Mzee Luhanjo na Balozi H. Mlango

May 4, 2010
77
12
Katibu mkuu kiongozi bwana F. Luhanjo ambaye yuko katika muda wa ziada wa miezi mitatu aliyoongezewa analaumiwa vikali na wafanyakazi wa wizara ya ujenzi kwa harakati zake zake za kuhakikisha katibu mkuu wa wizara hiyo balozi H. Mlango naye pia anaongezewa muda, balozi Mlango ambaye muda wake umeisha karibu mwezi wa pili sasa hakumudu kabisa nafasi hiyo na kuwa mzigo kwa wizara, tunahoji huu mpango wa kuongezea muda wastahafu hawa mantiki yake nini?

Kwani hakuna wazalendo wengine wanaoweza kushika nyadhifa hizo?
 
Kweli inasikitisha vijana walioiva na wazee ambao hawajafikia umri wa kustaafu tupo wengi sana lakini bado wanaendelea na mkakati wa kubebana na umri wao mkubwa wanatakiwa kuondoka na kuacha ofisi kwa mujibu wa sheria.
 
Katibu mkuu kiongozi bwana F. Luhanjo ambaye yuko katika muda wa ziada wa miezi mitatu aliyoongezewa analaumiwa vikali na wafanyakazi wa wizara ya ujenzi kwa harakati zake zake za kuhakikisha katibu mkuu wa wizara hiyo balozi H. Mlango naye pia anaongezewa muda, balozi Mlango ambaye muda wake umeisha karibu mwezi wa pili sasa hakumudu kabisa nafasi hiyo na kuwa mzigo kwa wizara, tunahoji huu mpango wa kuongezea muda wastahafu hawa mantiki yake nini?

Kwani hakuna wazalendo wengine wanaoweza kushika nyadhifa hizo?

Jamani si ujitokeze tu kuwa nafasi unaitaka? swala la wafanyakazi kwa dhama hizi kutomkubali kiongozi hususani katika nafasi hizi za kiutendaji linatokana na vitu vingi lakini kubwa zaidi inapotokea kiongozi yupo makini zaidi na utumiaji wa raslimali na uzibiti wa hali ya juu imekuwa ni sababu kubwa zaidi ya majungu na vita isiyo na sababu.
 
Hakuna vijana wa kufanya kazi wote wababaishaji mkikabidhiwa mtaangusha gari soon na kuuwa abiria.

Labda hizo nafasi serikali ianzishe mpango wa kuzitangaza badala ya uteuzi?!
 
Back
Top Bottom