Mzee sanyagi: Mwanzilishi wa muungano wa tanzania?

Netanyahu

Senior Member
Oct 2, 2008
147
22
Unajua nani alianzisha na kulipeleka wazo la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ?

Katika pekua pekua zangu kwenye majalala ya historia zinakokaa historia takataka za watu maarufu ambao hawako katika maktaba za historia rasmi kwa sababu walikuwa hawaelewani na watawala nilikutana na habari ya ajabu ya mtu aliyeanzisha wazo la muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar .Nikaona labda yaweza kuwa kweli pamoja na kuwa haijaandikwa katika historia rasmi.Wanahistoria mliobobea mwaweza kutusaidia kama si kweli ukweli ni upi?

Taarifa zinasema Mzee aliyeanzisha wazo la Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar anajulikana kama Mzee Sanyagi (Mwasanyagi) ambaye alikuwa Mchumi kutoka kule Iringa ambaye baadaye alikuja kuwa mpinzani fulani hivi ambaye baadaye alirudishwa kwao Iringa na ikawa mwisho wake.Sina uhakika kama bado mzima au alikufa.
Huyo ndiye alimshauri Nyerere Tanganyika iungane na Zanzibar.

Alikuwa akisema kuwa sababu iliyofanya amshauri Nyerere aungane na Zanzibar ni kuwa baada ya Tanzania kupata Uhuru Uchumi wa Tanganyika uliyumba sana mapato ya kodi yalipungua na hivyo kuifanya serikali iyumbe kwenye uendeshaji wa bajeti yake.

Wakati huo Mzee huyo aitwaye Sanyagi aliitwa na Nyerere akamwuuliza nini kifanyike .Mzee huyu akamwambia kuwa Nchi haiwezi kuwa na mapato makubwa ya Kodi ya kudumu na uhakika kama haina wafanyabiashara wazawa.

Wakati huo Nchi ilikuwa haina wafanyabiashara wengi wakubwa wazawa wa Tanganyika lakini bahati nzuri Zanzibar wakati huo ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa wa Kipemba wengi na uchumi wa Zanzibar ulikuwa mzuri mno kupitia wafanyabiashara wa Kipemba.

Hivyo Mzee Sanyagi akapendekeza kuwa ni vizuri Tanganyika iandae sera na mazingira mazuri ya kuvutia sana wawekezaji na wafanyabiashara wa Kipemba wapende kuja Tanzania bara kuwekeza ili Tanzania ivune kodi kubwa toka kwenye biashara zao kubwa.Na hilo ili lifanyike ni vizuri afanye mpango waungane na Zanzibar na kuwaondoa hofu wazanzibar awambie kuwa wao wako huru na salama zaidi kuishi Tanganyika kuliko Zanzibar ambako walikuwa wakiburuzwa na Karume.

Vikao vikaanza vya namna ya kupora walipa kodi wa Zanzibar ambao ni wafanyabiashara wa Kipemba ili wahamishiwe Tanganyika. Mikakati ikaundwa namna ya kumrubuni Karume akubali muungano.Ikaonekana kuwa kuna maeneo kama ulinzi,fedha,n.k ambayo yangeweza kutumiwa kumrubuni Karume akubali kuufanya huo muungano ukubalike.Karume akakubali muungano na kuchanganya udongo akiwa hajui wenye akili wa Tanganyika walichokuwa wakipanga.

Mara baada ya kuchanganya udongo na muungano kukamilika Tanzania bara wakaanza kazi ya kuvutia wapemba walipa kodi wahamie Tanzania Bara kwa mikakati ya sra za kuvutia sana.Kweli wapemba wengi wakaamua kuhamia Tanzania bara na kuwekeza Vitega uchumi vingi vya nguvu vinavyozalisha kodi kubwa kuliko Zanzibar.Tanzania Bara ikaanza kufaidi muungano kupitia kodi za wafanyabiashara wapemba na mambo yakaanza kuwa si mabaya kwenye bajeti ya serikali ya Tanzania bara.

