Mzee Pinda linda heshima yako - Jiuzulu tu

Elisha Ray

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
323
94
Kwa kweli naona kama Mh. Pinda umewekwa kwenye wakati mgumu katika position yako ya PM. Kwani kama ni kweli rais anasema 'ni upepo tu utapita' kweli ana uchungu na nchi hii? Kama waliompigia kura wanamwambia atoe baadhi ya mawaziri wabovu nae hataki hata kwa ushauri wa PM basi ni kweli haambiliki na PM bora kama wewe si mmoja wao na una uchungu na nchi hii uachie ngazi ujitofautishe nao na iwe rahisi kwako pia upinzani ukichukua nchi upate walau kazi wakati hawa wengine wakiwa jela huku wamefilisiwa mali walizoiba!!!

Wadau mnasemaje?
 
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari leo...ni vyema Mtoto wa Mkulima aliuzului tuu,hakuna sababu yakupambana na Watoto wa Wafanyabiashara na Mafisadi....Amezongwa na ukuta mnene sana wa chain of decision....Abakie mbunge tuu...Ingelikua ni mie najiuzulu Presha ya nini
 
Mbunge wa jimbo la jirani na la kwake ameonyesha ujasiri kwa kutetea maslahi ya wananchi. Pinda jifunze kwa mbunge wa Nkasi. Kibaoni hawakushauri?
 
ni wakati na hali ngumu kwa mtoto wa mkulima - inanikumbusha wimbo wa Dar Jazz usemao "ntawaachia wenzangu wakae"
 
Mzee Pinda,huu ndio wakati wa kuionyesha dunia ya kwamba,ulikuwa msaidizi wa Hayati J.K.Nyerere kwa miaka saba,hivyo upuuzi kwako mwiko,JIUZULU!
 
Ni kweli ni bora aanchie ngazi ili nae amtege baba Mwanaasha kuunda baraza lingine litakalomsaidia kukinusuru chama chake. Kuendelea kulia lia bungeni hakusaidii kabisa.
 
Pinda,Pinda,Pinda uliingia kwa mkwara wa kulia na sijui kama unakumbuka maneno uliyomwambia ALLAH, ( kwamba ukila au kusimamia rushwa... )jiuzulu mtu wangu,tofauti na hapo utakua kama kenge anayekimbilia mtoni kujikinga na mvua.
 
Pinda steap aside..no way out.JUST ADRESS IT TODAY COZ KESHO AKINA TUNDU LISSU WATAKUWAMBA MSALABANI,ZEGE LAKO HILI.KICHEKO.COM KAKUSALITI.
 
viongozi wetu hawashauriki,yaani wao ni kama wana hati miliki za kuongoza,kumbe busara ni kujitenga na makandokando yaliyopo.kama unashauri wenzako au mkuu wa nchi hawakuelewi au hakuelewi ya nini kuendelea kulazimisha kuwa mshauri wake wakati hayupo tayari kushauriwa nawe.jiondoe mwenyewe bila shuruti mh.pinda.
 
Sasa nimegundua kumbe JK ndiyo anataka kumtoa kafara waziri mkuu wake. "upepo utupita?". Hata Richmond ilipoanza ilikuwa upepo unaopita lakini uliangusha miti mikubwa. Pinda kama unataka ubaki safi,bora ukimbie kabla upepo haujaanza safari.
 
Achen kukurupuka, kujiuzuru kwa lowasa ni tofauti na hivo mnavofikiri kuwa na pinda nae ajiuzuru, maamuzi hayo yataipeleka nchi pabaya sana.
 
pinda anahofia usalama wake, lakini keshazeeka, kama anaipenda nchi, ni bora a-step aside kufa nini bana!!!!?
 
Ili kulinda heshima bora waziri wetu mkuu akajiuzulu Lowasa alijiuzulu na leo anakula pensheni anaitwa mstaafu, pinda atapata heshima zaidi kuliko kupambana na kina JK, bora afe kwa sumu kuliko kufa kwa presha na mawazo huku roho na damu ya watanzania wanaodhulumiwa na kunyanyasika ikiwa mikononi mwake, Kila la heri Mh Mizengo Kayanza Peter Pinda ktk kufanya maamuzi magumu..
 
Dear mr PM,tunaomba ulinde heshima yako na ututendee haki sisi watanzania wenzako,twakuomba ujiuzulu kesho ili ****** aaibike.

Nashindwa kukuelewa kama kweli miaka yako saba kuwa msaidizi wa mwalimu haya ndio uliojifunza.
 
Back
Top Bottom