kwenyemgawanyo wa asali na maziwa.Asali na maziwa ambavyo ni urithi wa nchi. Urithiuliotapakaa Kusi na Kaskazi na Mashariki na Magharibi. Urithi ulioenea tokachini ya ardhi na juu ya ardhi na juu ya maji na kwenye vilindi vya maji.Urithi uliojipambanua katika mazao ya nchi yakiwemo dhahabu na almasi na vitona na gesi na mafuta na wanyama na ardhi safi na misitu. Naam, urithi ambaowawakilishi wa Kaya wanauomba kwa unyenyekevu mkuu ili kuugawanya kwa wana wanchi. Nao wawakilishi wakiisha kuahidiwa kufikiriwa kutekelezewa maombi yao,hupiga makofi wakiwa na imani katika kusubiri kufikiriwa kusikilizwakutekelezewa ahadi zao ambazo msimu uliotangulia wa mgawanyo wa urithi wa asalina maziwa, waliomba pia na wakaahidiwa kufikiriwa kusikilizwa kutekelezewaahadi zao.Na ilipofika siku ya Jumatano ya wiki katika muendelezo wa vikao vyaBaraza, kama ilivyo ada alisimama mkuu wa mawaziri na nyuma ya mimbarialisimama kwa unyenyekevu akisubiri kujibu na kutoa ufafanuzi na kupangua hoja,na kuomba huruma kwa naibu mkuu wa Baraza juu ya maswali toka kwa wanabaraza,juu ya mgawanyo wa urithi wa asali na maziwa.Ndipo aliposimama mwanabaraza, mwakilishi wa wana wa Kayayake na kwa niaba ya wana wa nchi ili kuomba mwongozo kupitia kanuni ya 68 (7)ya juzuu ya Baraza. Naye kwa niaba ya wana wa nchi alitaka kujua kupitia kwanaibu wa mkuu wa Baraza kwenda kwa mkuu wa mawaziri, hatua za serikali ya wanawa nchi ilizochukua juu ya mgomo wa matabibu.Naye mkuu wa mawaziri akasema, "Chombo cha kutoa hakikiliwaonya matabibu wasigome, na waende kwenye mabaraza ya habari kueleza niayao ya kuacha kugoma. Nayo serikali ikaendelea kuwa sikivu, lakini matabibu hawakusikia…kauli ya serikali ni ya kuwa matabibu waheshimu amri ya ya chombo cha kutoahaki… tutatoa kauli sahihi ya serikali kesho.Tumeamua kulitaarfu Baraza lako Tukufu maana kwa kweli serikali inafanyakila lililowezekana na sasa watu husema LIWALONA LIWE!Ikawa ilipotolewa kauli hiyo, mioyo ya wana wa nchi ikazizimakwa hofu na taharuki na jazba na hasira na kukata tamaa juu ya kile alichosemamkuu wa mawaziri. Nayo kauli yake ni kauli ya serikali.Na katika kuwaongezea wana wa nchi uchungu na kukata tama nasononeko na woga, habari mbaya zikasambaa, bega kwa bega na kauli ya serikali,ya kuwa kiongozi wa Jumuiya ya matabibu amepatikana akiwa nusu mfu kwakusulubiwa na watu na kisha wakautosa mwili wake wenye majeraha na maumivukando ya msitu akiwa ameviringishwa kamba. Naye alipopatikana na kuonekana,hakika alionekana kuwa na maumivu mno! Mavazi yake yaligandamana na madonda.Mwili wake ulitapakaa damu. Uso wake walimpiga kiasi cha kumpotezea sura, maanaulivimba sana. Naam, walimpa mateso, na kumdhihaki, ya kuwa, kwa kuwa wewe nikiongozi wa matabibu, nawe upate adha ya kile mnachogomea kutoa, yaani tiba kwawana wa nchi.Nao wenzake walipopata habari walimtafuta na kumchukua kwahuruma na upole na majonzi na masikitiko, huku wakilia na kuapiza na kuonya nakulaani kauli ya mkuu wa mawaziri, ambayo ni kauli ya serikali, ya kuwa liwalona liwe!Na katika kuyatafakari hayo, ile sauti ya awali ikavuma tenakama mwangwi kondeni. Ikapenya ndani ya mioyo kama upanga ukatao kuwili.Ikaleta maumivu makali kama uchungu wa mama wakati wa kuzaa. Ikarudisha kumbukumbuzote za madhila waliyowahi kufanyiwa wana wa nchi. Nchi ya urithi wa asali namaziwa. Urithi unaomegwa na watu wa mataifa toka ng'ambo ya mbali. Sauti yenyemaneno ya kuhuisha fikra na mwamko wa kuhimiza wana wa nchi kuamkua toka lindila mawazo yaliyo mapumziko. Toka katika mawazo ya wanaofisadi. Mawazo ya watuwenye kuleta falsafa ya umasikini katika nchi. Sauti ikawa inasema;Ee mkuu mfalme wa kisasi
Mfalme wa kisasi uangaze!
Mwenye kuhukumu nchi, ujitukuze
Uwape wenye kiburi stahili zao.