Nyerere akaanza kuufurahia muungano kwa kodi zile zilizokuwa zikiingia na akawa mkali sana kwa yeyote aliyetaka kuvunja muungano ila alikuwa hataki kueleza siri hii kuwa Tanzania inafaidika nini kwa kuungana na Zanzibar.Siri hiyo alibaki nayo yeye moyoni na wateule wake wachache akiwemo Mzee Sanyagi aliyeanzisha hilo wazo.

Sasa hivi Tanzania ina wafanyabiashara wazawa wengi nje ya wapemba je kama Zanzibar wanataka muungano uvunjike watu wa Tanzania bara mnasemaje uvunjike au usivunjike? Au tuendelee kuwanung`ang`ania tuendelee kuvuna kodi kwa wapemba kama alivyomshauri Mzee SANYAGI mwanzilishi wa wazo la muungano wa Tanganyika na ZANZIBAR.

Tanzania ya leo tunawahitaji watu kama Mzee Sanyagi .Japo historia zao zilifichwa jalalani kwa kuwa hawakuimba wimbo wa kumsifu mtawala maisha yao yote na wakaishia maisha duni bila historia kuwakumbuka lakini walau walifanya kitu ambacho kilisaidia taifa vile walivyoweza hiki nilichookota jalalani.

Iko haja ya kufuatilia watu wale waliopinga serikali na waliowekwa kwenye majalala ya historia kujua walisimamia nini twaweza pata kitu cha maana kwao kuliko kwa hawa waimbao zidumu fikra za mtawala wakati vichwa vyao ni vitupu viwazavyo ufisadi na kujikomba toka jua linapochomoza hadi linapotua.

Naishia hapo nawahi naenda jalala lingine kuona kama nitaokota historia takataka ingine kama nitaipata maana kuna msemo usemao hata jalani mtoto wa maskini aweza okota mkate uliooza akala.
 
muungano wa tanganyika na zanzibar,uliletwa na covert operations za CIA,ili kuprevent what was then believed zanzibar becoming another cuba
 
[I said:
son of alaska;300098]muungano wa tanganyika na zanzibar,uliletwa na covert operations za CIA,ili kuprevent what was then believed zanzibar becoming another cuba
[/I]

Son of Alaska

Unachotaka kutuambia ni kuwa Nyerere alichoangalia kufanya muungano si kuangalia Tanganyika itafaidika na nini na muungano huo bali CIA na Wamarekani watafaidi nini ? Tufafanulie kidogo mheshimiwa.
 
Unajua nani alianzisha na kulipeleka wazo la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ?

Katika pekua pekua zangu kwenye majalala ya historia zinakokaa historia takataka za watu maarufu ambao hawako katika maktaba za historia rasmi kwa sababu walikuwa hawaelewani na watawala nilikutana na habari ya ajabu ya mtu aliyeanzisha wazo la muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar .Nikaona labda yaweza kuwa kweli pamoja na kuwa haijaandikwa katika historia rasmi.Wanahistoria mliobobea mwaweza kutusaidia kama si kweli ukweli ni upi?

Taarifa zinasema Mzee aliyeanzisha wazo la Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar anajulikana kama Mzee Sanyagi (Mwasanyagi) ambaye alikuwa Mchumi kutoka kule Iringa ambaye baadaye alikuja kuwa mpinzani fulani hivi ambaye baadaye alirudishwa kwao Iringa na ikawa mwisho wake.Sina uhakika kama bado mzima au alikufa.
Huyo ndiye alimshauri Nyerere Tanganyika iungane na Zanzibar.

Alikuwa akisema kuwa sababu iliyofanya amshauri Nyerere aungane na Zanzibar ni kuwa baada ya Tanzania kupata Uhuru Uchumi wa Tanganyika uliyumba sana mapato ya kodi yalipungua na hivyo kuifanya serikali iyumbe kwenye uendeshaji wa bajeti yake.

