LE GAGNANT
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 1,241
- 251
Hammie rajab, elvis musiba, ben mtobwa na sasa faraj katalambula. Nani wa kuziba pengo lao katika uandishi wa riwaya?
Huyu jamaa kumbe ni Prof. sasa? Una maanisha Hassan Katalambula? Nakumbuka kuwasiliana naye miaka ya 90 wakati Tanzanet imeanzishwa na kuanza kukutanisha Watanzania dunia nzima.
Katalambula uandishi wake hadi leo nashindwa kujua kama alisoma sana vitabu vya James Hadley Chase au alikuwa akiangalia sana film za kijasusi za USA. Kwa kweli jamaa aliweza sana kutunga kitabu ambacho kingeliweza sana kutokea kwenye mazingira yetu kwa wakati ule. Tofauti na Musiba ambaye aliingiza sana vikorombwezo ambavyo labda kwa leo ndiyo ungelisema vinawezekana na kuwa jambo la kawaida ila si kwa miaka ile.
Nina imani kuna siku atakuja FILM Director mzuri na kutengeneza film yenye hadhi ya KATALMBULA.
Kama jamaa angeliwezeshwa, nisingelishangaa kuwa angelikuwa kachukuliwa Hollywood au Bollywood kuandika film.
I believe Pili Pilipili was and to me is the best Play, yaani ukiisoma ile kitu huwezi weka chini hadi last page, tumepoteza shujaa wengi wa waliobakia ni wale wa kukopi na kupesti hadithi toka kwenye mtandao..... sorry kwa wanaomfahamu vizuri hivi ndie huy huyu alieandika na ile riwaya ya SIRI ya SIFURI???
Nilizoma riwaya zake za Simu ya Kifo na Pili Pilipili. Nakumbuka majarida yake ya Film Tanzania hasa lililokuwa likizungumzia "Kesi ya Wakenda." Faraj Hussein Hassan Katalambullah alikuwa akipenda kupataja kwao Igalula katika hadithi zake hasa akizungumzia safari za treni kwa kuwa Igalula ni mojawapo ya vituo vya reli ya kati.
Pumzika kwa amani ndugu yetu Katalambullah.