Mkuu hata lini wasio haki,
Hata lini wasio haki watashangilia?
Ee mkuu wanawaseta watu wako
Wanawatesa warithi wako

Nao husema, mkuu haoni
Mfalme wa wote hafikiri
Enyi wajinga miongoni mwa watu,fikirini
Enyi wapumbavu, lini mtakapopata akili?

Aliyelitia sikio mahali pake asisikie?
Aliyelifanya jicho asione?
Awaadhibuye mataifa asikemee?
Amfundishaye mwanadamu asijue?

Lakini mkuu amekuwa ngome kwetu
Na Mfalme wetu mwamba wetu wakukimbilia
Naye atawarudishia uovu wao
Atawaangamiza katika ubaya wao

Naam, mkuu, Mfalme wetu atawaangamiza.Nayo madhila ya kukosa tiba nimengi. Nayo yanawapata wana wa nchi walio na uwingi wa uduni. Waitegeaoserikali yao Tukufu yenye wingi wa nadharia za urithi wa asali na maziwa.Urithi ambao unasomeka katika vitabu na katika vinywa vya wakuu wa mabaraza namamlaka za nchi. Urithi ambao Baraza la saba linajaribu tena kukaa na kuangaliavipaumbele vya kumegewa. Na kwa kuwa afyani sehemu ya vipaumbele. Na kwa kuwa pia Baraza lililopita na lilolopohayajaweza kusema na shida za sehemu ya afya,na kwa vile afya imeonekana nawatu wote kuwa ni sehemu iliyo muhimu kabisa, Ndipo walipokusanyika matabibuwaliofika hapo kwa ahadi za kuona pepo ya urithi wa asali na maziwa. Naowasitimiziwe kile ambacho Jemedari Mkuu aliahidi kukitimiza, maana imeandikwakatika Yoshua bin Sira (38:1-15);Umheshimu tabibu kwa kadiri ulivyo na haja naye,
na kwa heshima iliyo haki yake,
kwa kuwa Bwana amemuinua kweli kweli.
Kwa maana ni kutoka kwake aliye juu,
tabibu alivyoupata ufundi wake,
hata na kwa mfalme atapokea ada.
Maarifa yake tabibu yatamwinua kichwa chake,
naye atasimama ni mkuu machoni pa wakuu. (na kuendelea).