Wakati huo Mzee huyo aitwaye Sanyagi aliitwa na Nyerere akamwuuliza nini kifanyike .Mzee huyu akamwambia kuwa Nchi haiwezi kuwa na mapato makubwa ya Kodi ya kudumu na uhakika kama haina wafanyabiashara wazawa.

Wakati huo Nchi ilikuwa haina wafanyabiashara wengi wakubwa wazawa wa Tanganyika lakini bahati nzuri Zanzibar wakati huo ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa wa Kipemba wengi na uchumi wa Zanzibar ulikuwa mzuri mno kupitia wafanyabiashara wa Kipemba.

Hivyo Mzee Sanyagi akapendekeza kuwa ni vizuri Tanganyika iandae sera na mazingira mazuri ya kuvutia sana wawekezaji na wafanyabiashara wa Kipemba wapende kuja Tanzania bara kuwekeza ili Tanzania ivune kodi kubwa toka kwenye biashara zao kubwa.Na hilo ili lifanyike ni vizuri afanye mpango waungane na Zanzibar na kuwaondoa hofu wazanzibar awambie kuwa wao wako huru na salama zaidi kuishi Tanganyika kuliko Zanzibar ambako walikuwa wakiburuzwa na Karume.

Vikao vikaanza vya namna ya kupora walipa kodi wa Zanzibar ambao ni wafanyabiashara wa Kipemba ili wahamishiwe Tanganyika. Mikakati ikaundwa namna ya kumrubuni Karume akubali muungano.Ikaonekana kuwa kuna maeneo kama ulinzi,fedha,n.k ambayo yangeweza kutumiwa kumrubuni Karume akubali kuufanya huo muungano ukubalike.Karume akakubali muungano na kuchanganya udongo akiwa hajui wenye akili wa Tanganyika walichokuwa wakipanga.

Mara baada ya kuchanganya udongo na muungano kukamilika Tanzania bara wakaanza kazi ya kuvutia wapemba walipa kodi wahamie Tanzania Bara kwa mikakati ya sra za kuvutia sana.Kweli wapemba wengi wakaamua kuhamia Tanzania bara na kuwekeza Vitega uchumi vingi vya nguvu vinavyozalisha kodi kubwa kuliko Zanzibar.Tanzania Bara ikaanza kufaidi muungano kupitia kodi za wafanyabiashara wapemba na mambo yakaanza kuwa si mabaya kwenye bajeti ya serikali ya Tanzania bara.

Nyerere akaanza kuufurahia muungano kwa kodi zile zilizokuwa zikiingia na akawa mkali sana kwa yeyote aliyetaka kuvunja muungano ila alikuwa hataki kueleza siri hii kuwa Tanzania inafaidika nini kwa kuungana na Zanzibar.Siri hiyo alibaki nayo yeye moyoni na wateule wake wachache akiwemo Mzee Sanyagi aliyeanzisha hilo wazo.

Sasa hivi Tanzania ina wafanyabiashara wazawa wengi nje ya wapemba je kama Zanzibar wanataka muungano uvunjike watu wa Tanzania bara mnasemaje uvunjike au usivunjike? Au tuendelee kuwanung`ang`ania tuendelee kuvuna kodi kwa wapemba kama alivyomshauri Mzee SANYAGI mwanzilishi wa wazo la muungano wa Tanganyika na ZANZIBAR.

Tanzania ya leo tunawahitaji watu kama Mzee Sanyagi .Japo historia zao zilifichwa jalalani kwa kuwa hawakuimba wimbo wa kumsifu mtawala maisha yao yote na wakaishia maisha duni bila historia kuwakumbuka lakini walau walifanya kitu ambacho kilisaidia taifa vile walivyoweza hiki nilichookota jalalani.

