Mzee maarufu wa Mailisita Joachimu Lakindi kwayu afariki dunia

richone

Senior Member
Apr 3, 2012
146
35
Mzee huyu aliwahi kutinga ikulu miaka ya 1990 akaishi Ikulu wakati akiwasilisha lalamiko lake la kunyang'anywa ardhi yake kule shiri njoro(mailisita)
Alitikisa tena vyombo vya habari miaka ya 2001 pale alipoamua kujitengenezea jeneza lake na kulipeleka nyumbani kwake akisema hayuko tayari kumbebesha mtu gharama zozote za kumzika.
Vitukoo vya mzee huyu vilitia fora pale alipoamua kujenga nyumba juu ya mti na akawa anaishi huko kama nyani. watoto walipomuomba wamjengee nyumba alikataa akasema ataishi juu ya mti huku akisema kuna kontena alilokuwa amemuagiza Padre Urio msaidizi wa askofu wa jimbo katoliki la moshi amtengenezee ambapo padre urio alisema litakmilika muda sii mrefu.
ninawapa pole watoto,wajukuu na wale wote wanaoishi Shiri njoro. namkaribisha kikwete ahudhurie maziko kwani ndio tupo kwenye maandalizi ila tunamuomba asiufanye msiba huu kuwa wa kitaifa kama anavyokurupuka.
 
Back
Top Bottom