Ikawa hivyo. Wana wa nchi wakiwa wanasononeka na yaleyanayotokea, kwa shingo upande wakaimeza kwa uchungu kauli ya mkuu wa mawaziri,ya kutolea maelezo mgomo wa matabibu wanaoshughulika na afya zao. Kwa kuwa waliahidiwa kwa kinywa cha mkuu mwenyewe, mbeleya kadamnasi ya wana wa nchi na mbele ya wawakilishi wa Kaya za wana wa nchi yakuwa kesho serikali itatoa kaulirasmi, wana wa nchi walifutika sime zao alani. Sime za machungu na maumivu yamioyo iliyokosa matumani ya ahadi za maisha bora kwa kila mwana wa nchi.Napo kesho ilipowadia, Baraza Tukufu lilikaa tena ilikuendeleza ya siku iliyotangulia. Pamoja na kwamba yalikuwako na mengine mengiya kutolea maamuzi na ufafanuzi juu ya mgawanyo sahihi, suala la afya liliendelea kutamalaki kila konaya pande za nchi na ndani ya mioyo na vinywa na vichwa na masikio wa watu,kadhalika miongoni mwa wanabaraza. Nao kila mmoja kwa nafasi yake akangoja kwashauku na kihoro na hamu ya kutaka kusikia ni nini kauli sahihi ya serikali yaoTukufu juu ya hatima ya mgomo wa matabibu.Hata mkuu wa mawaziri alipoijongelea mimbari, mkuu wa Barazaalitoa ruhusa kwa wanabaraza kuelekeza hoja zao kwake-yaani mkuu wa mawaziri.Miongoni mwa wanabaraza walioelekeza vilio vyao na maombi nasala na shutuma na kero za wana wa Kaya zao, alisimama mmoja baada ya ombi lakekupitishwa na mkuu wa Baraza. Naye akamsihi kwa hoja na busara ya kuwa ni kwanini asiseme ‘sasa imetosha' kwa uongozi wake dhaifu juu ya suala la malalamikoya matabibu. Hoja hiyo ikaonekana kuwa unyonya mbele ya upepo mkali wakisulisuli. Hoja iliyoongezewa kasi ya kupeperushwa na mkuu wa Baraza kwakumsihi mkuu wa mawaziri aitupilie mbali.Ni katika muono huo wa kuendelea kuona ni kipi sahihi chakufanya kunusuru hali tete inayofuka mfano wa joto la tanuru, ndipo akasimamayule mwanabaraza ambaye ilimpasa kutolewa nje ya Baraza na askari wa Barazakutokana na kudhaniwa kuvuka mipaka ya kanuni zilizomo ndani ya juzuu laBaraza. Kwa unyenyekevu na hekima akaomba mwongozo kupitia kanuni ya 116 yajuzuu. Naye akaeleza kwa kina na weledi na ufafanuzi na hoja, kuwa, ikimpendezayeye mkuu wa Baraza, atoe mamlaka kwa kamati ya Baraza yenye kuwiwa na kero zajamii za wana wa nchi, ili iweze kutatua tatizo la mgomo wa matabibu.Ikawa yule mwanabaraza akiisha kusema hayo, alikaa akisubirimajibu ya mkuu wa Baraza. Naye kwa mamlaka na kwa mkato akajibu, "Nitatoamaelezo baadae!" Napo muda bila kusonga sana mkuu wa Baraza akasema, tena kwamvumo wa ukali, kuwa yaliyoko mikononi mwa chombo cha kutoa haki hayana budikuachwa humo! Na kwamba si heri kuinukia suala la mhimili mwingine wa mamlaka.Na kama likiwapo jambo lingine kama hilo lenye kuleta uchochezi juu ya sualalililo nje ya mamlaka ya Baraza, na liachwe! Na kwa hiyo haitampasa tena Waziriwa afya kulitolea maelezo. Ndipoaliposema tena kwa kupaza sauti ili wanabaraza wote wamsikie na wafumbe vinywavyao, kuwa KAULI YA WAZIRI HAITATOLEWA! SHAURI LIKO MIKONONI MWA CHOMBO CHAKUTOA HAKI, NA LIMEFUNGWA!Na kwa kauli dhaifu ya mkuu wa mawaziri na inayoashiriakushindwa kutekeleza majukumu na hatimaye kuwashukia wanyonge kwa ghadhabuzilizopotoka, hakika isifike siku. Siku ambayo nao wana wa nchi watasema, LIWALO NA LIWE!
 
"LIWALO NA LIWE" Hili ndilo hitimisho la kauli aliyoitoa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano ya Tanzania wakati akiliambia bunge kwamba serikali atatoa tamko kuhusu mgomo wa madaktari unaoendelea nchini siku inayofuata bungeni.

Aliitamka kauli hiyo kwa ukali sana. Nashindwa kuelewa alimaanisha nini hasa kwa sababu baada ya kauli hiyo kuna matukio fulani yametokea ambayo si ya kawaida, mojawapo linaloendelea sasa hivi ni la kutekwa na kudhuriwakwa kiongozi wa madaktari nchini.

Tukio hili limeambatana na matukio ya hata waliokuwa hawajaanzankugoma nao wameanza. Sasa wana JF naombeni mniambie jinsi mnavyoweza kutafsiri, kwa sababu LIWALO NA LIWE imechukuliwa kama kaulimbiu ya TUCTA na CWT katika maandalizi ya migomo yao ambayo tunaitarajia siku chache za usoni.
 
Nadhani alistahili apigiwe kura ya kutokuwa na imani na wabunge - kaqma wangekuwa makini. Ta\fsiri ya haraka ni kwamba ataamua na kufanya lo lote bila kujali matokeo/athari za uamuzi au vitendo vyake. Na huyo si kiongozi wa kuleta maendeleo na kulinda amani. Ninamuelewa Mbunge Myika kwa kauli za wana CCM kama PM.:crazy:
 
Back
Top Bottom