Iko haja ya kufuatilia watu wale waliopinga serikali na waliowekwa kwenye majalala ya historia kujua walisimamia nini twaweza pata kitu cha maana kwao kuliko kwa hawa waimbao zidumu fikra za mtawala wakati vichwa vyao ni vitupu viwazavyo ufisadi na kujikomba toka jua linapochomoza hadi linapotua.

Naishia hapo nawahi naenda jalala lingine kuona kama nitaokota historia takataka ingine kama nitaipata maana kuna msemo usemao hata jalani mtoto wa maskini aweza okota mkate uliooza akala.

Source pls
 
nyerere,alikuwa ndio kwanza kaibuka,cold war ilikuwa inapamba moto,A BABU,cia walihofu akiichukua zanzibar,basi sphere ya influence ya mrusi itapanuka na zanzibar itaanza kumsumbua usa kama alivyokuwa akifanya mcuba.hivyo basi it did not take much for the CIA to convince nyerere-ndio maana huu muungano una utata sana
 
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kazi ya CIA na rekodi zipo. Ofisa wa CIA aliyechora na kusimamia mpango mzima aliitwa Frank Carlucci. Sheria ya kuanzisha muungano iliingia kwenye rekodi kama sheria iliyopitishwa kwa kasi kuliko zote Tanzania, ambapo muswada uliandaliwa, kujadiliwa, kupitishwa na kusainiwa katika muda usiozidi masaa 36! (siku moja unusu!)
 
Kithuku tumwagie hizo rekodi mkuu manake wengine hatujaziona bado au kama vipi tuelekeze wapi pa kuzipata manake mkuu hapo anasema zake kaokota jalalani,wewe unasemaje??
 
Soma kitabu "Mwalimu: The Influence of Nyerere" kilichoandikwa na Colin Legum na G. R. V. Mmari (James Currey Publishers, 1995). Soma maneno ya Frank Carlucci mwenyewe kwenye kitabu hicho ukurasa wa 173:

"Nyerere had to do something about the Zanzibar problem. I don't know for a fact whether hecame up with the idea himself or whether we gave him the prescription. Whether our urging him to do something about Zanzibar had an effect on him......I do know the situation in Zanzibar was one of continuing deterioration. In the absence of action from Tanganyika, the place would have been controlled by the communists"

Hiyo "we" kwenye nukuu ya Carlucci ni CIA. Carlucci baada ya kufanikisha mission hiyo na nyingine nyingi alipanda ngazi hadi kuwa mkurugenzi wa CIA na baadae waziri wa ulinzi wa Marekani.

Soma pia hii journal article ya Amrit Wilson (2007),AbdulRahman Mohamed Babu: Politician, Scholar and Revolutionary. Journal of Pan African Studies 1(9):8-25. Hii nakuwekea link yake hapa chini usome mwenyewe, sihitaji kukutolea nukuu yoyote. Natumaini zitakupa mwanga.
http://www.jpanafrican.com/docs/vol1no9/AbdulRahmanMohamedBabu.pdf
 
Hiyo link ya journal naona haijakaa vizuri, nakuwekea tena hapa:
[media]http://www.jpanafrican.com/docs/vol1no9/AbdulRahmanMohamedBabu.pdf[/media]
 
Kithuku,
Hiyo nukuu ya Carlucci inaonyesha mashaka vile vile. Hajui kama ni wao (CIA) waliokuja na wazo hilo au kama Nyerere alikuwa nalo kichwani mwake kutoka mwanzo. Walichofanya CIA ni kucheza mchezo wa kuhakikisha kuwa lengo hilo linafanikiwa, lakini sidhani walipandikiza wazo kichwani mwa Nyerere/.
 
Hapana, anajua vizuri sana kuwa ni wao! Ni jasusi huyu anacheza na maneno, lakini ukisoma kitabu chote utapata mengi zaidi. Ziko pia sources nyingine zinazothibitisha jambo hili.
 
kwenye post hapo juu nimemaanisha jasusi anaecheza na maneno kwenye mahojiano ni Carlucci, si huyu Jasusi wa JF!
 
Back
Top Bottom