Mzee Paul Kimiti aaga Rasmi Bungeni kwa mbwembwe

Regia Mtema

R I P
Nov 21, 2009
2,970
864
Leo katika kikao cha Bunge cha jioni wakati wabunge wakichangia hoja ya Uchumi Mheshimiwa Paul Kimiti ameaga rasmi Bunge kwa kujifagilia kwa mafanikio aliyoyapata.Kimiti ameleza kuwa maekuwa Mbunge kwa kipindi cha miaka 30 na wakati anaingia Bungeni alikuwa ana ajenda kuu nne kwa wananchi wake wa jimbo la Sumbawanga Mjini.Amedai kuwa agenda zake zilikuwa ni Elimu,Afya,Barabara na Maji. Amejifagilia kuwa ameweza kutekeleza ajenda zote kwa kiwango cha ufanisi.Amedai alipokuwa akiingia Bungeni Halmashauri yake ilikuwa ina shule nne(4) tu za Sekondari lakini sasa zimefikia ishirini na tano(25) hivyo anajipongeza sana kwa hilo. Hapa mimi ndipo paliponigusa hayp mengine ya Afya,Barabara na Maji sitayaongelea ninaongelea hili la Elimu.

Hoja zangu ni hizi..
1. Kwa kipindi cha miaka 30 kuongeza shule 21 ni kitu cha kujivunia?shule zenyewe ambayo majengo yake yako chini ya kiwango.Give me a break Kimiti,21 tu unajisifia.Je yeye kwa kipindi cha miaka hii 30 ameongeza nyumba ngapi.miradi mingapi,magari mangapi? na kipato chake kimependa kwa kiwango gani?naamini atakuwa amefanikiwa kwa almost 99% ya maratajio yake kiuchumi n.k.Je hayo mafanikio yake binafsi yako proportional na haya ya shule 21?

2. Shule hizi 21 alizoongeza kwa kipindi cha miaka 30 zina walimu wa kutosha?vifaa vya kufundishia na kujifunzia je?zina maktaba?madarasa yanaubora kiasi gani?

3.Tangu kuanzishwa kwa shule hizi ni wanafunzi wangapi wameenda kidato cha tano na sita kwa kiwango cha division one na two?

Mwisho,nimefurahishwa na uamuzi wake wa kujitoa mwenyewe kwenye sistimu bila kusubiri sistimu imteme..Ningefurahi zaidi kama ningemsikia na Hon Malecala naye akiaga Bungeni kwamba hatagombea tena,sorry kwa nitakaowakwaza kwa kusema hili..
 
Swali lingine la kujiuliza ni je kati ya hizo shule 21 ni ngapi zime jengwa kwa bidii yake yeye kama mbunge au hata mwananchi? Maana siyo kile shule inayo jengwa ni kwa jitihada za mbunge. Zingine una kuta wakazi wameamua kuchanga wenyewe, zingine zina jengwa na mashirika mbali mbali nk. It's sad miaka 30 hicho ndicho anacho jivunia. Kama hizo ndizo standards zetu basi kwa miaka yetu karibia hamsini ya uhuru Tanzania tume fanikiwa sana.
 
Mzee wetu huyu hayumo kwenye orodha ya wezi wa mali za nchi hii. Alikuwa mtu wa karibu wa Mwalimu.
 
Kuna Shirika fulani la kidini huyu mzee yumo - He looks like a "devouted christian": Kuna siku tulitoka wote OT JHB alinihubiria "neno" mpaka tunafika JN: Tulikuwa kwenye SAA - tulipoteremka nikamuuliza "lakini mbona muda wote (it was 2008) upo kwenye serikali na wenzio lakini ATCL ndo tunaizika sasa - mmelifanya nini shirika hili au mnapenda sana kupanda ndege za watu? - Alicheka tu na kuchukua taxi na kuondoka.
 
he is one of the remaining smart heads legacy ya mwl. nyrerere angalia hotuba ya mwl, mei mosi 1995 pale uwanja wa sokoine mbeya ambapo kwa muda huo mzee kimiti alikuwa RC mwl aliwachana wagombea watarajiwa wa urais akiwamo JK na EL kwa wakati huo na kiukweli mzee huyu amebaki kuwa mfuasi wa kweli wa falsafa ya mwl, alimsikia na kumfuata sio mwizi na wala sio tajiri wa kutisha..
 
Nawashukuru mliotupatia account ya Mzee wetu Kimiti; kuna tetesi kuwa ilikuwa aukwae u PM wakati wa ngwe ya kwanza ya Mkapa..........nani anazo habari kamili?
 
Swali lingine la kujiuliza ni je kati ya hizo shule 21 ni ngapi zime jengwa kwa bidii yake yeye kama mbunge au hata mwananchi? Maana siyo kile shule inayo jengwa ni kwa jitihada za mbunge. Zingine una kuta wakazi wameamua kuchanga wenyewe, zingine zina jengwa na mashirika mbali mbali nk. It's sad miaka 30 hicho ndicho anacho jivunia. Kama hizo ndizo standards zetu basi kwa miaka yetu karibia hamsini ya uhuru Tanzania tume fanikiwa sana.

Hili nalo neno..Hivi ndio vitu vya muhimu vya kuzingatia.
 
hahaha! Kimiti yuko safi, ila fagio alilotumia kujifagilia limemwangukia.

All the best! hata Malecela angeng'atuka tu hana msaada.
 
Nawashukuru mliotupatia account ya Mzee wetu Kimiti; kuna tetesi kuwa ilikuwa aukwae u PM wakati wa ngwe ya kwanza ya Mkapa..........nani anazo habari kamili?
Mkapa hakupenda Waziri Mkuu ambaye angeliweza 'kumfunika' kwa utendaji mahiri uliojaa uadilifu kama ambavyo Mzee Kimiti angelifanya.
 
hahaha! Kimiti yuko safi, ila fagio alilotumia kujifagilia limemwangukia.

All the best! hata Malecela angeng'atuka tu hana msaada.

Kabla hamjaendelea kuwakandia hawa wazee, inabidi mketi chini kwanza na kujua historia zao na mengi ambayo wamelifanyia taifa hili including wellbeing yenu nyie mnaowakandia. Unaweza kumuona Mzee Malecela hana msaada lakini huwezi kuelewa behind scenes amefanya ama amechangia mangapi katika vikao muhimu vya Bunge na CCM kuepusha majanga ambayo yangeliweza kuliletea taifa letu madhara makubwa.

Wengi wenu humu mnapo soma ama kusikiliza hotuba za Mwalimu Nyerere kwa mara ya kwanza huwa mnashangaa kuona jinsi mzee huyu alivyokuwa na busara nyingi na alivyoipenda nchi na wananchi wake kwa moyo wake wote. Hawa wazee waliokuwa na Mwalimu ndio walioijenga nchi hii kwa moyo bila kuwa na tamaa yoyote ya kujilimbikizia mali tofauti na ulivyo uongozi wa sasa iwe ni uongozi wa juu nchini, uwaziri, ubunge, udiwani hata ujumbe wa nyumba kumi! Wazee hawa wangeliamua kuwa wabadhilifu na wapenda mali nadhani leo nchi hii ingelikuwa na wananchi wengi wanaozaliwa, kukulia na kufia barabarani ama kwenye viambaza vya nyumba za matajiri mjini na vijijini. Tuwape heshima wanayostahili tafadhali, hata wakitaka kuendelea kukalia viti hadi siku ya kuondoka duniani wanastahili!!
 
Hongera Kimiti! Nadhani Malecela, Makweta, Mzindakaya na wale wengine wenye zaidi ya miaka 20 wapishe wengine!
 
Hongera Kimiti! Nadhani Malecela, Makweta, Mzindakaya na wale wengine wenye zaidi ya miaka 20 wapishe wengine!

Nakubaliana na wewe Mkuu Masanilo.Wengine kama Mzindakaya,Makweta wao wameaga,tatizo ni kwa ndugu yetu Malecela,kagoma kuachia ngazi.
 
Internet Explorer Wallpaper.jpg

Kong'oli link hapo juu
 
Mkapa hakupenda Waziri Mkuu ambaye angeliweza 'kumfunika' kwa utendaji mahiri uliojaa uadilifu kama ambavyo Mzee Kimiti angelifanya.
Na kama alikuwa karibu na Mwalimu Mkapa asingependa kumpa mtu kama huyo uwaziri mkuu.
 
Mwisho,nimefurahishwa na uamuzi wake wa kujitoa mwenyewe kwenye sistimu bila kusubiri sistimu imteme..Ningefurahi zaidi kama ningemsikia na Hon Malecala naye akiaga Bungeni kwamba hatagombea tena,sorry kwa nitakaowakwaza kwa kusema hili..

GS,
Sorry for what and for who?
Unavyosema ni sawasawa si akina Kimiti na Malecela tu, hata hicho chama chenyewe walichopatia tiketi ya ubunge kimeshindwa kama walivyoshindwa wabunge wenyewe, miaka zaidi ya 40 ya utawala wa CCM wananchi wengi bado masikini wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, wote waondoke!
 
Nakubaliana na wewe Mkuu Masanilo.Wengine kama Mzindakaya,Makweta wao wameaga,tatizo ni kwa ndugu yetu Malecela,kagoma kuachia ngazi.

naomba kukusahihisha kwenye BOLD hapo mzee makweta hajaaga na amesema anagombea tena kumbuka kauli yake kuwa ubunge sio kwa vijana na walemavu na akaenda mbali akasema yeye kazi anayojua ni ubunge tuu sasa asipogombea unataka akafanye kazi gani.
 
Hivi Mheshimiwa mamaa Anna Abdallah ana miaka mingapi Bungeni? jana nimesikia akidai kuwa nchi haiwezi kuongozwa na vijana pekee bali lazima kuwepo na wazee! Alikuwa akijibu 'dongo' la mheshimiwa Zitto aliyetaka vijana wapewe nafasi zaidi na wazee waachie ngazi! Inaelekea mama bado hajachoka na Bunge! Hivi si alishapitia ukuu wa mkoa pia?
 
naomba kukusahihisha kwenye BOLD hapo mzee makweta hajaaga na amesema anagombea tena kumbuka kauli yake kuwa ubunge sio kwa vijana na walemavu na akaenda mbali akasema yeye kazi anayojua ni ubunge tuu sasa asipogombea unataka akafanye kazi gani.

Nimekupata Mkuu!Noted..
 
hahaha! Kimiti yuko safi, ila fagio alilotumia kujifagilia limemwangukia.

All the best! hata Malecela angeng'atuka tu hana msaada.

Hii nimeikubali wazee wote na wabunge ambao wameshaaka zaidi ya vipindi viwili au vitatu na zaidi ingekuwa makini na kupendeza zaidi km wote wangeachia ngazi,km hujaweza kufanya mabadiliko kwa kipindi cha miaka kumi na tano,wewe utakuwa sio mbunge bora bali bora mbunge....eg Malecela,kina Rita Mlaki,kina Mzee Shelukindo nk wako wengi....
 
Kabla hamjaendelea kuwakandia hawa wazee, inabidi mketi chini kwanza na kujua historia zao na mengi ambayo wamelifanyia taifa hili including wellbeing yenu nyie mnaowakandia. Unaweza kumuona Mzee Malecela hana msaada lakini huwezi kuelewa behind scenes amefanya ama amechangia mangapi katika vikao muhimu vya Bunge na CCM kuepusha majanga ambayo yangeliweza kuliletea taifa letu madhara makubwa.

Wengi wenu humu mnapo soma ama kusikiliza hotuba za Mwalimu Nyerere kwa mara ya kwanza huwa mnashangaa kuona jinsi mzee huyu alivyokuwa na busara nyingi na alivyoipenda nchi na wananchi wake kwa moyo wake wote. Hawa wazee waliokuwa na Mwalimu ndio walioijenga nchi hii kwa moyo bila kuwa na tamaa yoyote ya kujilimbikizia mali tofauti na ulivyo uongozi wa sasa iwe ni uongozi wa juu nchini, uwaziri, ubunge, udiwani hata ujumbe wa nyumba kumi! Wazee hawa wangeliamua kuwa wabadhilifu na wapenda mali nadhani leo nchi hii ingelikuwa na wananchi wengi wanaozaliwa, kukulia na kufia barabarani ama kwenye viambaza vya nyumba za matajiri mjini na vijijini. Tuwape heshima wanayostahili tafadhali, hata wakitaka kuendelea kukalia viti hadi siku ya kuondoka duniani wanastahili!!
acha mawazo mgando wewe, sio kila aliyefanya mema abaki hadi afe, na usilete usultani hapa. nchi si kanisa au msikiti, na huwezi kukuza demokrasia kwa namna hiyo. What if itakua better without huyo malechela....Kumbuka hakuna marefu yasiyo ya ncha

.
 
Back
Top Bottom